Sunday, April 22, 2018

BLOG YA MUZIKI WA ZAMANI HATARINI KUTOWEKA HEWANI

WAPENZI  wa blog hii, nasikitika kuwataarifu kuwa kuna uwezekano mkubwa blog hii isiwe hewani tena baada ya muda mfupi kutokana na masharti ya sheria mpya inayohusu usajili wa blogs iliyoanzishwa Tanzania. Blog hii ni  ilitokana na wazo nililolipata mwaka 2009, baada ya kuona kuwa kuna ukosefu mkubwa wa historia ya muziki wa Tanzania, nami niliona nianzishe blog hii kuchangia katika kukusanya taarifa hapa na pale kuhusu muziki wa Tanzania. Nawashukuru wote ambao kwa namna moja au nyingine walichangia katika kupata taarifa ambazo nimeziandika katika blog hii. Ushauri kwa serikali kupitia Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, wizara ambayo imeleta sheria hii mpya na ambayo pamoja na mambo mengine ina dhamana ya kutunza historia ya muziki wetu, itafute namna ya kuendeleza kazi kama hizi ambazo zinafanywa bure na bloggers ili kuhifadhi historia ya nchi yetu.

No comments: