Friday, April 27, 2018

BAADA YA MIAKA 35, ABBA WAINGIA TENA STUDIO


 Katika maelezo yao waliyoyatoa kupitia ukurasa wao wa Instagram, walisema wazo liliwaijia kujaribu kuona itakuwaje wakiingia tena studio, wenyewe wanasema ni kama bile wanaendelea walipoacha kwani wana nyimbo kadhaa ingawaje tarehe ya kuziachia haijatajwa, japo wimbo wao mmoja I still have faith in you, utaonyeshwa kwenye luninga kuanzia mwezi wa Disemba, kwa kutumia taaluma ya kidijitali ambapo vitakavyokuwa vinaonekana vikifanya onyesho ni vivuli tu vya wanamuziki hawa.
Abba walikuwa na nyimbo nyingi maarufu kama Waterloo, I have a dream na kadhalika. Kundi hili lilisambaratika mwaka 1982.

No comments: