Thursday, March 29, 2018

Download: Stamina ft Chemical x Baraka The Prince_Wivu


Akipangacho Mungu,binadamu huwezi kukizuia/ Aliyekupa ndio aliyeninyima iko siku atanifikiria/ In @therealfidq voice.

Download

Watch & Download: Queen Coco ft Sultan King_Wewe Tu (Official Video)


Watch Here

CAMERA YAKUTWA ZIWANI IKIWA NZIMA BAADA YA KUDONDOKA MIEZI MIWILI ILIYOPITA

Katika hali ya kushangaza huko nchini Marekani, kamera moja ambayo ilipotea baada ya kuanguka ziwani na kukaa huko kwa miaka miwili imepatikana ikiwa nzima.

Inaelezwa kuwa kamera hiyo iliokotwa kwenye ufukwe huko Taiwan ikiwa imefunikwa na matope na uchafu mwingine bila hata kutambulika, lakini ilivyosafishwa ikagundulika kuwa...
bado ni nzima.

Kamera hiyo iliokotwa na wanafunzi pamoja na walimu wao ambao walikuwa kwenye ufukwe huo na tayari wameanza kumtafuta mmiliki wake kupitia mtandao wa Facebook.

MR NICE: SIMKUBALI MSANII YEYOTE NAJIKUBALI MI MWENYEWE


Msanii wa muziki Bongo, Mr. Nice amedai kuwa hamkubali msanii yeyote zaidi yake hata akipewa fursa ya kutaja orodha ya wasanii watano anaowakubali nafasi hizo zote atajipatia yeye.

Muimbaji huyo aliyetamba na style ya Takeu amesema hayo nchini Rwanda alipokuwa akifanya show weekend iliyomalizika. Mr Nice amewataja wasanii...
anaowakubali ni Lady Jaydee, Professor Jay na Jose Chameleone kutoka nchini Uganda.

“Lady Jaydee ni legendari mwenzangu, ni wanamuziki mwenzangu, hivyo hivyo kwa Professor Jay,” amesema.

“Jose Chameleone is Friend of mine ambaye ninaweza nikavua viatu vyangu nikamwambia vaa Jose, dah huyu mtu unajua mimi simkubali mwanamuziki yeyote, namkubali Mr. Nice tu ukiniambia nikupe top five yangu msanii wangu nitakuambia ni Mr. Nice,” amesisitiza.

Mr. Nice kwa sasa anafanya vizuri na ngoma inayokwenda kwa jina la Tuheshimiane.

ADHABU YA ROMA YAFUTWA NA WAZIRI MWAKYEMBE


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Harisson Mwakyembe leo Machi29, 2018 ametangaza kufuta adhabu ya kufungiwa kwa msanii wa muziki Roma Mkatoliki.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam Waziri Mwakyembe amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa Roma Mkatoliki atakuwa huru kufanya shughuli zake za muziki kama ilivyokuwa awali kwa sharti moja la kukamilisha...
taratibu za kujisajili BASATA.

Kwa upande mwingine, Roma Mkatoliki ambaye naye aliongozana na Waziri Mwakyembe amesema kuwa hata kama ameachiwa huru lakini wimbo wake wa kibamia ameviomba vituo vya redio na runinga kutocheza wimbo huo baada ya kufutiwa adhabu yake.

Mwanzoni mwa mwezi Machi serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.

JUX: IKIFIKA WAKATI WATU WATAJUA HATUWEZI KUFICHA UJAUZITO

Jux ameeleza hayo wakati alipokuwa anahojiwa na moja wapo ya chombo cha habari nchini Tanzania baada ya kuenea picha ya mpenzi wake Vanessa mitandaoni ikiwa inamuonesha tumbo lake limeja jaa mithiri ya ujauzito.

"Kiukweli Vanessa hana ujauzito ile ni picha tu, labda siku hiyo alikuwa ametoka kula 'ameshiba' na kupigwa picha vibaya ndio ikatokea hivyo. Lakini hakuna kitu kama hicho, hivyo vitu inabidi...
viende kwa mipango pia lazima mwenzako umshirikishe endapo unataka kufanya hivyo na mkubaliane ili mambo yaweze kwenda sawa", amesema Jux.

Pamoja na hayo, Jux ameendelea kwa kusema "ikifika 'time' watu watajua kwasababu sisi hatuwezi kuficha mambo hata kama sisi hatuto-post lakini inaweza akaja ku-post mtu mwingine kwa kutuona sehemu fulani".

Jux kwa sasa anafanya vizuri kibao chake kipya kilichopewa jina la 'fimbo' aliyoachia siku za hivi karibuni.

NAY WA MITEGO: BASATA HAWAWEZI KUNIPANGIA CHA KUIMBA


#Mwandishi: Kesho Unaachia Ngoma Mpya Kuna Mabadiliko Gani Katika Wimbo Huo Mpya Kuepuka Kufungiwa Tena.? #BabaYaga: Hakuna Mabadiliko Yoyoteeee Naendelea Na Muziki Wangu Ule Ule Coz Mashabiki Wangu Ndo Wanao Upenda Na Ndio Walio Nipokea Nao✊🏿 #Amshapopo

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye anajulikana kuwa miongoni mwa wasanii wabishi linapokuja suala la maadili ya kazi zao, Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego kwa mara ya kwanza amesalimu amri ya serikali na kuwasilisha kazi yake BASATA kukaguliwa, lakini asema sio sababu ya kumzuia kufanya atakalo.
Akizungumza na Nay wa Mitego amesema ameamua kufanya hivyo ili kukwepa lawama za serikali, lakini bado msimamo wake ni uleule kuwa...
hawawezi kumpangia cha kuimba kwenye muziki wake, kwani ndio kitu ambacho mashabiki wake wanakitaka na ndio kinachomuingizia pesa.

“Nimejaribu kufuta utaratibu, nadhani hii ni ngoma ya kwanza kwa mara ya kwanza kabla haijattoka niliwatumia BASATA, nafanya muziki wangu kama nilivyokuwa naufanya nimepunguza baadhi ya vitu, siwezi nikahama kwenye muziki wangu, yaani nitaendelea kufanya muziki wangu ule ule, nimewafikishia wimbo wangu lakini si kwa ajili ya kupangiwa mashairi ya kuimba, sitaki kuanza kuzuiliwa nyimbo zangu”, amesema Nay wa Mitego.

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wasanii kufungiwa nyimbo zake na Nay wa mitego kuwa miongoni mwa wahanga wa mara kwa mara wa tukio hilo.

MIMI MARS :SIWEZI KUOLEWA NA MWANAUME WA KABILA LA WAPARE

Msanii ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya 'Sitamani' chini ya Mdee Music, Mimi Mars amesema hawezi kujihusisha mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwenye kabila la Mpare kwa madai makabila hayo wanatabia ya ubahili na kujisikia. 

Mimi amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuulizwa swali na ripota wa kipindi hicho kuwa anatamani mwanaume wa...
kabila gani ambaye awe naye katika mahusiano au ndoa.

"Kutokana na mimi mwenye kuwa ni Mpare kwa hiyo tabia za wanaume wa kipare ninazifahamu vizuri halafu wanasema mafahari wawili hawezi kukaa zizi moja hivyo najua tutashindwana tu kwasababu wote tunajisikia, wabahili 'so' tukikaa wawili 'type' hiyo mambo yatakuwa magumu", amesema Mimi Mars.

Pamoja na hayo, Mimi ameendelea kwa kusema "inanibidi nitafute kabila ambalo tofauti na mimi ndio maana sitoweza kuwa kabila hilo ila sio kwa ubaya ila mimi mwenyewe tu nimesema sitoweza.

Download: Wakwanza x Vidy Mb_Sikati Tamaa rmx


Download

Watch & Download: Ervixy ft Mwana FA_Text (Official Video)


Watch Here

Download: Orezi_Ijo Wakanda


Download

FAIZA ALLY ATEMA POVU BAADA YA ZARI KUPATA DILI NCHINI TANZANIA


Tokeo la picha la zari dili nono
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Faiza Ally huenda akawa ni moja ya mastaa ambao wamekasirishwa na kitendo cha mwanamama Zari kupata dili la kutangaza nepi za watoto za Soft Care. 

Faiza Ally amesema kuwa ameshangazwa na kampuni hiyo kumtumia Zari kutoka Uganda kwenye matangazo yao ile hali kuna Watanzania wengi na wenye majina ambao...
wangetumika kutangaza bidhaa zao.

“I know this is gonna look bad for somepeople but let me be honest , how stupid Tanzanian can be , mastaa wote watanzania , watu wote watanzania hamkuona hata mmoja anae stahili kupata dili zaidi ya zari ? Ina maana uhitaji bongo umeisha mpaka tuweke watu kutoka nje ?? Kwa nini tunawapa kipa umbele wageni tunajizarau sisi ??? Mlishawahi kuona Uganda na kenya wamempa nani dili wakamuacha wa kwao ?? Eti sasa hivi mganda na mkenya wanapongezan na sisi wote tunaonekana hatukufaaa,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, Faiza amemshangaa mwanamitindo Noel ambaye yeye ndiye aliyehusika kwa kiasi kikubwa kufanya connections hadi Zari kupata dili hilo.
“Noel you know all the Tanzania star na uko karibu hukuona anae faa ? I don’t hate zari but I hate kuona vitu wanavyo stahili kupata watanzania kapata mganda this is no good ! Hakuna nchi duniani utaenda ukaona mgeni anapewa kipa umbele zaidi ya mwenyeji , kiasi mpaka ukiwa unasuburi tax mpaka mwenye nchi apate na wewe ndio unafata,“ameeleza Faiza Ally.

Mtazamo wa Faiza umepigwa na baadhi ya Watanzania waliotoa maoni yao kwenye posti yake wakidai kuwa wanawake wengi wa Tanzania wanautumia umaarufu wao vibaya.

mimahrayvannyWabongo mpo serious na Instagram mganda yupo serious na kazi acha tu apewe.
 
oddy_is_a_baeMarekani yenyew iliongozwa na mkenya sembuse Tz mwachen zari wa watu anastahili
rukkysaidWanaangalia vitu vingi dear,kwa mfano wewe ile post ya mchupi umechoka vile kweli wanaweza kukupa dili km hyo kirahis.
iam_g_mtonyohakuna mtu anayeweza kushawishi kuwa balozi @faizaally_ kwanza hatujui kujiwekea brand alafu tupo cheap sana unafikiri angeenda mbongo hicho kitu kisingejulikana yaana hakuna wa kutustua bongo, wenye makampuni wanatarget za mbali sio za hapo ulizofikiria wewe..! Zari ni brand tosha kama ulikuwa hujui, na anajimudu. SASA wewe kwa mfano ndo kampuni ni yako ungemuita nani aje kuwa barozi!
 
mwana_heriFaiza jamaniii kha eti “hakuna nchi duniani utaenda ukaona mgeni anapewa kipaumbele zaidi ya wenyeji” iiii hamjuwi mambo ya nchi zilizoendelea  HEAD OF THE BANK OF ENGLAND IS A CANADIAN CITIZEN (one of the top jobs available) because he was the best man for the job! First foreigner to run that institution in over 300 years but they had to make changes walisikia how successful alivyokuwa akiwa head of the Canadian bank. Sisi wa chini huku ndio usiseme! Mpaka unajiuliza kwa nini hawakumpa hii kazi mwenzao? Ma employer hapa wanaajiri sana watu wa eastern European sana wakiulizwa kwa nini hamuajiri watu wenu jibu ni moja “they are lazy and have no work ethic” mara leo mgonjwa, mara kesho kafiwa, mara anataka holiday! Muajiri ataweza? Lazima achukuwe mfanyakazi bora! Wewe unaonekana kama ni mpambanaji endelea tu kujitahidi please acha roho ya kwa nini mwenyeezi mungu hapendi, mshukuru tu kwa anachokupa akuongezee na juwa cha mwingine hakiwezi kuwa chako.
 

Jana Machi 28, 2018 Zari alisaini dili hilo nono la kutangaza bidhaa za Softcare Diapers ingawaje bado haijajulikana mkataba huo umemuingizia kiasi gani cha fedha.

DMX AHUKUMIWA MWAKA MMOJA KWENDA JELA

Rapper kutoka nchini Marekani anayeunda kundi la Ruff Ryders, DMX amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi. 

DMX alikamatwa July mwaka jana, kwa mujibu wa CBS rapper huyo anadaiwa kiasi cha dola milioni 1.7 ambapo inasemekana alifungua akauti benki nyingine na kutumia jina jingine ili kukwepa...
kodi.

DXM alikuwa akikabiliwa na mashtaka 14 ya ukwepaji kodi, hata hivyo alilipa faini ya dola 5000,000 za Kimarekani kinyume na hapo angetumikia kifungo cha miaka 44 jela.
Imeripotiwa kuwa DMX ameingiza zaidi ya dola milioni 2.3 kwa mwaka 2010 hadi 2015 lakini msanii huyo alikwepa kulipa kodi. Rapper huyo ni baba wa watoto 15.

TAMMY THE BADDEST: MSANII ILI UUZE UNATAKIWA UWE NA MUONEKANO


Female Rapper Tammy The Baddest amesema muonekana wa msanii mbele ya mashabiki wake una nafasi katika kuuza muziki wake anaofanya. Tammy amesema kuwa msanii si kuandika nyimbo tu na kuingia studio kurekodi bali hata muonekano wake ni kitu cha kuzingatia.

“Msanii kama msanii hasa mtoto wa kike unatakiwa uwe full package, sio unaonekana tu umefanya muziki basi, no!, you have to sale, ili kuuza ni lazima uwe na muonekano mzuri hata kama una shida mtu...
aone mmmh!, kumpa Tammy show kiasi fulani hapana,” Tammy amefunguka.

Ameongeza kuwa muuoneka wake ndio kila kitu kwake japokuwa muda mwingine inakuwa tabu kwake kwa kuwa baadhi ya mashabiki wake hufikiri ana fedha nyingi kitu ambacho si kweli.

MSAMI AMZUNGUMZIA UWOYA NA KUDAI HAMJUI DOGO JANJA


Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja inazidi kugonga vichwa vya habari, safari hii msanii Msamii aliyekuwa mpenzi wa Irene hapo awali anatajwa sana katika ndoa hiyo.

Msanii na Irene wameacha maswali mengi baada ya hivi karibuni kuanza kusifiana katika mitandao kitu ambacho baadhi ya watu wanadai hakileti picha nzuri katika...
ndoa ya Irene na Dogo Janja.

Sasa muimbaji huyo akizungumza na E-Newz, EATV amesema yeye amejua na Irene kwa kipindi kirefu hivyo hata kama mrembo huyo amejuana na mtu mwingine si sababu ya wao kushindwa kuendelea kuwa marafiki.

“Naichukulia kawaida sana, nikikujua leo baada ya miaka mitano mbele ukajuana na mtu mwingine, mkawa na maisha mengine mimi nakujua wewe huyo mtu mwingine simjui,” amesema.

“Kwa hiyo ni vitu ambavyo haviwezi kupotea tu, kwanini nianze kupotezea kwamba yule sasa hivi yupo na fulani sitakiwi kuongea naye, maisha hayako hivyo” ameongeza.

Hata hivyo ameonya kuwa Irene siyo mke wake na anatambua kuwa ni mke wa mtu.

Download: Phyno ft Kranium_One Chance


Download

Watch & Download: Yamungu ft Barnaba_Kaniroge (Official Video)


Watch Here

Watch & Download: Sauti Sol ft Khaligraph Jones_Rewind (Official Video)


Watch Here

Download: Mansu Li ft Chemical_Sina Gari


Download

Watch & Download: Beka Flavour ft Mr. Blue_Tuwe Sare (Official Video)


Watch Here

Download: Nay Wa Mitego (Mr Nay)_Amsha Popo


Download

Download: Harmonize ft Diamond Platnumz_Kwa Ngwaru


Download

Thursday, March 22, 2018

LEO TUNATIMIZA MIAKA 23 TOKA ALIPOFARIKI MARIJANI RAJAB, FAMILIA YAKE KUFANYA HITMA...video ya Marijani akiwa jukwaani


ALHAMISI, Machi 23 mwaka 1995 ndio siku alipofariki  mwanamuziki gwiji mtunzi muimbaji na mpiga gitaa Marijani Rajabu. Alizikwa kesho yake Ijumaa Machi 24 kwenye makaburi ya Kisutu.
Leo hii 23 Machi 2018 familia ya gwiji huyu itafanya hitma kwa kumbukumbu ya marehemu baba yao, nyumbani kwa binti yake mkubwa huko KIjichi.
Historia ya gwiji huyu inaanzia siku alipozaliwa tarehe 3 Machi mwaka 1955, katika eneo la Kariakoo.  Mama yake alikuwa mama wa nyumbani wakati baba yake alikuwa na shughuli za uchapishaji. Maisha yake ya utoto yalikuwa ya kawaida ila alikuwa kipenda sana uimbaji wa Tabu Ley na mwimbaji mmoja wa Guinea Sorry Kandia.  Alisoma shule ya Msingi ikiambatana na elimu ya Madrasa.   Mwaka 1970 Akiwa bado shuleni, utaona umri wake ulikuwa miaka 15 tu,  alijiunga na STC Jazz, ikiwa chini ya mpiga gitaa maarufu wakati huo Raphael Sabuni, kabla ya hapo bendi hii ilikuwa unajulikana kama The Jets. Katika bendi hii Marijani aliweza kutoka nje ya Tanzania kwa mara ya kwanza ambapo alikwenda Nairobi na kurekodi nyimbo zilizotoka katika label ya Phillips., hili jambo la mwanafunzi kusafiri na bendi likaleta shida na kwa vile STC ilikuwa mali ya umma akaachishwa kazi na mwaka1972 alijiunga na The Trippers ya David Mussa ambayo kwa wakati huo ilikuwa inapiga zaidi nyimbo za hoteli na za kukopi na muimbaji wao kiongozi wakati huo alikuwa Ali Rajabu. Hapa ndipo ubora wake ulifunguka haswa na kuweza kuinyanyua Trippers, ambayo sasa ilibadili jina na kuwa Safari trippers kutokana na msimamo wa serikali wakati huo wa kutaka majina ya nyumbani yatumike bala ya yale ya kigeni na  kuwa moja ya bendi maarufu za wakati huo. Waliweza kutoa vibao vilivyopendwa mfululizo na kuweza kuzunguka nchi nzima. Vibao kama Rosa nenda shule, Georgina,Mkuki moyoni, viliweza kuuza zaidi ya nakala 10000 za santuri na hivyo kuwezesha bendi kuwa na vyombo vyake vizuri. Bendi wakati huo ikiwa na wanahisa wanne, ambao kwa bahati mbaya wakati bendi ndio iko juu, wakakosa kuelewana na ukawa ndio mwisho wa bendi hiyo. Marijani alishiriki kutunga, kuimba nyimbo karibu zote za Trippers sanjari na kupiga gitaa kwa baadhi ya nyimbo. Mfano wimbo Olila ambao alipiga rhythm na kuimba.
Mwaka 1976, Marijani na baadhi ya wanamuziki wa Trippers waliamua kuihama bendi na kwenda baadaye kuasisi Dar es salaam International chini ya umiliki wa Mzee Zakaria Ndabemeye ambaye bado yu hai hadi sasa. Baadhi ya wanamuziki hao ni pamoja na Abel Baltazar kutoka Msondo, Kassimu Mponda kutoka Trippers, Abdallah Gama, Joseph Mulenga, Haruna Lwali na George Kessy Omojo waliokuwa wanapiga muziki Magot pale, Said Mohamed kutoka Polisi Jazz, Cosmas Chidumule kutoka Urafiki, Belesa Kakere kutoka Biashara Jazz, Joseph Bernard kutoka Trippers, Ali Rajabu kutoka Trippers, na King Michael Enock kutoka Dar es salaam Jazz. Akiwa Dar Inter alishiriki kutunga nyimbo mbili, Betty na Sikitiko. Hata hivyo kama waswahili wanavyosema mafahari wawili hawakai zizi moja ndivyo ilivyotokea kati yake na Abel Balthazal kiasi cha hatimaye Marijani kufukuzwa ndani ya bendi kutokana na ubishi kuhusu wimbo aliotunga Marijani, kuna maelezo kuwa wimbo ulionekana unafanana na wimbo fulani toka Kongo na hivyo Marijani akatakiwa aubadilishe na ndipo ugomvi ukaanza. Hata hivyo mwishoni mwa mwaka 1978, Marijani alirejeshwa tena kundini kutokana na rundo la wanamuziki wa Dar Inter kuihama bendi kwa kishindo kikubwa na kwenda kuifungua bendi mpya kabisa ya Orchestra Mlimani Park. Aliporejeshwa Marijani alikuja na wanamuziki wengi wapya wakati huo kama akina Christopher Kasongo, Mohamed Tungwa, Mafumu Bilal, Hamis Milambo, Athuman Momba, Mzee Alex Kanyimbo na wengine na kuja na mtindo wa Super Bomboka. Katika kudhihirisha hasira zake kwa Abel, Marijani alimtungia Abel wimbo wa kumnanga ukiitwa Kidudu mtu ambao hata hivyo RTD waliukataa kuurekodi, jambo lililokuwa kawaida enzi hizo kwa redio kukataa wimbo. Sifa nyingine ambayo Marijani alikuwa nayo ni kuibua wanamuziki chipukizi kama alivyofanya mwaka 1983 alipomuibua kutoka Tanga kijana Mkuu Waziri Kungugu Kitanda Milima almaaruf Fresh Jumbe ambaye kwa hakika kabisa Marijani hakujutia kumchukua kijana huyo. Alimuamini kupita maelezo kiasi kwamba wakati mwingine alikuwa akimuachia bendi aongoze na yeye anapumzika nyumbani. Mbali na Fresh, wanamuziki wengine ni kama vile Tino Masinge, Mohamed Mwinyikondo, Juma Choka na wengine kibao. Ni vizuri kuelezea hapa kuwa kadri ya maelezo yake mwenyewe marehemu  baada ya kurekodi Zuena na Mwanameka na nuimbo nyingine katika album hiyo alichoambulia ni malipo ya nauli toka RTD ya sh 2500/- tu. Kilichosikitisha zaidi ni kuwa nyimbo zao tisa ziliuzwa kwa kampuni ya Polygram bila ridhaa yao.
Hata hivyo safari ya Dar International ilikoma mwaka 1987 kutokana na sababu za kawaida za kufa kwa bendi lakini kubwa ni uchakavu wa vyombo. Hata hivyo Marijani aliendelea kufanya muziki na kwa kipindi kifupi amewahi kucheza na Kurugenzi ya Arusha na Mwenge Jazz ambayo alirekodi nayo wimbo mmoja wa Ukimwi na hata kupitia bendi ya Watafiti ambayo hatimae ilikuja kuwa 38.. Mwaka huohuo wa 1987 Marijani na Muhidin Maalim Gurumo waliliongoza kundi la wanamuziki zaidi ya 50 kutunga nyimbo maalum hasa kwa maadhimisho ya miaka 10 ya CCM na 20 ya Azimio la Arusha. Naizungumzia Tanzania All Stars. Aidha mwaka 1994 aliwahi kurekodi zong zing na marehemu Eddy Sheggy. Bendi yake ya mwisho ilikuwa ni Africulture ama Mahepe Ngoma ya Wajanja, iliyokuwa mali ya Rogers Malila, alikokuwa na wanamuziki kadhaa kama akina  Hassan Kunyata, Mgosi na wengine. Bado Marijani ataendelea kukumbukwa na wapenda muziki kote nchini na hata Afrika kwa ujumla kwa nyimbo zake zenye mafundisho na tamu huku akienzi utamaduni na ngoma za kwao Kigoma.

VIDEO YA MARIJANI AKIWA JUKWAANI


Monday, March 19, 2018

CHRISTIANO RONALDO AWA MCHEZAJI WA KWANZA KUFUNGA MABAO MENGI MWAKA 2018

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemfunika nyota wa Barcelona Lionel Messi pamoja na washambuliaji wengine akiwa ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi ndani ya mwaka 2018. 

Ronaldo amefanikiwa kufikisha mabao 21 kwenye mashindano yote tangu mwaka 2018 uanze, baada ya jana usiku kufunga mabao 4 kwenye ushindi wa...
mabao 6-3 iliyopata Real Madrid dhidi ya Girona.

Kwa idadi hiyo ya mabao imemfanya nyota huyo raia wa Ureno kuwazidi nyota kadhaa akiwemo mpinzani wake Lionel Messi mwenye mabao 16 pekee ndani ya mwaka 2018 katika michuano yote.

Kwa upande mwingine Ronaldo amefanikiwa kufunga Hat-trick yake ya 50 katika maisha yake ya soka. Kati ya hizo 44 ameifungia Madrid, 5 timu ya taifa ya Ureno na 1 Manchester United.

Mbio za kiatu cha dhahabu kwa La Liga maarufu (PICHICHI) zinaongozwa na Messi mwenye mabao 25 akifuatiwa na Ronaldo mwenye mabao 22. Mbio za Ubingwa zinaongozwa na Barcelona wenye alama 75 wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye alama 64.

MADEE: SIWEZI KUACHA MUZIKI LABDA NIFE

Rais wa Manzese, Madee amesema hana mpango wowote kwa sasa wa kuachana na muziki kama watu wanavyofikilia katika vichwa vyao, kwa madai muziki ndio maisha yake hivyo atafanya mpaka pale kifo kitakapokuja kumchukua. 

Madee ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) inayorushwa na EATV baada ya msanii huyo kuonekana kusajili wasanii wake wapya kila...
kukicha jambo ambalo lilipelekea baadhi ya watu kudhania pengine Madee ana mpango wa kuacha na kuimba kwa sasa.

"Music my life yaani toka napata akili naanza muziki nikasema nitakuachana na kazi hii labda siku ambayo nitakuwa nimemaliza pumzi zangu 'kufa'. So hata kama ntakuwa sipeleki nyimbo kwenye stesheni mbalimbali, si-rekodi lakini ntakuwa bado ntakuwepo nimeegemea kwenye biashara ambayo itakuwa inahusiana na muziki", amesema Madee.

DIAMOND AWEKA REKODI YOUTUBE AMTUPA MBALI DAVIDO NA WIZKID



Wazungu wanasema ‘Hard work Pays’ huu msemo unajidhihirisha kwa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye kila kukicha anaendelea kuweka rekodi kwenye muziki wake na awamu hii sio views wa kwenye mtandao wa YouTube bali ni Subscribers.

Diamond kwenye akaunti yake ya YouTube tayari amefikisha Subscribers milioni 1+ na kuwa msanii wa muziki wa 8 barani Afrika kuwa na...
Subscribers zaidi ya milioni 1.

Kwa sasa Diamond Platnumz ameungana na wasanii kama Amr Diab kutoka Misri mwenye Subscribers milioni 1.6, Kundi la muziki la Die Antiwoord kutoka Afrika Kusini subscribers milioni 1.8, Dzjoker Chemsou milioni 1.6, Lartiste milioni 2.2, Ilias Tiiw milioni 1.8, Sofia Carlsberg milioni 1.8 .

Wengine ni Tamar Hosny milioni 2.8, shady Srour milioni 2.8 wote kutoka Misri na Saad Lamjarred kutoka Morocco ambaye ndiye msanii wa muziki anayeongoza kwa bara la Afrika kuwa na Subscribers wengi milioni 4.4 .

Kwa upande wa wasanii wengine kutoka Afrika kama Davido, Wizkid, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sarkodie, Alikiba na Cassper Nyovest wote bado hawajafikisha Subscribers milioni 1 ingawaje hao wanatumia mtandao wa VEVO, na akaunti inayoongoza kuwa na Subscribers wengi ni ile ya kundi la PSquare ina subscribers laki 7.

Wiki iliyopita Diamond Platnumz aliachia album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ na tayari imepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki barani Afrika ambapo imeanza kutrend kwenye mitandao ya kununulia nyimbo kwenye baadhi ya nchi kama Burkina Faso.

Watch & Download: Chemical x Centano_Kilwa Yetu (Official Video)


Watch Here

BLACK PANTHER YAZIDI KUWEKA HISTORIA YAINGIZA BILIONI 1.182.5



Filamu ya ‘Black Panther’ imezidi kufanya vizuri katika mauzo yake duniani. Filamu hiyo imetajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 605.4 kwa Marekani ndani ya mwezi mmoja tangu ilipotoka February 16 ya mwaka huu, pia imeingiza kiasi cha dola bilioni 1.182.5 duniani kote. 

Kutokana na kiasi hicho kilichoingiza filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Marvel Studios, imevunja rekodi zilizowahi kuwekwa na filamu kibao kwenye...
box office.

Black Panther ambayo imeongozwa na Ryan Coogler, ilitumia bajeti ya kiasi cha dola milioni 200–210 katika kuitengeneza.

Black Panther imewakutanisha waigizaji kama Chadwick Boseman ambaye ndio staa wa filamu hiyo, Lupita Nyong’o, Michael B. Jordan, Danai Gurira, John Kani na Connie Chiume.

Download: Lulu Diva_Homa


Download

MTI WASABABISHA HASARA YA MAMILIONI SERENA HOTEL

Stori ya kuifahamu leo March 19, 2018 ni ya mti mkubwa ambao umeanguka katika hoteli ya kifahari ya Serena jijini Nairobi siku ya Jumamosi, umesababisha hasara ya Mamilioni ya pesa. 

Mti huo aina ya mkaratusi uliharibu magari ya thamani ya wateja waliokuwa wametembelea hoteli hiyo ya kifahari na kuyaachwa yakiwa katika hali mbaya.
Magari aina ya...
Prado na Mercedes Bens S-Classs ni baadhi ya magari yaliyoharibiwa kwa kuangukiwa na mti huo. 
 

 


 

 


 

 

 


Download: Mgalilaya ft Mesen Selekta_Final


Download

WEMA AWASHTUA MASHABIKI BAADA YA KUPOST UA NA KUANDIKA MANENO HAYA

Ku-trend kwa ua rose jeusi kwenye mitandao ya kijamii imekuwa kama ni kitu cha kawaida kwa watu wengi ambapo huenda kukawa kuna dosari katika mapenzi au kuachana kwa wapendanao basi watu hutumia ua rose jeusi kuwajulisha watu kuwa wameachana au kuna dosari katika penzi.

Baadhi ya mastaa wamekuwa waki-post pia ua hilo jeusi kwenye mitandao ya kijamii endapo panapotokea dosari kwenye mapenzi ila kwa upande wa muigizaji na miss Tanzania 2006 Wema Sepetu imekuwa tofauti ambapo amepost...
ua rose jekundu katika page yake ya instagram.

Wema Sepetu ameandika>>>A Red Rose is a Symbol of Love”  akimaanisha “kuwa ua rose jekundu ni alama ya upendo”




Sunday, March 18, 2018

Watch & Download: Christian Bella ft Malaika Band_Lamba Lamba


Watch Here

Watch & Download: Timbulo_Post (Official Video)


Watch Here

Download: Kikosi Cha Mizinga ft Chege_Urefu Wa Kamba


Download

FASHION: DAD UGLY SNEAKERS ZAZIDI KUSHIKA CHAT


Ukizungumzia kwenda na wakati basi juua kwa sasa raba zilizopewa jina la ‘Dad Ugly Sneakers’ ndio zinahit sana kitaani hasa kwa mastaa.

Katika ulimwengu huu wa mitindo watu wengi wanapenda kwenda na wakati kwa kuvaa vitu vilivyo na majina makubwa. Mfano:- bidhaa za Louis Vuitton, Balenciaga, Zara na nyinginezo. Ila tokea kuingie trend ya viatu vilivyopewa jina...
la ‘Dad Ugly Sneaker’ basi baadhi ya mastaa wameamisha mapenzi yao huko.





Unaweza kuhoji kwa nini viatu vimepewa jina hilo, hii ni kwa sababu ya kuonekano wake kuwa mbaya yaani hauvuti. Watu kama Kim Kardashian, Jade Smith, Bella Hadidi na wengineo wameshatinga raba hizi na ku-roll nazo kitaani.