Showing posts with label HABARI & UDAKU. Show all posts
Showing posts with label HABARI & UDAKU. Show all posts

Wednesday, May 2, 2018

FACEBOOK WATANGAZA KUIMARISHA FARGHA ZA WATUMIAJI WA MTANDAO HUO

Kutokana na kampuni ya Facebook kukumbwa na kashfa ya data za watumiaji wa mtandao huo hivi karibuni, kampuni hiyo imetangaza kufanya mabadiliko kadhaa ii kuimarisha faragha ya watumiaji wa mtandao huo.

Facebook imeeleza kuwa imeongeza faragha kwa watumiaji wake kwa kuweka sehemu ya kufuta historia ya ulichokitafuta katika...
mtandao huo.

Kampuni hiyo ilikumbwa na kashfa ya kutothamini faragha za watumiaji wake huku watumiaji zaidi ya milioni hamsini walidukuliwa katika kipindi cha uchaguzi wa Marekani jambo ambalo Mkurugenzi wa kampuni hiyo Mark Zuckerberg amesema halitajirudia tena.

UWOYA NA DOGO JANJA RAHA TUPU



Msanii wa Muziki wa Bongo Flava, Dogo Janja azidi kuyaanika mapenzi aliyonayo hadharani kwa mke wake ambaye ni Muigizaji,Irene Uwoya.

Dogo Janja kupitia ukurasa wa instagram amepost picha akiwa na mke wake huyo na kuandika caption iliyoandikwa hivi “thamani ya upendo wako ni ya maisha kama maisha yalivyo ni...
upendo.”

Irene Uwoya nae hakukaa kimya alimjibu Dogo Janja na kusema “Nakupenda leo jana na milele.”

WEMA SEPETU AIVUNJIA UKIMYA NGOMA MPYA YA OMMY DIMPOZ



Kimya kingi kina mshindo – Malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameshindwa kuzuia hisia zake kwenye wimbo mpya’Yanje’ wa Ommy Dimpoz ambao amemshirikisha Seyi Shay kutoka Nigeria.

Madam Sepenga amefunguka kuwa muziki wa aina hiyo ndio muziki anaoupenda na kumwambia msanii huyo kwa sasa anaimba...
muziki wa kikubwa.

Kupitia mtandao huo Wema ameadika:
Wanasemaga Kimya Kingi kina MSHINDO mkubwa… Ngoma Imenibamba Hatare… Sijui kwasababu ndo aina ya Mziki ninaopenda… Forever Bae Umemaliza wallahy… This One Is Just Amazing…
.
.
.
Alafu kama naona GROWTH… Yaani Mziki unaoimba now kama wa Kikubwa zaidi… Keep it Up kipenzi… Umeua… Yaani Ni Balaa… Kazi Nzuri umefanya kummezesha Seyi Shai Swahili…
.
.
.
WellDone… You outdid yourself… Proud of You… Ladies & Gentlemen ebu tufanye kutembelea Bio yake @ommydimpoz tukaicheck hii video na tusikilize hii track… Ni Moto wallahy… .
.
.
Naona hii ulituliza kichwa kweli kweli… Wen you talk about Mziki Mzuri sasa ndo huu apa… cc @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz

Friday, April 27, 2018

BABU WA KITAA AKIRI STAREHE NDIYO CHANZO CHA YEYE KUPOTEA KIMUZIKI

Babu wa Kitaa Athibitisha Usemi wa Country Boy
Siku za nyuma kidogo Country Boy alisema kuwa moja ya kitu klichoua muziki wa msanii babu wa kitaa ni kutokana na kuendekeza starehe na kulewa umaarufu na ndio maana ameshindwa kuendelea na muziki wake.

akiongea na radio clouds fm ,Babu wa kitaa alikiri kuwa usemi wa ndugu yake Country Boy ni kweli na kwamba...
alilewa kuwa na jina na wimbo mzuri alikuwa ameutoa mara ya kwanza na ndio maana aliacha kufanya kazi na kuendekeza starehe.

IDRIS SULTAN NA JERRY MURO WAJIBIZANA MTANDAONI KISA MAANDAMANO

Idris Ajibizana na Jerry Muro Katika Mitandao ya Kijamii
Msanii  wa maigizo ya uchekeshaji nchini idris sultan ameingia katika majibizano na aliyekuwa mwanahabari jerry muro baada ya Idris kupost clip iliyokuwa ikisapoti maandamano ya amani yaliyotakiwa kufanyika April 26 na  wananchi waliokuwa wakiiipinga serikali.

Idris katika clip hiyo aliwataka watu kuandamna kwa amani na sio vita wala kusababisha kukosekana kwa amani ndipo Jerry Murro nae...
alipotoa maoni yake kuhusu mawazo hayo ya Idris.

AKOTHEE ATAMANI KUONGEZA MTOTO WA SITA


MSANII mwenye vituko kutoka nchini Kenya, Esther Akothee, kidizaini kama anatamani kuongeza mtoto wa sita baada ya kuacha meseji tata mtandaoni. Mkali huyo wa Ngoma ya Oyoyo ambaye haishi vituko kila kukicha, juzikati aliwapa sapraiz mashabiki wake kwa kusema kuwa endapo atabeba mimba tena, basi lazima kuwe na mkataba.

“Mhmmm vile wanaume walinizalisha na kuniacha hoi! Wakati huu nikibeba mimba ni mpaka contract (mkataba)! Kwanza tuweke account ya mimba! iiitwe...
pregnant account (akaunti ya mimba), post natal account (akaunti ya kujifungua), school fee account (akaunti ya ada ya shule) na holiday account (akaunti ya mapumziko).
Bila hizi Sheria kutimizwa! Nenda uzae nje au ununue mtoto! Hamtujazi ujinga. Angalia fridge pale nyuma! Sasa nikule watoto ama? Na ndiyo nimetoka hospitali na mtoto mgeni.

Baba na lawyer wako wapi?” Aliandika Akothee katika ukurasa wake wa Instagram na kuweka picha akiwa na baadhi ya watoto wake. Akothee mwenye watoto watano, kwa sasa yupo katika uhusiano na meneja wake, Nelly Oaks.

HARMONIZE: SIJAWAHI KUTAMANI KUFANYA KOLABO NA ALIKIBA


Msanii kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka iwapo yupo tayari kufanya kolabo na Alikiba. Muimbaji huyo amesema hajawahi kutamani kufanya kolabo na msanii huyo na si Alikiba pekee bali na wasanii wengi.

“Lengo la Watanzania wote ni kuona ni kiasi gani tunaweza ku-push muziki wetu na kuupeleka mbali. Sijawahi kutamani kufanya kolabo na Alikiba, sijawahi kutamani kufanya kolabo na...
msanii yeyote lakini ikitokea kipindi tunafanya,” amesema.

“Vitu vingine lazima viwepo ili game izidi kupamba moto, so mimi sidhani kama kuna kitu cha ajabu sana,” Harmonize ameiambia Radio Five.

Kwa sasa Harmonize anafanya vizuri na kolabo aliyofanya na Diamond inayokwenda kwa jina la Kwa Ngwaru, huu ni wimbo wa pili kufanya pamoja baada ya ule wa Bado uliotoka mwaka 2016.

DIAMOND AANGUKIA MIKONONI MWA BINTI KUTOKA RWANDA


Mara nyingi mastaa wengi hupenda kufanya mahusiano yao siri hadi pale habari zinapovuja ndipo wanaamua kuweka kila kitu wazi. Mara baada ya kuachana na Zari The Boss Lady kumekuwa na tetesi kuwa Diamond anatoka na msichana maarufu hasa katika mitandao nchini Rwanda, Shaddy Boo.

Tetesi zinaibuka wakati kukiwa na stori kama hizo kuwa Diamond amerudiana na mwanamitindo Hamisa Mobetto ambao walifanya mahusiano yao kuwa siri hadi pale...
walipojaliwa kupata mtoto.

Taarifa zinaeleza kuwa Diamond na Shaddy wamekuwa karibu sana hasa muimbaji huyo anakuwepo nchini Rwanda na kuna baadhi ya picha pamoja na video zinaeleza hilo.

Katika birthday ya Diamond October 02, 2017 iliyofanyika Hyatt Regency Dar es Salaam, Shaddy ni miongoni mwa watu waliohalikwa.

Kama hiyo haitoshi katika show ya Diamond aliyofanya Naivasha, Kenya January 01, 2018 mrembo huyo alikuwepo na kuna baadhi ya picha zinawaosha wakiwa chumbani pamoja na Lukamba ambaye ni mpiga picha wa WCB.



Katika picha hizo mbili za mwanzo utaona Shaddy na Lukamba walikuwa hotel moja ukitazama kwa makini. Taa iliyo juu ya meza inaweza kuthibitisha hilo.

Picha ya juu ni kipindi ambacho bado Diamond alikuwa Kenya, utaona wawili hao kuna mmoja wapo wamevaa ‘sendo’ za mwenzake au wamevaa sare. Hata hivyo mwisho wa siku hizi zote zinabaki kuwa ni tetesi.

Pia inaelezwa kuwa Shaddy alikuwa ameolewa na producer Meddy Saleh kutoka Rwanda na walijaliwa kupata mtoto mmoja kabla ya kutengana.
Picha zaidi za Shaddy pamoja na video zake.

 
Video Player
Video Player
Video Player
Video Player

Tuesday, April 24, 2018

ELYCENT ARUDI KUIPANDISHA BENDERA YA YA HIPHOP NCHINI KENYA



Msanii wa muziki wa rap kutoka nchini Kenya, Mwakima Elisha a.k.a Elycent amezungumzia mabadiliko ya biashara ya muziki na ukubwa wa kukubalika kwa muziki wa hip hop na rap tofauti na ilivyokuwa  kipindi cha nyuma.

Akipiga Story na Dizzim Online juu ya mapokezi ya wimbo wake mpya wa ‘Hip Hop Is Back’ , Elycent amethibitisha kuwa muziki wa kuimba ulifanya vizuri kibiashara ambapo amesema kuwa anachokiona ni...
uwezekano mkubwa wa kila rapa mkali kutengeneza pesa nyingi kwenye muziki wa hip hop kwa sasa.

“Manzeeeee…hip hop is on fire right now na hawa singers they can confess bout that. when I say hip hop is back namaanisha imerudi na ubaya tena kwa ubaya Boss. Vile narogaa na nachora lines na tusiende mbali, lets jump on my new jam ‘Hip Hop Is Back’ can tell that na hiyo hata rappers wa Kenya na East Africa hawabishani”. Amesema  Elycent.

“Nimeachia Song na nashukuru Mungu inajipush bila mimi kutumia nguvu kubwa, so! from there unaweza amini kuwa kwa sasa hivi from hip hop ground tunaweza tengeneza pesa mob ya muziki tofauti na vile ilikuwa kitambo, so kikubwa we need support tu ya mafans”. Ameongeza.

Hata hivyo Elycent anasikika akimtaja Aslay katika wimbo wake huo mpya na alipoulizwa juu ya kutambua soko la muziki la Aslay, aliongeza kuwa moja ya soko la muziki linalokuwa katika mawazo yake pindi anapokuwa akiandaa muziki mzuri kwa mashabiki ni Soko la Tanzania na nchi tofauti zinazotumia na kuelewa lugha ya Kiswahili.

TAKWIMU ZA SIMON MSUVA LIGI YA MOROCCO ZAZIDI KUWA TISHIO

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva amezidi kuchukua headlines katika Ligi hiyo kwa uwezo wake anaoendelea kuuonesha kila mechi anayocheza.

Msuva hadi sasa ndio mchezaji pekee wa kigeni aliye na magoli mengi Ligi Kuu Morocco akiwa na magoli...
9, ila katika TOP 10 ya wachezaji wanaoongoza kwa magoli Ligi Kuu Morocco hakuna raia yoyote wa kigeni zaidi ya Simon Msuva.

Bado game nne Ligi Kuu Morocco msimu wa 2017/2018 iweze kumalizika, ambapo Ligi hiyo inashirikisha timu 16 Simon Msuva hadi sasa amekosa game tatu kutokana na kuitwa Taifa Stars katika ya game 26 Difaa El Jadid ilizocheza na amecheza game 23, mzunguuko wa kwanza amekosa game moja pekee.

CRYSTAL ATOZWA TSH MIL 1.2 BAADA YA KUTOKULA APPLE KWENYE NDEGE

Mwanamke mmoja kutoka nchini Ufaransa amedai kuwa anakabiliana na faini ya Dola za Marekani 500 sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni 1.2 baada ya apple alilokuwa amepewa bure kwenye ndege kukutwa kwenye begi lake.

Mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Crystal Tadlock ambaye alikuwa anasafiri kutoka Paris, Ufaransa kwenda Marekani alipewa apple hilo kama...
kitafunwa kwenye ndege aliyokuwa amepanda.

Anaeleza kuwa aliamua kulitunza ili kulila akiwa amepanda ndege yake inayofuata akiwa anaelekea Denver lakini lilikutwa wakati wa ukaguzi na mawakala wa mipaka wa Marekani aliposhuka kwenye ndege hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Minneapolis.

TAZAMA PICHA 15 ZA MAZISH YA AGNESS MASOGANGE JIJINI MBEYA

Leo April 23, 2018 Mwili wa Agnes Gerald ‘Masogange’ umezikwa rasmi jioni nyumbani kwao Mbalizi Mbeya. Shuka chini kutazama PICHA 15 kutoka katika mazishi...
































VITA YA MIAMBA YA SOKA UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUENDELEA LEO


Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya inatarajiwa kuendelea hii leo siku ya Jumanne kwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali kupigwa dimba la Anfield ambapo Klabu ya Liverpool itakuwa mwenyeji dhidi ya AS Roma.

Liverpool wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya klabu baada ya...
kuing’oa Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1.

 
Wakati wapinzani wao klabu ya AS Roma nao hawakupata bahati ya mtende kuingia kwenye hatua hiyo bali walilazimika kupindua matokeo mbele ya walfe wa soka wa Hispania, FC Barcelona na kuwatoa kwa faida ya bao la ugenini.
 
Rekodi ya Liverpool na AS Roma kabla ya kukutana kwenye mchezo wao wa leo wa klabu bingwa Ulaya.

Mchezo mwengine wa klabu bingwa Ulaya unatarajiwa kupigwa kesho siku ya Jumatano wakati Bayern Munich ikiwakaribisha Real Madrid ya Hispania.

JEBBY AZIKWA WASANII WATOA KIDOGO WALICHO NACHO KUFANIKISHA MAZISHI


Msanii wa Bongo Fleva, Jebby amezikwa katika makaburi ya Mailimbili mjini Dodoma. Jebby ambaye amewahi kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Swahiba’ alifariki dunia hapo juzi April 22, 2018 mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa mdogo Jebby, Hamis Omary msanii huyo hakubahatika kuwa na mke wala mtoto, pia kuna nyimbo zaidi ya...
nne alirekodi ambazo zipo tayari ila hazijatoka.

Wapili kushoto ni msanii Suma G.

Professor Jay ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria katika msiba huo ambapo amekabidhi Tsh. 550,000 zilizochangwa na wasanii kwa ajili ya msiba huo, msanii mwingine aliyehudhuria ni pamoja na Suma G.

MADONNA ASHINDWA KESI YA BARUA YA KUACHWA NA TUPAC



Malkia wa muziki wa Pop kutoka nchini Marekani na mshindi wa tuzo za Grammy, Madonna ameshindwa kesi ya haki ya kulinda kutotolewa kwenye jamii kwa mambo yake binafsi na marehemu Tupac Shakur.

Mwaka jana, mwana mama huyo alikwenda mahakamani kuzuia mnada uuzwaji wa barua ya kutemwa na Tupac. Hata hivyo, jitihada zake hizo...
zimegonga mwamba.

Barua hiyo ambayo iliandikwa na hayati Tupac ambaye alikuwa mpenzi wa Madonna katika kipindi ambacho hakikufahamika, inatarajiwa kuuzwa kwa mnada mwezi Julai mwaka huu.

Tupac aliandika barua hiyo kwenda kwa ex wake huyo Januari 15, 1995 ikiwa ni miezi 18 kabla ya kifo chake. Sasa barua hiyo inatarajiwa kuuzwa kwa kianzio cha dola 100,000 sawa na zaidi ya shilingi milioni 228 za Kitanzania.

Saturday, April 21, 2018

SNURA: MENEJA WANGU HAUSIKI KWENYE MAISHA YANGU YA KIMAPENZI


Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Snura Mushi a.k.a Snuu Sex amesema Meneja wake HK hachangii kitu chochote kwenye mahusiano yake ya kimapenzi.

Akipiga story na Dizzimonline msanii huyu ambae kwasasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘Vumbi la mguu’ amesema meneja wake yupo kwa ajili ya kusimamia kazi zake tu za muziki na...
sio mahusiano yake ya kimapenzi.

“Labda niseme kitu kimoja ukiona nimefanya kitu chochote kwenye mapenzi au chochote kinachotokea  kwa mpenzi wangu basi fahamu meneja wangu hajachangia kitu chochote hapo ni mimi mwenyewe tu” Amesema Snura.

Aidha Snura ametoa ahadi kwa mashabiki zake kuwa hivi karibuni ataachia Movie ya ‘Vumbi la Mguu’ hivyo waandelee kuwa karibu na msanii huyo.

Friday, April 20, 2018

AMBER LULU: SIJAWAHI KUTAMBULISHWA WALA KUFIKA NYUMBANI KWA PREZZO


Msanii wa Muziki Bongo, Amber Lulu amefunguka kuhusu mipango yake ya kuolewa.

Muimbaji huyo ambaye yupo katika mahusiano na rapper Prezzo kutoka nchini Kenya, amesema ndoa ni majaliwa ya Mwenyenzi Mungu ila anaamini muda wowote ataolewa.
“Ndoa ni majaliwa kwa hiyo any time, Mungu akitujalia mtaona nitavaa sana...
shela,” amesema Amber Lulu.

Hata hivyo amekiri kuwa hajawahi kutambulishwa au kufika nyumbani kwa Prezzo kwani msanii huyo mara nyingi ndiye amekuwa akija hapa nchini.

SHOCK NEWZ: AGNESS MASOGANGE AFARIKI DUNIA


Video Queen maarufu nchini Tanzania, Agness Gerald maarufu kama Masogange amefariki dunia jioni ya leo Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, jijini Dar es salaam.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na ndugu wa karibu na marehemu, Dick Sound ambaye amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii kwenda kuhifadhiwa mochwari- Muhimbili. Kwa mujibu wa Steve Nyerere, Marehemu Agnes 'Masogange' Gerald, alifariki leo Saa 10 jioni katika hospitali ya Dr. NGOMA Mwenge DSM, baada ya...
kusumbuliwa na Ugonjwa wa Pumu.

Mwili wa Marehemu Agnes, utasafirishwa Jumapili hii kuelekea Mbeya kwa Mazishi. Kwa sasa msiba utakuwa kwao Makongo DSM.

Kumbuka kutakuwa na mabadiliko ya ratiba, hivyo Endelea Kukaa na sisi kwa Updates zaidi.

 
Wiki tatu zilizopita marehemu alishindwa kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili kwa kulazwa hospitalini, hii ni kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu wiki iliyopita.

Mastaa mbalimbali wa muziki na waigizaji wa filamu wametoa pole kufuatia taarifa hizo za mshtuko za kifo hicho, na Bongo5 inatoa pole kwa familia yake katika kipindi hiki kigumu.

Wednesday, April 4, 2018

USICHO KIJUA KUHUSU KAHAWA HURAHISISHA MZUNGUKO WA DAMU

Wanasayansi wamegundua kuwa unywaji wa kahawa unasaidia mzunguko wa haraka wa damu kwa kusafisha calcium katika mishipa.

Taarifa iliyotolewa na  “The Telegraph”, imesema wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Brazil cha Sao Paulo wamechunguza mpango wa lishe na kiwango cha calcium kwenye mishipa ya wafanyabiashara karibu 4,400 wa...
kahawa.

Kwa mujibu wa habari hiyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wanywaji wa kahawa wana kiwango kidogo cha calcium katika mishipa yao na mzunguko mzuri wa damu.

Hata hivyo wanasayansi wameonya kuwa ni vizuri kutozidisha vikombe vitatu vya kahawa kwa siku.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la “American Heart Association”.