HATIMAE mwili wa Ahmad Manyema umelazwa katika nyumba yake ya milele. Mzee Hamad manyema mwimbaji na mtunzi wa miaka mingi, amezikwa leo katika makaburi ya Mabibo Makutano. Watu wengi wakiwemo wanacham wa CUF tawi la Chechnya, ambako alikuwa mwanachama mzuri wa chama hicho, wanamuziki wengi wakongwe, na majirani wengi walihudhuria mazishi haya. Ahamed Manyema alifia katika hospitali ya Mwananyamala alfajiri ya Jumapili. Mungu Amlaze Pema Peponi
No comments: