Wednesday, May 2, 2018
UWOYA NA DOGO JANJA RAHA TUPU
Msanii wa Muziki wa Bongo Flava, Dogo Janja azidi kuyaanika mapenzi aliyonayo hadharani kwa mke wake ambaye ni Muigizaji,Irene Uwoya.
Dogo Janja kupitia ukurasa wa instagram amepost picha akiwa na mke wake huyo na kuandika caption iliyoandikwa hivi “thamani ya upendo wako ni ya maisha kama maisha yalivyo ni...
upendo.”
Irene Uwoya nae hakukaa kimya alimjibu Dogo Janja na kusema “Nakupenda leo jana na milele.”
WEMA SEPETU AIVUNJIA UKIMYA NGOMA MPYA YA OMMY DIMPOZ
Kimya kingi kina mshindo – Malkia wa filamu Bongo, Wema Sepetu ameshindwa kuzuia hisia zake kwenye wimbo mpya’Yanje’ wa Ommy Dimpoz ambao amemshirikisha Seyi Shay kutoka Nigeria.
Madam Sepenga amefunguka kuwa muziki wa aina hiyo ndio muziki anaoupenda na kumwambia msanii huyo kwa sasa anaimba...
muziki wa kikubwa.
Kupitia mtandao huo Wema ameadika:
Wanasemaga Kimya Kingi kina MSHINDO mkubwa… Ngoma Imenibamba Hatare… Sijui kwasababu ndo aina ya Mziki ninaopenda… Forever Bae Umemaliza wallahy… This One Is Just Amazing…
.
.
.
Alafu kama naona GROWTH… Yaani Mziki unaoimba now kama wa Kikubwa zaidi… Keep it Up kipenzi… Umeua… Yaani Ni Balaa… Kazi Nzuri umefanya kummezesha Seyi Shai Swahili…
.
.
.
WellDone… You outdid yourself… Proud of You… Ladies & Gentlemen ebu tufanye kutembelea Bio yake @ommydimpoz tukaicheck hii video na tusikilize hii track… Ni Moto wallahy… .
.
.
Naona hii ulituliza kichwa kweli kweli… Wen you talk about Mziki Mzuri sasa ndo huu apa… cc @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz @ommydimpoz
Sunday, April 29, 2018
Friday, April 27, 2018
BAADA YA MIAKA 35, ABBA WAINGIA TENA STUDIO
Katika maelezo yao waliyoyatoa kupitia ukurasa wao wa Instagram, walisema wazo liliwaijia kujaribu kuona itakuwaje wakiingia tena studio, wenyewe wanasema ni kama bile wanaendelea walipoacha kwani wana nyimbo kadhaa ingawaje tarehe ya kuziachia haijatajwa, japo wimbo wao mmoja I still have faith in you, utaonyeshwa kwenye luninga kuanzia mwezi wa Disemba, kwa kutumia taaluma ya kidijitali ambapo vitakavyokuwa vinaonekana vikifanya onyesho ni vivuli tu vya wanamuziki hawa.
Abba walikuwa na nyimbo nyingi maarufu kama Waterloo, I have a dream na kadhalika. Kundi hili lilisambaratika mwaka 1982.
BABU WA KITAA AKIRI STAREHE NDIYO CHANZO CHA YEYE KUPOTEA KIMUZIKI
Siku za nyuma kidogo Country Boy alisema kuwa moja ya kitu klichoua muziki wa msanii babu wa kitaa ni kutokana na kuendekeza starehe na kulewa umaarufu na ndio maana ameshindwa kuendelea na muziki wake.
akiongea na radio clouds fm ,Babu wa kitaa alikiri kuwa usemi wa ndugu yake Country Boy ni kweli na kwamba...
alilewa kuwa na jina na wimbo mzuri alikuwa ameutoa mara ya kwanza na ndio maana aliacha kufanya kazi na kuendekeza starehe.
Subscribe to:
Posts (Atom)
