Wednesday, December 2, 2015
KASONGO MPINDA CLAYTON HATUNAE TENA
Marehemu Mutombo Audax (kushoto), akiwa na marehemu Kasongo Mpinda
HAKIKA siku hii ni ya simanzi, nimetoka makaburi ya Kinondoni ambapo tumemzika mwanamuziki David Musa Gordon wa Safari Trippers, nafika nyumbani taarifa inakuja kuwa mwanamuziki mwingine mkongwe Kasongo Mpinda Clayton amefariki jioni hii nyumbani kwake Mwananyamala na mwili umepelekwa hospitali ya Mwananyamala.
Mungu Amlaze Pema
Friday, November 27, 2015
DAVID MUSA AFARIKI DUNIA
Kushoto mwenye miwani David Musa, wa tatu Marijani Rajabu na kulia mwisho Jumanne Uvuruge mtunzi wa wimbo wa Georgina.
Mungu amlaze pema
Monday, November 23, 2015
MFAHAMU MBARAKA YUSUPH MWANAMUZIKI WA NATIONAL PANASONIC NA POWER IRANDA
Hayo ni maneno ya Mbaraka Yusuph, kati ya wacharazaji mahiri wa zamani wa magitaa yote pamoja na Saxophone, aliyewahi kuzitumikia bendi mbalimbali hapa nchini, zikiwamo, The Smashers, National Panasonic, OSS ‘Power Iranda’, Seven Blind Beats na the Big Africa ya Arusha..ENDELEA HUKU
Monday, November 9, 2015
MWANAMUZIKI MKONGWE CAPT JOHN SIMON AFARIKI DUNIA
| Capt John Simon |
MWANAMUZIKI mkongwe ambaye kwa siku za karibuni alikuwa kwenye bendi ya Shikamoo Jazz, Capt John Simon, amefariki dunia leo katika hospitali ya Muhimbili. Mzee huyu alikuwa mmoja ya waanzilishi wa NUTA Jazz band, na baadae kadri ya maelezo yake mwenyewe, Mheshimiwa Rashid Kawawa, ndie alimtoa NUTA Jazz na wanamuziki wengine na kwenda kuanzisha JKT Jazz Band, iliyopata umaarufu kama Kimbunga Stereo.
| Waimbaji wa NUTA Jazz Band, toka kulia John Simon, Muhidin Gurumo, na kushoto Ally Akida |
Mzee John Simon pia alikuwa mwanzilishi wa Shikamoo Jazz Band, bendi ambayo ameitumikia mpaka siku zake za mwisho. Capt John Simon pia alikuwa makamu mwenyekiti wa CHAMUDATA mwishoni mwa miaka ya 90, akiwa makamu wa John Kitime, na hatimae kuwa mwenyekiti baada ya John kitime kujiuzuru nafasi yake. Taratibu za mazishi zitapatikana baada ya ndugu kukutana. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga.
Wednesday, October 14, 2015
MWANAMUZIKI ENZI ZA MWALIMU PART 1
Shule zote zilikuwa na bendi ya shule. Ambayo kila asubuhi ilipiga muziki wakati wa wanafunzi kukaguliwa kama wamekuja shuleni wasafi, moja ya ndoto za wanafunzi wengi ni kuwa katika bendi ya shule. Aidha kuwa mpiga ngoma au mpiga filimbi na kubwa kuliko yote ni kupata bahati kuwa mshika kifimbo. Shule zilishindana kwa kuzivalisha bendi mavazi bora na upigaji kuwa makini na hivyo siku za sikukuu kila shule ilijitahidi bendi yake ndio iwe bora. Hakika nakumbuka raha iliyokuwepo wakati shule mbalimbali zilipokutana siku ya siku kuu au kukiwa na maandamo na kisha kila bendi kupita mbele ya mgeni wa heshima, wanafunzi tulijitahidi kuwa wakakamavu wenye nidhamu ili shule yetu ishinde.
TANU Youth League (TYL) ilikuwa na matawi kila mahala. Kimuziki TYL ilichangia sana, kwani kila kwenye tawi la TYL lazima kulikuwa na kundi la muziki aidha kwaya au ngoma, na mara nyingi vyote na sehemu nyingi TYL pia ilinunua vyombo vya bendi na hivyo karibu kila wilaya ilikuwa na bendi. Hapa ndipo wanamuziki wengi maarufu wa miaka hiyo na ambao nyimbo zao bado maarufu mpaka leo walikotokea. Pale Iringa, vyombo vya TYL hatimae viliishia kuwa chini ya shule ya Sekondary ya Mkwawa na hivyo pale kulikuwa na bendi nzuri sana ambayo iliweza kuja kurekodi RTD, kati ya waliokuwa wanamuziki wa bendi hiyo, mpia solo ni mzazi wa producer mmoja maarufu wa Bongo fleva na hata yeye alikuja kuwa na bendi yake TZ Brothers, mpiga rythm kwa sasa ana chuo kikubwa cha muziki pale Tabata, wakati muimbaji mmoja wa bendi hiyo alianzisha bendi maarufu pale Arusha.
Tuesday, October 6, 2015
Smokie Norful - Forever Yours - 2014
Com sua voz de tenor soulful e uma capacidade infalível para fundir gospel contemporâneo, com sensibilidades de hip-hop, Smokie Norful é uma das luzes mais brilhantes no cenário gospel atual. O filho de um Metodista Episcopal ministro Africano, Norful passou seus primeiros 14 anos em Muskogee, OK, Com dois anos , ele estava escolhendo melodias no piano, por quatro, ele estava ativamente tocando e cantando na igreja de seu pai, e por dez anos, ele era um artista de destaque em um álbum personalizado montado por um diretor musical regional. Embora a música era sua paixão duradoura, Norful em vez optou por estudar história na Universidade de Arkansas em Pine Bluff, acabou trabalhando como instrutor de história por quatro anos antes de se mudar para Chicago em 1998, a fim de ganhar um mestrado em Divindade do Seminário Teológico Garrett .
With his soulful tenor voice and an unerring ability to fuse contemporary gospel with hip hop sensibilities, Smokie Norful is one of the brightest lights in today's gospel scene. The son of an African Methodist Episcopal minister, Norful spent his first 14 years in Muskogee, OK, with two years he was picking melodies on the piano, for four, he was actively playing and singing in his father's church, and for ten years he was a featured artist on a custom album assembled by a regional musical director. Although music was his enduring passion, Norful instead chose to study history at the University of Arkansas at Pine Bluff, ended up working as a teacher of history for four years before moving to Chicago in 1998 to earn a master's degree in divinity from Garrett Theological seminary.
02.No Greater Love
03.I Need a Word
04.I've Got What You Need
05.Imperfect Me
06.Forever Yours
07.In the Meantime
08.Nothing Is Impossible
09.Run Run
10.He Loves Me
11.I Feel Good
12.Always Remember
13.Love
14.Say So
Clique Aqui Para Baixar (Click Here To Download)
Subscribe to:
Posts (Atom)
