Thursday, January 4, 2018
Mary Mary - Incredible - 2002
01.Incredible
02.God Bless Atk
03.He Said
04.In the Morning
05.Ordinary People
06.Trouble Ain't
07.Little Girl
08.This Love
09.I Try
10.Hold On
11.God Has Smiled on Me
12.You Will Know
13.So Close
14.Thank You
15.Give It Up Let It Go
Clique Aqui Para Baixar (Click Here To Download)
J Moss - V4... The Other Side - 2012
Born and raised in Detroit, MI, gospel singer and producer J. Moss is part of a very talented family of gospel musicians, including his father, Bill (of Bill Moss & the Celestials), and his cousin, part of the group the Clark Sisters. Eventually, J. (or James) would start his own group, a duo with brother Bill called the Moss Brothers. Over the next few years, the Moss Brothers would record a pair of albums and tour regionally, but the call of further education lured James away -- but not for very long. It would only be two years in at Michigan State University before J. realized that his true calling was in music, namely putting to work his skills in production and composition. A small-potatoes solo career inked just after returning to Detroit fizzled rather quickly, but it would be his participation in the production trio known as PAJAM that would catapult J. to greater success in his chosen genre. The group, made up of James, Paul Allen, and Walter Kearney, produced and composed a number of gospel hits, using traditional elements of gospel alongside more up-to-date hip-hop and R&B sounds. In 2004, J. Moss, with songs written with his PAJAM partners, decided to give a solo album another shot. The resulting work, The J. Moss Project, was released in 2004 and became a hit. J. decided to keep on working as a solo artist and in 2007 -- after a bit of delay -- released a follow-up entitled V2.... In addition to his already impressive résumé, J. Moss has had a hand in work by other artists such as Patti LaBelle and *NSYNC.
01.God's Got It
02.Imma Do It
04.Strong Enough
05.Good & Bad
06.Good Day (Feat.Karen Clark Sheard & Kierra "KiKi" Sheard)
07.Caught Up in Love
08.Shout
09.You Did (Feat.James Fortune)
10.Holy Is Your Word
11.The Prayers (Feat: Hezekiah Walker, LFP & Dorinda Clark-Cole)
12.The Other Side of Victory
13.Keep Your Head Up
14.Good & Bad [Remix Club Mix]
MTUNZI WA LUNCHTIME MZEE GABRIEL OMOLO AFARIKI DUNIA
Mzee Gabriel Omolo Aginga anayejulikana kwa wapenzi wengi wa muziki wa zamani kwa wimbo wake Lunchtime, alikuwa ni mmoja wa wanamuziki wachache waliotamba Kenya katikamiaka ya 70 ambao walikuwa bado hai. Katika video moja iliyotoka karibuni ilimuonyesha Mzee Gabriel ambae uzeeni alikuwa mkulima akiangalia mifugo yake akiwa katika afya nzuri.
| Gabriel Omolo (Picha kwa hisani) |
Gabriel alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi na kufariki katika hospitali ya Busia jana Jumatano usiku. Rafiki yake wa toka utotoni na mwanamuziki mwenzake Charles Makawita ambaye walitoka wote katika kijiji cha Nyabenda Uhoro, kwenye kaunti ya Siaya alisema Gabriel alikuwa na miaka 79 na alifariki kutokana na matatizo ya kushindwa kupumua. Mke wa marehemu Alice Adeya ndiye aliyemtaarifu Charles kuwa mwenzie anaumwa.
Gabriel alizaliwa 1939, alijifunza gitaa akiwa shule ya msingi ya St Peter Claver ambako pia alikuwa anaimba kwenye kwaya ya shule hiyo. Kwenye miaka ya 60 alijiunga na ile bendi maarufu ya Equator Sound Band ambayo wakati huo ilikuwa na miamba akina Peter Tsotsi, Nashil Pichen Kazembe, Daudi Kabaka na Fadhili William. Gabriel ndie aliyepiga gitaa la bezi kwenye wimbo Pole Musa wimbo uliotungwa na Peter Tsotsi. Marehemu Gabriel alipigia pia Eagles Band , Blue Shades na baadae Apollo Komesha Band
Septemba 1974 Gabriel alikuwa Mkenya wa kwanza kupata tuzo ya International Golden Disc kutokana na mauzo ya wimbo wake wa Lunchtime. Kampuni ya Phonogram Records ilihakikisha kuwa single ya wimbo huo iliuza nakala 150,000.Afrika ya Mashariki na Afrika Magharibi.
Remix ya wimbo huo ilifanywa mwaka 2005, ikiwa ni miaka 35 toka ilipoachiwa nyimbo hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 1970. Remix ilifanywa na mwanamuziki marehemu Poxi Presha na Paddy makani, Mkongo aliyekuwa akiishi Kenya. Tunamuomba Mungu Amlaze Pema Gabriel Omolo
Thursday, December 21, 2017
SANAA KATIKA MIKAKATI YA KUWA NCHI YA VIWANDA
Sanaa ni pana sana. Ukiangalia kila kinachokuzunguka, kina usanii ndani yake. Mpangilio wa habari katika gazeti hili, mpangilio wa lugha, mpangilio wa picha, halafu ukinyanyua macho na kuangalia vitu vilivyokuzunguka, majengo, mavazi, samani, vyombo vya usafiri, mpangilio wa rangi wa vitu hivyo au ukisikia sauti za muziki vyote ni kazi za aina mbalimbali za sanaa. Katika zama hizi za kauli mbiu ya ‘nchi ya viwanda’, inashangaza kuwa matayarisho ya wasanii wa kuambatana na nchi ya viwanda haitiliwi mkazo, lakini bidhaa zote za viwanda zinahitaji usanii, kama ni kuchora nembo nzuri au kuweka tangazo zuri la mali au hata kutengeneza sura nzuri ya bidhaa zitakazozalishwa katika ‘nchi ya viwanda’ ni kazi ya sanaa. Bila matayarisho ya wasanii bora tutakuwa na mali nzuri zisizo na sura ya kumvutia mlaji. Hakika mpaka leo naamini kuwa kama wasanii wangehusishwa katika kukamilisha lile gari lililotengenezwa Tanzania na kupewa jina ‘nyumbu’, mambo kadhaa yangekuwa tofauti, kwanza lingepatikana jina la kuvutia zaidi na pili gari lile lingebuniwa sura ya kuvutia zaidi. Watu wengi hununua magari kutokana na muonekano wa gari, bila hata kujiuliza mambo mengine ya kiufundi kuhusu gari husika.
Kama nilivyosema sanaa ni pana sana leo nizungumzie sanaa ya kutumia mdomo. Binadamu wote kwa kawaida tuna midomo na pia kwa kawaida wote tunaweza kutoa sauti mbalimbali na mdomo huo. Mungu kawapa watu mbalimbali vipaji vya kuweza kutumia mdomo huo, kuna waimbaji wa staili mbalimbali, wako watambaji, waghani wa mashahiri, wasimuliaji wa hadithi, watangazaji, wachekeshaji, wahubiri, wanasiasa, na wengine wengi wa aina yao, wote hawa wanafanya sanaa zao kwa kutumia mdomo, japokuwa katika hawa hawa wengine hujiona sanaa yao ni bora kuliko ya wengine na mara nyingi hukataa katakata kuitwa wasanii. Jambo moja lisilo pingika ni kuwa kila msanii hupenda kupata jukwaa la kuonyesha sanaa yake, na ndio maana kulibuniwa majukwaa, na hatimae majumba makubwa ya kuonyesha sanaa ambayo nayo huwa na majukwaa makubwa ya kupendeza. Wasanii hutayarisha shughuli zao na kisha hualika watazamaji au wasilikizaji. Msanii aliyetayarisha au kutayarishiwa shughuli ni wazi ndie anayestahili kuweko jukwaa kuu kwani hata wanaokuja kumtazama wangetaka iwe hivyo ili wamuome na kumsikia vizuri. Kwenye shughuli za wasanii ambao hutumia midomo yao kuhubiri siasa, mara nyingi huweza ikaonekana ni vizuri kualika wasanii wengine, kama vile wanamuziki au wacheza ngoma au wanamuziki wa bongofleva na kadhalika ili waje wafanye sanaa zao kuleta burudani au kutoa ujumbe wa siku hiyo, kabla msanii aliyetayarisha shughuli hajapanda jukwaani na kuhubiri siasa. Katika shughuli za namna hii huwa hakuna utata sana kwani jukwaa kuu huanza kutumika na wanasiasa bila ya kuingilia. Lakini kuna tabia moja ambayo imejijenga hapa kwetu wakati shughuli inafanywa na wasanii wasio wanasiasa, ambao ili kufanikisha shughuli yao hualikwa wanasiasa, ni kawaida sana katika shughuli za namna hii ukakuta wanasiasa wamepangiwa viti kwenye jukwaa kuu na wenye shughuli kulazimika kujengewa jukwaa dogo pembeni, au kulazimika kufanya shughuli zao za sanaa kwenye sehemu ambayo hawaonekani. Nitoe mfano, siku chache zilizopita kulikuwa na shughuli kubwa ambayo ilihusu wasanii kuhamasisha uzalendo, wasanii kutoka sehemu mbalimbali nchini walikusanyika Dodoma kwa ajili ya shughuli hiyo. Shughuli ilipangwa kufanyika katika ukumbi mzuri uliojengwa kitaalamu kwa shughuli kama hizi. Na shughuli hiyo ilikuwa ikionyeshwa mubashara nchi nzima, hii iliwezesha ambao hawakuweza kuja Dodoma wafaidi na kuelewa yanayofanyika Dodoma bila wasiwasi. Siku hiyo ukumbi huu ‘ukaboreshwa’ kwa ajli ya shughuli, na jukwaa dogo lilitengenezwa pembeni, na hapo ndipo wasanii walipopangiwa kufanya shughuli zao, katika jukwaa kubwa vikapangwa viti vya kukalia viongozi watazamaji wa maonyesho ya sanaa. Jengo hili lenye sehemu ya kukaa yenye zaidi ya viti mia tano, ikaachwa na viti vikapangwa kwenye jukwaa ambapo ndipo sehemu sahihi ya kuonyeshea kazi za sanaa. Ni nini kinasababisha ukumbi mzuri ule usitumike inavyotakiwa? Kwani viongozi wakikaa viti vya mbele na kuangalia sanaa zikiendelea jukwaani itakuwa wamedharauliwa? Mkao huo unaleta utata mwingine mkubwa kwa wasanii wanaofanya onyesho, wanakuwa katika utata, je wanafanya onyesho kwa ajili ya hadhira hivyo wawape mgongo viongozi au wanafanya onyesho kwa ajili ya viongozi hivyo waipe hadhira mgongo? Kwa aliye angalia kupitia onyesho lile kupitia luninga, onyesho lilionekana ni la hovyohovyo tu, wasanii wakionekana hawajui wanataka kufanya nini.
Baada ya viongozi kumaliza kilichowaleta wakaondoka, viti viliendelea kuwa jukwaani hivyo wasanii wakawa wanafanya maonyesho yao chini ya jukwaa, na hivyo kutokuonekana vizuri kazi yao na watazamaji kuamua kuondoka mmoja mmoja. Matayarisho yote yamekuwa bure. Hata ule moto wa uzalendo uliotegemewa kuwashwa umegeuka cheche tu. Ushauri tu kwa wasanii wote niliyowataja hapo juu, itapendeza kila moja akiheshimu kazi ya mwenzie na kuruhusu ifanyike katika sehemu stahili, na si kujali tu kiongozi atakuwa wapi na kutokujali mamia ya hadhira yatawezaje kufaidi sanaa iliyopo ambayo imetayarishwa kwa muda mrefu na gharama kubwa..
PAKUA ANKO KITIME APP

PAKUA APP YA ANKO KITIME KWENYE SIMU YAKO UPATE TAARIFA ZOTE ZITAKAZOTUNDIKWA KWENYE www.theiringa.blogspot.com
HABARI vichekesho PICHA video
Wednesday, November 15, 2017
HISTORIA FUPI YA DEKULA KAHANGA VUMBI
![]() |
| Vumbi Dekula Kahanga |
![]() |
Orch. Maquis Original 1987 Wapiwapi Chang'ombe Bar,kutoka kulia ni: Mbuya Makonga "Adios",Dekula Kahanga"Vumbi",Mpoyo Kalenga na William Maselenge. Alie chuchumaa ni Juma Choka |
Kwa wapenzi wa muziki wa dansi Tanzania, jina la mpiga gitaa Dekula Kahanga Vumbi si geni, wengi hasa humfahamu kama mwanamuziki wa Maquis Original, na wanakumbuka mlio wa gitaa lake katika nyimbo kama Makumbele na Ngalula hasa pale ambapo Assossa anamhamasisha aongeze utamu kwa kutaja jina' Vumbi Vumbi'. Lakini Je, alianzia wapi? Kwanza kabisa baba yake hakupenda kabisa apige gitaa, ulikuwa ugomvi mkubwa lakini bahati nzuri alikulia kwa bibi yake katika mji wa Uvira, mkoa wa Kivu, Jamhuri ya Kongo. Kwa bibi kama walivyo wabibi wengi, alikuwa na uhuru zaidi na akaanza kwa kutengeneza magitaa yake, ambalo yalikuwa yakivunjwa kila baba yake alipokuwa akija kumtembelea bibi yake. Jirani na alipokuwa akiishi kulikuweko na bar inaitwa Sikiya sosi ambapo palikuweko na bendi ikiitwa Gramick Jazz, bendi iliyopitiwa na wanamuziki wengi ambao baadae walikuja Tanzania akiwemo Dr RemmyOngala. Vumbi alikuwa akisikiliza muziki ukipigwa ndani ya hiyo bar na yeye akawa anafuatisha kwenye gitaa la kutengeza mwenyewe la nyuzi tatu, hatimae bibi yake akamnunulia gitaa dogo la nyuzi nne ambalo alikuwa anaenda nalo mpaka shule, ambapo mwalimu wake siku nyingine alikuwa akimwita awatumbuize wanafunzi wenzie. Hatimae akakutana na jamaa aliyekuwa akipiga katika bendi iliyokuwa ikimilikiwa na mapadri, akawa anamnunulia sigara huyu jamaa nae akaanza kumfundisha chords mbalimbali za kupiga gitaa. Aliendelea vizuri hatimae akajiunga na bendi hiyo ya mapadri iliyoitwa Kyalalo Band akiwa mpiga rhythm. Wanamuziki wa Kyalalo hawakuruhusiwa kujiunga na bendi zilizo kuwa zinapiga muziki kwenye bar, wala bendi yenyewe haikuruhusiwa kwenda kupiga kwenye bar, kulikuweko na ukumbi mkubwa wa kanisa na hapo ndipo walipofanya mazoezi na maonyesho, lakini baadae Vumbi akajiunga na bendi Bavy National tena kama mpiga rhythm,
na hapo akakutana na mwimbaji Issa Nundu ambae alikuwa anafanya hospitali na jioni kujiunga na bendi, hatimae Kyanga Songa ambaye kazi yake ilikuwa Bwana Shamba nae alijiunga nao.
Katika kipindi hicho wakazi wa Kongo ya Mashariki, ambako kunazungumzwa Kiswahili, walikuwa wakisikiliza na kuzijua bendi nyingi kutoka Afrika ya Mashariki, bendi kama Tabora Jazz, Mangelepa, Simba wa Nyika, Mlimani Park zilisikilizwa sana, na nyimbo kama Kassim ilikuwa moja ya nyimbo maarufu wakati huo na hivyo ikawa ndoto ya Vumbi na wenzie kuwa lazima siku moja waende huko unakotoka muziki mtamu huo ili nao waweze kushiriki. Katika kipindi hicho Kyanga Songa na Issa Nundu waliondoka kwenye bendi yao ya Bavi National na kuelekea Tanzania. Bendi ikatetereka sana, lakini nae wakati huo akawa anahamu sana ya kuja Afrika Mashariki. Bahati nzuri mtu mmoja Alida Shanga akamjia akiwa ametumwa na Marehemu Mzee John Luanda aliyekuwa anamiliki Chamwino Jazz kuja kutafuta wanamuziki toka Kongo, nae akawachukua wanamuziki kadhaa akiwemo Vumbi na kituo chao cha kwanza kilikuwa Tandale jijini Dar es Salaam. Na siku waliofika tu na wakaanza mazoezi siku hiyo hiyo. Wakiwa vijana bado yeye na wenzie watatu walikuja wakiwa na staili ya kuimba na kucheza steji show ambayo wakati huo iliitwa sarakasi, na pia wao ndo kilikuwa kikundi cha kwanza kuanza kurap katikati ya nyimbo. Waimbaji wakiwa ni Sisko Lunanga, Fanfan Bwami, na mwenzao mmoja Baposta Kilosho ambae hatimae alirudi Kongo. Recording ya kwanza ilimuacha Julius Nyaisanga akishangaa vituko vya vijana hawa. Katika bendi ya Chamwino wakati huo wapiga magitaa walikuwa Vumbi Dekula, Kazembe wa Kazembe (huyu alikuwa Msukuma ambaye aliishi kwa muda Kongo na alikuwa mpiga gitaa hodari sana), na Mzee Albert, na hatimae wakamchukua Muhidin ambae alikuwa mpiga bezi wa Dr Remmy. Siku moja walienda kuomba kupiga na Maquis Original(lift), wakati huo wakipiga nyimbo za kopi, nyimbo kama Mario, Maze na kadhalika, hivyo wakazipiga hizo na watu wakafurahi sana na kuwatuza fedha nyingi, wakachanganyikiwa maana bendi yao ya Chamwino ilikuwa haina mshahara na si mara moja walitembea kwa miguu kutoka Buguruni hadi Tandale kwa kukosa hata nauli. Japo wakati huo walikuwa wadogo kwa umri na hata umbo walifika mahala marehemu Kasheba alikuwa anawaita ‘Vimario’, upigaji wao ulikuwa mzuri sana. Nguza aliwashauri wawe wanakuja kupiga kabla Maquis hawajaanza kupiga. Hivyo wakaamua kuacha Chamwino, na wakawa wanasindikizana na Maquis, hili lilimuudhi aliyewaleta na siku moja wakiwa Silent Inn, maafisa wa Uhamiaji walikuja kuwachukua wakalazwa Central Police na kisha kupelekwa gereza la Keko. Wakiwa huko walimwandikia Mzee Luanda kuwa wanarudi Chamwino, basi wakaachiwa na kurudi kusuka upya Chamwino Jazz. Lakini hawakukaa muda mrefu Mzee Makassy akaja kuwaomba waingie katika bendi yake, wenzake waimbaji wakaenda yeye akabaki Chamwino, lakini muda si mrefu Nguza akamwambia aandike barua ajiunge na Maquis. Nae akafanya hivyo na ndio kujiunga rasmi na Maquis kama mpiga gitaa la second solo. Aliwakuta wanamuziki kama Maneno Uvuruge, Omari Makuka, Keppy kiombile, Ilunga Lubaba, William Maselenge na wengine wengi. Aliendelea kupiga second solo hadi siku moja bendi ilikuwa inapiga maeneo ya Ukonga, kwa kawaida Mzee Lubaba alikuwa anapiga kuanzia saa tatu mpaka saa sita, na kisha Nguza Viking akiingia na kuendelea .
![]() |
| Maquis wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma, wa pili toka kulia na shati jeusi Vumbi, wapili toka kushoto na suruali nyeusi Issa Nundu |
Siku hiyo Nguza hakuonekana Vumbi akaweza kupiga nyimbo zote za Nguza, na kesho yake akaambiwa afike ofisini akasainishwa rasmi mkataba wa kuwa mwanamuziki wa Maquis. Baada ya muda mfupi Nguza akaacha bendi.
Muda mfupi baada ya hapo walirekodi ule wimbo maarufu wa Makumbele, solo ya wimbo huu ilikuwa awali ikipigwa na Mzee Lubaba, lakini afya ya mzee Lubaba ilianza kuzorota nae akawa anawafundisha nyimbo zake wanamuziki wengine, wimbo wa Makumbele alifundishwa Omari Makuka na akawa anaupiga katika maonyesho mbalimbali, lakini wakati wa kutaka kurekodi kamati ya uongozi ya Maquis iliamua Vumbi aufanyie mazoezi na aurekodi. Kurekodi kwa album ya Makumbele ilitokana na safari ndefu ya bendi ambayo ilichukua miezi mitatu katika mikoa ya Ziwa, hivyo bendi iliporudi Dar ilikuta sifa ya bendi imepungua, hivyo walirekodi album ya Makumbele iliyokuwa na nyimbo kama Tipwatipwa, Ngalula na Makumbele, sifa ya bendi ikarudi juu tena kwa mara nyingine. Na ni wakati huo ambapo bendi ilihamia katika ukumbi wa Lang’ata Kinondoni. Vumbi aliedelea kupiga katika bedi hii mpaka alipoamua kuhamia Sweden ambako yuko mpaka leo akiendelea kupiga muziki.
Sunday, November 12, 2017
JE UTAMU WA GITAA LA RYTHM UTAWEZA KURUDI TENA?
![]() |
| Harrison Siwale (Satchmo) mpiga rythm, Mbaraka Mwinyishehe mpiga solo, Abdul Mketema mpuliza saksafoni |
Lakini katika makala ya leo tuzungumzie gitaa la rythm. Chombo hiki bado kinapigwa katika bendi nyingi lakini umuhimu wake umeshuka sana. Katika kipindi cha miaka ya 60 na 70, gitaa hili lilikuwa na umuhimu mkubwa na wapigaji wake waliweza kubuni staili zao wenyewe. N kujijengea sifa kubwa. Kati ya wapiga rythm maarufu alikuweko Satchmo, hilo ndio lilikuwa jina la kisanii la Harrison Siwale, huyu alikuwa Mzambia aliyekuja weka masikani yake katika mji wa Tanga. Alipitia bendi kubwa za Tanga ikiwemo Atomic Jazz Band na hatimae Jamhuri Jazz Band. Satchmo alikuwa na staili peke yake ya kupiga rythm, sikumbuki kusikia mtu mwingine akipiga rythm ya aina yake kabla ya hapo, lakini hakika wapiga rythm wengi walichukua mtindo wake na kubuni vionjo vya aina yao. Rythm yake ilitawala nyimbo za Jamhuri Jazz Band wakati huo. Ufundi wake unaonekana sana katika nyimbo kama Mganga no 1 na 2, au Blandina. Kule Tabora Mzee Kasim Kaluwona nae alikuwa na staili tofauti ya upigaji wa gitaa la rythm uliyoifanya Tabora Jazz kuwa na staili yake peke yake, kumbuka gitaa lake katika wimbo Asha, au Dada Lemmy. Charles Kazembe akiwa na Morogoro Jazz anakumbukwa katika upigaji wa rythm kwenye nyimbo kama Wajomba Wamechacha. Hao ni wachache tu kulikoweko na wengi marufu. Katika kipindi hiki huko Zaire kulikuwa na mipigo mbalimbali ya gitaa la rythm, ila kitu kipya kikaanzishwa ambapo katika ufungaji wa nyuzi ,wapiga rythm wakauondoa uzi namba nne katika gitaa hilo na kuweka uzi namba moja, hivyo kukawa na nyuzi namba moja 2 katika gitaa moja, hapo ndipo akina Vata Mombasa wakaweza kuleta utamu mpya katika upigaji wa rythm, ufungaji wa aina hii wa nyuzi za gitaa ulifahamika kama 'double string'. Wakati huo Orchestra Kiam wakawa wanajivunia kupiga rythm kwa spidi kali sana,vibao kama Kamiki, Bomoto ni ushahidi wa kazi hizo. Utamu wa ufungaji wa nyuzi kwa staili hii uliweza kusikika vizuri katika gitaa lililopigwa mwanzo kabisa wa wimbo Andoya. Umuhimu wa gitaa la rythm ulikuwa ukionekana kwa bendi nyingi kuwa na mtindo wa 'kuachia rythm', huo ulikuwa ni mpangilio ambapo gitaa la rythm liliachwa lipige peke yake wakati magitaa mengine yakiwa kimya. Hapo mpiga rythm aliachiwa kucheza na gitaa alivyotaka na kuonyesha umahiri wake wote. Mtindo huu ulipendwa sana na wapenzi wa muziki. Utaratibu huu umerudi kwa njia ya ajabu sana, bendi nyingi za taarab vimeanza 'kuachia rythm' lakini kwa kuwa bendi hizo hazitumii tena gitaa la rythm , jukumu hili linafanywa na mpiga solo, tena vipande vingi vinavyopigwa ni vile vilivyopigwa na bendi za zamani!! matokeo ni yaleyale, wapenzi wa muziki hupanda mzuka na kucheza sana wakati wa kipindi hicho.
Kwa ujumla bendi nyingi za dansi hazitilii umuhimu tena gitaa la rythm. Kinanda kimechukua nafasi ya gitaa hili. Kuna bendi ambazo zinalo gitaa la rythm lakini kwa mfumo wa sasa wa muimbaji kuchukua nafasi kubwa ya wimbo gitaa hilo limerudishwa nyuma sana. Lakini kwenye muziki kila kitu kina utamu wake kamwe chombo kimoja hakiwezi kuziba pengo la chombo kingine.
Subscribe to:
Posts (Atom)







