Kwa masikikitiko makubwa naomba niwataarifu kuwa mwanamuziki nguli Shaaban Dede, Kamchape, Super Motisha hatunae tena. Amefariki asubuhi hii Muhimbili. Kwa siku chache alionekana kama anapata nafuu lakini hatimae asubuhi hii mwenzetu ametutangulia. Shaaban Dede alizaliwa Kanyigo Bukoba mwaka 1959, alianza kupenda muziki toka akiwa mdogo kwa vile wajomba zake walikuwa na bendi iliyoitwa Ryco Jazz, hatimae nae pia akaanza muziki kwa kujiunga na Police Jazz Band ya hukohuko Bukoba, lakini alianza kufahamika zaidi alipotoka huko na kuwa mwanamuziki wa bendi kadhaa nchini ikiwemo Tabora Jazz, Dodoma International, Bima Lee,Orchetra Safari Sound, DDC Mlimani Park na JUWATA na hatimae Msondo Ngoma. Blog hii inatoa pole kwa ndugu wapenzi na jamaa wote wa Shaaban Dede.
Tusubiri taarifa zaidi kuhusu msiba huu kutoka kwa nduguze.
Mungu Amlaze Pema Shaaban Dede
No comments: