Friday, July 7, 2017

MAZISHI YA SHAABAN DEDE KATIKA PICHA

MWANAMUZIKI mkongwe Shaaban Dede leo mchana amezikwa katika makaburi ya Kisutu akisindikizwa na kundi kubwa sana la wapenzi ndugu na marafiki. Uwingi wa waombolezaji wa mazishi ya Dede yanakumbusha sana mazishi ya Marijani Rajabu mwaka 1995. Katika makaburi haya ya Kisutu ndipo pia amezikwa, Shem Karenga, Kassim Mapili, Marijani Rajabu na leo nguzo nyingine ya muziki wa dansi Shaaban Dede amelazwa katika makaburi haya.























Wednesday, July 5, 2017

KWA MASIKITIKO MAKUBWA TAARIFA IMETUFIKIA KUWA SHAABAN DEDE AMEFARIKI DUNIA ASUBUHI HII MUHIMBILI

Kwa masikikitiko makubwa naomba niwataarifu kuwa mwanamuziki nguli Shaaban Dede, Kamchape, Super Motisha hatunae tena. Amefariki asubuhi hii Muhimbili. Kwa siku chache alionekana kama anapata nafuu  lakini hatimae asubuhi hii mwenzetu ametutangulia. Shaaban Dede alizaliwa Kanyigo Bukoba mwaka 1959, alianza kupenda muziki toka akiwa mdogo kwa vile wajomba zake walikuwa na bendi iliyoitwa Ryco Jazz, hatimae nae pia akaanza muziki kwa kujiunga na Police Jazz Band ya  hukohuko Bukoba, lakini alianza kufahamika zaidi alipotoka huko na kuwa mwanamuziki wa bendi kadhaa nchini ikiwemo Tabora Jazz, Dodoma International, Bima Lee,Orchetra Safari Sound, DDC Mlimani Park na JUWATA na hatimae Msondo Ngoma. Blog hii inatoa pole kwa ndugu wapenzi na jamaa wote wa Shaaban Dede.
Tusubiri taarifa zaidi kuhusu msiba huu kutoka kwa nduguze.

Mungu Amlaze Pema Shaaban Dede

Saturday, July 1, 2017

MAHABUBA

Image result for BLACK ROMANTIC


STORI ZA KUSISIMUA ZA MAPENZI,VISA NA MIKASA YA UKWELI KABISA.

Nilikua mwajiriwa katika kampuni moja maarufu jijini dare s salaam , katika kuajiriwa kwangu huko nikawa msaidizi maalumu wa bosi wa kampuni ile , basi siku moja moja nilikuwa naenda kujirusha na bosi wangu .


Ukizingatia kwamba sikuwa na mume wala mchumba na kwa kweli huyu bosi ndio alikuwa mtu wa kwanza kufanya nae tendo la ndoa , hivyo nilifurahia mhemko wake na jinsi alivyokuwa ananipenda na kunijali kila kitu nilipata na zaidi .

Alifanya yote haya bila kunificha kwamba ana mke na watoto nyumbani kwake kwahiyo wakati mwingine chochote kinaweza kutokea nijiandae kwa shuguli hiyo pevu kama mke wake akishitukia dili hilo .

Tulikuwa na uhusiano na huyu bosi kwa miezi 4 hivi mpaka siku moja katika tembea tembea mitaani nikakutana na kijana mmoja mtanashati akanieleza kwamba ananipenda na kunizimia sana yaani ameshanifia

Huyu kijana alihangaika kwa mwezi mzima mpaka siku nikaja kumkubalia akawa ndio mpenzii wangu halali sasa , nilimwamini sana nay Eye aliniamini sana , miezi 3 tokea kujuana na huyu kijana aliniambia kuhusu kufanya nae tendo la ndoa .

Nilifikiria sana wakati mwingine nilitaka kulia jinsi alivyokuwa ananishika na kuniomba tendo la ndoa akiwa chumbani kwangu , alijaribu kunishika sehemu kadhaa akanivua nguo nami nilimtolea nje nilimkatalia .

Basi siku moja nikamwomba tukaangalie afya zetu , kijana wa watu alikasirika sana wiki nzima hakufika nyumbani kwangu wala kunipigia simu , kumbe alitaka tufanye tendo la ndoa bila kinga ? sasa ningejuaje kuhusu afya yake ? au ananiamini nini mimi ?

Maisha yaliendelea na mambo mengine yaliendelea tu wiki ya 3 alinipigia simu akaniomba msamaha turudiane na alikubali kwenda na mimi kupata vipimo vya afya zetu kujua kwanza kabla hatujaanza mambo mengine yoyote yale .

Basi ndio hivyo majibu yaliyoka mazuri , ndio mapenzi yetu alikuwa zaidi na penzi nilimpa bila hiyana wala aibu yoyote , yeye mwenyewe alifurahia mambo yangu na kwanza alikuwa anatoroka nyumbani kwao kuja kulala kwangu wakati mwingine mwezi mzima .

Tuliendelea kwa miezi kadha na huyu kijana huku na mimi nikiwa na bosi wangu kule kazini , basi bwana siku moja , sisi officini tulitakiwa kwenda kutoa damu hospitali ya muhimbili katika maadhimisho ya siku ya afya duniani . Watu walipimwa afya zao na mimi nilipimwa , majibu yangu yalikuwa ya kutatanisha sikuamini macho yangu wala masikio yangu , nilienda hospitali ingine napo majibu yalikuwa yale yale kwamba nimeadhirika na UKIMWI .

Haya majibu yalimfikia mpaka bosi wangu nae akatambua hilo akasikitika sana nay eye alivyoenda kupimwa akakutwa hajaadhirika , basi nikajua moja kwa moja ukimwi nimepata kutoka kwa yule kijana wa mitaani na sio mtu mwingine .

Nikamwomba huyu kijana tukaangalie afya zetu kwa mara ingine tena hospitali , tukaenda kule kupima afya zetu , yeye ndio alikuwa wa kwanza kupokea majibu yake , alikutwa ameadhirika akupata mshituko wa ghafla yaani haamini .

Mshituko huo ulimpelekea aanguke chini na kuzimia watu walienda kumbeba na kumpeleka hospitali kupatiwa huduma ya kwanza basi hapo ndio magonjwa mengine yalianza kujitokeza na kujulikana sana .

Kumbe huyu kijana alikuwa na urafiki wa kimapenzi na shugamami mmoja mtaa wa pili huyu shuga mami mume wake alifariki dunia miaka 5 iliyopita kwa UKIMWI watu wanaema TB sijui , ndio huyu kijana kuona zile pesa za shuga mamy akaenda kwake .

Kijana aliumwa kwa miezi 3 hivi kisha akafariki dunia akaniacha duniani mwenyewe , kule kazini nilifukuzwa kaza na bosi wangu kisa nilitaka kumwambukiza ugonjwa wa ukimwi , lakini siku moja alinipigia simu kunieleza kwamba mke wake ameadhirika na UKIMWI pia lakini yeye anasema hajaadhirika .

Hapo ndio nilishangaa sana , kwanini mke wa aadhirike yeye asiadhirike au mke wake nae alikuwa anatoka nje ya ndoa bila mume wake kujua ? basiu hiyo ni siri yao nyumbani kwao mimi hayanihusu .

Lakini ndio hivyo nilikuwa nimeshaadhirika na UKIMWI kazi nimeshafukuzwa sina cha kufanya wala kutafakari nilifikiria zaidi kuhusu ugonjwa wangu wa UKIMWI na jinsi nitakavyoweza kuishi maisha marefu kwa matumaini .

KAHABA

Baada ya kuona maisha magumu na sina lolote la kufanya mimi kama mwanamke mrembo na mwenye mvuto niliamua kutafuta njia rahisi zaidi ya kujipatia kipitano nilifikiria njia nyingi sana ambazo zingeweza kunipatia angalau mlo na mavazi katika siku zangu za maisha zilizobakia baada ya kugundulika nina virusi vya ukimwi

Nikaanza kutafuta sehemu ambazo naweza kuuza mwili wangu kwa pesa za chapchap niweze kuendeleza maisha yangu ya kila siku , nilikuwa na ramani yangu kwanza pale OHIO , JOLLY , MACHENI , BILLS NA LATAVERNA hizo ni sehemu 5 kuu za starehe jijini dare s salaam kwahiyo huko naweza kufanya kazi za kujiuza kwa wiki nzima kila siku bila kuchoka .

Ohio ilikuwa nzuri ila tatizo lake ni kwamba kila anayepita pale anakujua halafu unatakiwa uonyeshe maungo yako hazarani mimi sikuzoea tabia hizo na sikuwa na mhemko huo kwahiyo nilivaa miwani yangu na kuacha mapaja nje tu waangalie wenyewe kama wanapenda watakuja . Kule macheni tatizo lake ni mashoga wengi sana , yaani mwanaume anaweza akaja kutafuta Malaya akakuchanganya wewe ni shoga , wale mashoga wanaojiuza hawana tofauti na sisi wanawake tunaojiuza wakati Fulani ulitokea ugomvi mkubwa watu waliamulia tulimgombea mwanaume .

Billa nako kuzuri ila vijana wengi sana halafu hawana pesa , na vitoto vidogo vingi , nilikuwa naogopa matatizo na vijana wa kule sikupenda kufanya mchezo na watoto wadogo waliokuwa wananitaka hata kwa dau gani nilingoja wanaume wenye pesa zao tu sio zaidi .

Basi nilianza safari za kuelekea jolly club kwa ajili ya kujiuza mwili wangu nipate angalau chochote cha kula na kufanya katika maisha yangu , pale jolly club nilikutana na dada mmoja anaitwa Aisha , huyu dada nae ni kahaba mzoefu akaanza kunionyesha mambo kadhaa wa kadha kuhusu biashara ya ukahaba na kadhalika . Hapa ndio nilijufunza kwamba sio makahaba wote ni masikini au hawajiwezi kuna wengine wanajiweza na wanazo fedha ila wanapenda kufanya ukahaba yaani wamechoka na dunia wengine walikuwa na wanaume wao wakaachika wakaamua kuja huku kwenda na mwanaume wowote yule anayekuja .

Wengine wana matatizo katika ndoa zao kupigwa na kadhalika wanaamua kuja huku kujiuza au kukaa huku ili kuepuka matatizo katika ndoa zao au mahusiano yao , wengine ndio kama hivyo waume zao hawana nguvu za kutosha kufanya nao tendo la ndoa wanaamua kuwa makahaba kila mtu na lake na mambo yake pia .

Wengine wanafanya huu ukabaha Kwa- ajili ya kupeleleza yaani ni wapelelezi wa polisi au watu Fulani katika serikali wako katika mitaa hii kuzuga tu , ili wafanikishe kazi zao za uchunguzi kama polisi wa usalama sehemu walizoko .

Mwisho wa yote siku hizi kuna vita kubwa katika biashara hii ya ukabaha mjini dare s salaam , mfano kule jolly kuna wazungu na wahindi wanakuja kufanya biashara ya ukahaba kwahiyo wewe mwamfrika unakazi ngumu kuwapita wale wazungu na wahindi au wachina .

Siku hizi wanaume wengi wanapenda kitu kinaitwa JICHO yaani kufanya mapenzi kinyume na maumbile , hii nayo ni soko kuu , mfano mwingine anaweza kuja kwako anataka jicho na wewe hutoi jicho maana yake unakosa soko suluhicho ni kujitoa mhanga na kufanya mapenzi kwa kuwa mteja ni mfalme .

Mbaya zaidi kuna wanaume wengine wanakuja wanaweza kukuchukua uende nao kufanya ngono kumbe wanakupiga filamu za ngono wakati unafanya kitendo hicho haswa wazungu wengine wanakupa ufanye mapenzi na mbwa wao au wanyama wao wengine mambo yanaenda hivyo .

Biashata hii ya ukahaba ilinichanganyia sana kwa miaka 2 niliyoifanya na kwa kweli hakuna aliyenijua kama nimeadhirika na ugonjwa wa ukimwi nilikuwa najitunza na kutuza siri zangu hizi kuu na sikupenda kuzoeana na watu sana hadi waniulize hivyo

Siwezi kuhesabu ni watu wangapi nimefanya nao ngono lakini ni zaidi ya 300 siku zingine nafanya kazi na watu zaidi ya 3 kwa siku moja kwahiyo mambo yanaendelea halafu wengi hawakupenda kutumia mipira ya kiume yaani kondo walipenda kuja hivi hivi tu bila kinga chochote kile

Na mimi nilikuwa nimeshaadhirika nilichokuwa natafuta ni fedha za kuendeleza maisha yangu kwahiyo hata kama nikifanya ngono zembe bila kinga mimi hainiumi sana kwa kuwwa nilishajua hali yangu sikuweza kuitengua siku wa chochote cha kufanya zaidi ya hichi .

Hii ilikuwa ni kulipiza kisasi kwa maasi ambayo yule kijana alinifanyia kuniambukiza UKIMWI kwa makusudi huku akijua kabisa ameadhirika siku nyingi ,kwakuwa yeye ameamua kuniuwa mimi basi na mimi nauwa wengi zaidi na sijali kuhusu dhambi hizi nilizozifanya na sijutii kabisa .

MAISHA YA MTAANI

Huku mitaani waliniita majina kama JLo wakati mwingine salma hayek yaani wale waigizaji maarufu duniani kwa urembo nilio nao na mvuto wake , hakuna hata mmoja aliyekuwa na mawazo kama nimeadhirika au la kwa maana yule kijana niliyekuwa nae kama mpenzi alikufa kifo cha ghafla watu walisema amekufa kwa pressure .

Mitaani napo nilikamua kinoma , waume za watu walikuja mpaka mlangoni kwangu na magari yao , wananipakia na kunipeleka katika kumbi za starehe na sehemu nyingine nyingi sana wengine walinihonga mali na mambo kibao kisa wamenipenda wanataka ngono

Na kwa uhakika hawa wanaume niliwapanga sawia kabisa na hakuna aliyeweza kutambua mimi nina wanaume wangapi na wanaishi wapi wengi walijua ni washirika wangu katika kazi zangu na mambo yangu mengine kwanza sikupenda kuongea na mwanaume wowote chumbani kwangu wote nilikuwa nawaambia tukutane mbali kidogo na nyumbani haswa kati katika ya jiji .

Katika hawa wateja wangu kulikuwa na kijana mmoja anayeitwa juma huyu juma alikuwa na rafiki yake mmoja anayeitwa Shy , kijana mwembamba mwenye umbo la wastani , hana ndevu halafu ni mcheshi sana , alifanikiwa kuiteka moyo wangu , sasa nilitaka kumwambia mara kibao kwamba nimemzimia

Tatizo ni kwamba anayekuja kunichukuwa pale ni juma , juma huja pale kwa kusindikizwa na Shy , basi juma akanitambulisha katika website moja inayoitwa darhotwire www.darhotwire.com , nyumbani nikienda kupumzika nilipenda kushinda katika tovuti hii kuchat na marafiki na watu wengine .

Huyu shy nae nilimkuta katika site hii usiku wa manane anachat na jamaa zake , ila siku moja nilikutana na kijana mwingine anayeitwa politeman , huyu ndio alinichanganya kabisa , kwanza jina lake na jinsi aliyokuwa anaongea kweli nilizimia mwenyewe bado nikawa na siri kubwa moyoni je hivi tukifanya ngono inakuwaje ?

Maisha yaliendelea tu , basi nikimpenda politeman , huyu kijana akawa anakuja mpaka nyumbani kwangu wakati mwingine na huwa nampa computer yangu aitumie tukaenda zaidi nilimshitukia kumbe huyu polite ana urafiki wa kimapenzi na dada mwingine anayeitwa salma siku moja walipanga kwenda kufanya mapenzi lakini polite akakataa ?

Sikuamini macho yangu wala masikio siku nyingi kama naota kumbe polite alikuwa na urafiki na dada mmoja anaitwa Maria Chipz ?? Sikuamini , nilimuheshimu sana maria na sikutegemea kama anaweza kufanya hivyo hata siku moja , muda ukaenda kumbe kuna dada mwingine anaitwa REHEMA naye alikuwa anampenda Politeman Miss upanga Naye anampenda Politeman we acha tu

Nikamwaga chini sikupenda tabia zake za kitoto kitoto anazowafanyia hao kina dada wengine ingawa nilifanya nae mapenzi kama mara 4 hivi na mara zote hatukutumia kinga na nilikuwa nimeadhirika ila ni siri yangu , polite hajui na wengine wote hawajui lakini ndio maisha hayo

Haya ndio hivyo , nami sasa hivi nakaribia kufariki dunia niko zangu kitandani hapa hospitali ya Amana mkoani dar es salaam , kweli maisha ni safari ishi upendavyo na sio watakavyo , mwisho wa yote dunia sio hadaa wala dunia haikuchukii au haitaki kukufanyia chochote kibaya

Bali watu ndio hadaa , hata kama ni ndugu yako rafiki yako , hakikisha humpi nafasi akutawale aweze kukumiliki wewe na kukuamrisha chochote kile anachotaka yeye , kama ukifanya hivyo ndio utaishia kubaya kama mimi

Bosi wangu alinimiliki sana nikampa penzi , kijana wa mitaani nae alinimiliki mpaka sasa nimeaona faida zake na hasara zake

Wacha ningoje siku zangu nife nizikwe niende ahera Kwaheri .

UTAMU WA BINAMU

Image result for HANDSOME AFRICAN BOY


Chriss ni kifupi cha jina Christopher jina nililopewa na mama yangu mara tu baada ya kunizaa.Alinipa jina hilo ambalo linafanana na jina la baba yangu kama kumbukumu yake mara baada ya baba yangu kufariki ningali nikiwa tumboni.
Chriss kama wengi wanavyopenda kuniita nimezaliwa katika mazingira ya kijijini ambapo ata huduma za kijaamii kama umeme, maji na hospitali ni shida.Nilizaliwa huko mkoani Iringa na shughuli kubwa ya mama yangu ni kilimo tena kilimo cha jembe la mkono.
Katika hayo hayo mazingira magumu niliweza kusoma na kufaulu vyema mpaka nikafanikiwa kupata degree yangu ya kwanza katika chuo kikuu cha Dodoma.Baada ya hapo nilirudi kijijini kwenda kuendelea na maisha yetu.Kipindi nilichomlaiza chuo kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwani mama yangu alikuwa mgonjwa sana akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya titi.
Hali hiyo ya ugonjwa ilinipelekea mimi kutumia hela zote za akiba nilizojiwekea kutokana na mkopo niliokuwa nikipewa na serikali.Ndoto zangu za kuanzisha biashara kwa kutumia pesa hizo zikayeyuka.Nashukuru ingawa hela ziliisha lakini mama alipona na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Ni mwaka wa pili sasa tangia nimalize chuo na sijapata kazi.Hali inayonifnya nizalilike sana pale kijijini kwetu.Vijana wenzangu ambao hawakupata nafasi ya kusoma wamekuwa wakinisimanga kwa madai kuwa nilipoteza mda wangu kusoma mpaka chuo kikuu.
Watoto wa kike nao wamekuwa wakinikataa kwa madai kuwa sina kitu cha kuwapa.Hali ilikuwa mbaya zaidi pale mpenzi wangu niliyempenda kwa dhati alipoamua kuniacha na kuolewa na mwanaume mwingine kwa madai kuwa amechoka kunisubiri.
Maisha ya kijijini yalinichosha sana na nikaanza mikakati ya kwenda mjini mahali ambapo niliamini ningeweza kupata kazi kirahisi.Mtu wa kwanza kumfikiria ni mjomba wangu ambaye alikuwa jijini Mbeya.Huyu ni tajiri mkubwa sana lakini ndugu zake pamoja na mama yangu wamemtenga kwa madai kuwa ni mbinafsi, mchoyo na pia wanamuhusisha na imani za kishirikina.
Tabia yangu ya kuishi vizuri na kila mtu na kutoamini imani za kishirikina ilinifanya mimi niweze kupendwa sana na mjomba wangu huyo.Katika ukaribu huo mjomba alinihadi kunitafutia kazi kama tu nitaweza kwenda kwake huko jijini Mbeya.
Basi siku moja alinipigia simu na kuniomba niende kwake kwa sababu mfanya kazi wake wa kazi za nje(houseboy) aliondoka ghafla hivyo nikamsaidie saidie kazi ndogo ndogo huku na yeye akiendelea kunitafutia kazi.
Kwa kuwa nilishachoka kukaa kijijini na tayari nilishakuwa na jeraha ya kuachwa na mpenzi wangu niliona hiyo ndio sababu pia ya kondoka kijijini.Nilims
hirikisha mama yangu swala hilo ingawa yeye alinipinga vikali kwa kigezo kuwa mjomba wangu huyo si mtu mzuri kwa sababu ana mambo ya kishirikiana.
Kwa kuwa mimi sikuyaamini hayo maneno nikijua ni chuki tu za ndugu kwa sababu ya mafaniko ya mjomba hivyo nilimshawishi mama mpaka akakubali.Basi nilijiandaa nikapanda gari na kuelekea jijini Mbeya.Siku nasafiri mjomba alinieleza kuwa yeye na mkewe wamepata safari ya kwenda Zambia ila nikifika nitapokelewa na mwanaye yaani binamu yangu Lisa.
Kweli nilivyofika stend nilipokelewa na binamu yangu Lisa.Tangia nikiwa stend nilishitushwa sana na uzuri aliokuwa nao dada binamu huyo.Nikajikuta nikimtamani na kujisemea laiti ningepata demu kama huyu ningemtia mimba siku ya kwanza tu atakayenifunulia mapaja.Tulifika nyumbani tukamkuta binti mwingine ambaye bila hata kutambulishwa nilijua tu alikuwa ni dada wa kazi(house girl).
Samia huyu ni kaka yangu binamu anaitwa Chrisss.Chriss huyu ni dada yetu wa hapa nyumbani anatusaidia kazi anaitwa Samia.Huo ulikuwa ni utambulisho mfupi mara baada tu ya binit huyo kutupokea mizigo.Alionekana mwenye raha na aliyefurahia maisha ya hapo nyumbani.
Basi nikawa nimeingia kwenye jumba la mjomba jumba dogo sana lakini la kifahari.Nilioneshwa chumba nikaweka mizigo na baada ya kuoga kisha kula niliamua kwenda kulala.*****
Taswira ya umbo na sura ya dada yangu binamu mtoto wa mjomba zilitosha kabisa kuninyima usingizi usiku wa siku ya kwanza kufika katika jiji la Mbeya.Licha ya ugeni niliokuwa nao lakini mapokezi mazuri ya binti huyo yalinifanya nivutiwe naye ghafla.
Uzuri wake wa umbo la kibantu ulinimaliza tangu alipokuja stend kunipokea.Japo alikuwa ni ndugu yangu lakini sikujua kwa nini hali hiyo ilinitokea.Nilijaribu kuzuia hisia zangu lakini ilishindikana nikajikuta mtarimbo wangu ukiwa unasimama bila adabu na kuinua sehemu za mbele ya suruali yangu kila nilipovuta taswira ya utamu aliokuwa nao kutona na umbo lake na sura yake nzuri aliyojaliwa na mungu.
Ingawa ni usiku lakini kwa kweli nilishindwa kulala katika chumba nilichokaribishwa nilale.Ndio nilishindwa kulala maaana kwenye chumba hicho ndicho alikuwa akilala binamu yangu huyo na alinipisha kutokana na uhaba wa vyumba.
Kwenye chumba hicho kulikuwa na picha za binti huyo na kila nilipozaingalia sehemu zangu za siri ziliumuka na kusababisha kukosa usingizi.Nilisindwa kuelewa kwa nini hali hiyo ilinitokea siku hiyo wakati mimi nilishazoea kujizuia na huwa sina taamaa za kijinga.Kwa mara ya kwanza nilipata hamu ya kujichua(kupiga punyeto) kwa kungalia picha hizo za dada binamu yangu.
Wakati naendelea kuwaza jinsi ya kupiga punyeto ili niweze kulala nilisikia mtu akigonga mlango wangu.Nilishindwa kuelewa nifanyaje maana viungo vyangu vya siri vilikuwa vimesimama wima. “samahani binamu naomba ufungue mlango mara moja nichukue mafuta yangu niliyasahau ili asubuhi nisikusumbue” alisema mgongaji wa mlango huo kuashiria kuwa alikuwa ni binamu yangu ambaye picha zake ndo zilikuwa zikininyima usingizi.
Nilijifunga vizuri kwa kutumia shuka nililokuwa nimejifunika ili kuficha mtarimbo ambao ulikuwa umesimama kama nguzo ya umeme.Bado haukutaka kukaa vizuri lakini nilijitahidi kuulazimisha ulalie pembeni kisha mimi nikaenda kufungua mlango.
“Samahani kwa usumbufu alisema binamu huyo mara baaada ya kunipa tabasamu zito”Nilibaki nimemtumbulia macho mara baada ya maneno hayo maana alikuwa ndani ya khanga moja ambayo ilikuwa imetepeta maji kuashiria kuwa alikuwa ametoka bafuni kuoga.
Na hiyo ndo sababu alikuwa anataka mafuta yake akajipare usiku huo.Nilipitisha jicho la wizi kuanzia kifuani kisha tumboni na baadaye chini ya kitovu nikajikuta nazidi kusimka kwa jinsi dada binamu alivyokuwa mtamu.
Niliporudisha tena macho yangu juu nilikutana na macho ya dada binamu yakiwa laini yaliyolegzwa kama mtu aliyetoka kufanya mapenzi mda huo.Wote tuliganda na kila mmoja akimuangalia mwenzake kwa jicho la matamanio.Ghafla…… ***********ITAE
NDELEA********

SIRI CHUMBANI

Image result for HOT african girl
Huyu ni Manka, mmh jamani Manka anawachanganya akina kaka, wajomba na hata wazee, oshiii! Kwa kifupi hana kasoro, ukibahatika kumuona na kumchambua ungeweza kudhani ukikufuru kuwa pengine mama yake aliamua kumuumba mwanaye mwenyewe na kuhakikisha amekuwa mzuri lakini ukweli kazi hii kubwa ya uumbaji ilifanywa na Mwenyezi Mungu pekee, mtoto ana kisura kilaini kama cha mtoto mchanga, ngozi nyororoo...sijui ana kula nini, meno meupe yenye mwanya wa wastani, akicheka hakika utapenda, wasichana wenziye wanamtamani, wanataka awe na umbo kama lake, wanaume wanaotaka kuoa wanaweke wazuri waliomuona wanachukulia mfano wa Manka, hana maringo hiyo ndiyo sifa yake kuu, ana umbo la kuwateka watu wa kila rika.
Siku hiyo alibaki mwenyewe, nyumbani kwake maeneo ya Sinza kwa Remmy, alikuwa alifanya usafi na baadaye akaendea bafuni kuoga, alijisugua na alipomaliza aliingia chumbani na taulo laini akajifuta maji mwilini na kuanza kupakaa mafuta ya kuirutubisha ngozi yake, kila alipojiona kiooni alimsifu mwenyezi Mungu kwa kazi nzuri ya uumbaji.
Mbele ya Dressing table yake iliyojaa vipodozi vya dharama, alitoa manukato ya J- Lo na mafuta ya Max Clare na St Elizabeth Aden, alipomaliza akapakaa uso wake ‘poda’ kidogo kisha akavaa sketi fupi inchi 12 na kitopu kilichoacha wazi kitovu chake kilichoingia ndani nusu inchi, hali iliyomfanya avutie sana, juu ya kitovu alikuwa na matiti makubwa kiasi yenye kuleta yaliyojaa na kusimama kwa kujitegemea ingawa alivaa sidiria.
Simu ikaita, akatembea kivivu na kuiokota, hakujua ni nani, zilikuwa namba mpya kutoka nje ya nchi.
“Haloo! Manka...Habari za Tanzania!” Sauti ya upande wa pili ilisikika.
“Nzuri, shikamoo!” Manka alishaijua sauti ya mtu aliyepiga.
“Jamani, si nilikuambia sipendi shikamoo, ok, unaendeleaje?” Ilikuwa sauti ya mzee Alex Ganza, mfanyabiashara maarufu jiji la New York na Afrika mashariki, ni mtanzania aliyezaliwa Kilimanjaro na kununua uraia Marekani.
“Safi! Nimekumisi sana Anko!” Manka alipenda kuita Anko, ingawa siri halisi hakuwa Anko.
“Mi’zaidi, naomba uniite mpenzi...Manka hukumbuki nilikulea ili uwe mke wangu!”
“Najua na nakuheshimu kama baba yangu, umenilea na nilikuwa nataka upate mkwe siku za karibuni!” Manka alisema , lakini kauli hiyo ikamtibua Alex.
“Mkwe! Nooo! Usiolewe na mwanaume mwingine, nitakuoa mimi, nakupenda Manka, toka ukiwa na siku moja duniani nilikulea, nataka nile matunda yangu..”
“Sijui kama itawezekana, tayari ninaye mwanaume ninayempenda!”
“Mwanaume gani mzuri kuliko mimi, mwanaume gani tajiri kushinda mimi, mwanaume gani ambaye angeweza kukuokota jalalani na kukusomesha hadi leo una elimu ya juu na unasimamia mali zangu? Wewe ndiye mke wangu, Manka...nakupenda!”Alilalaimika kimapenzi, Manka akajikuta akimuonea huruma, lakini bado alikuwa ana ampendaye.
“Ok, nimekuelewa, njoo basi tuongee vizuri, nakupenda wewe pamoja na huyo mpenzi wangu anayeitwa Boy...” Kauli hiyo ilimrufahisha nusu na kumuudhi nusu, iliyomchukiza ni kwamba anampenda pia Boy.
“Sawa, nimeota ndoto ya ajabu, usiku wa kuamkia leo!” Akabadili mazungumzo mzee Alex Ganza.
“Ndoto gani?”
“Siri ya Chumbani!”
“Unamaanisha nini, sijakuelewa mpenzi!” Naye akaamua kumfurahisha kwa kumuita mpenzi.
“Nikija nitakueleza, mapumziko mema mpenzi wangu!mmwaaa!”
“Na wewe pia! Mmmwaaaa!” Alimaliza na kukata simu.
******
Alipokata simu, akatafuta jina la mpenzi wake anayetingisha mtima wake na kumpigia, huyo ndiye aliyetaka kumkabidhi mwili wake auendeshe anavyotaka.
“Boy, njoo basi unipeleke kiwanja, ninazo hela za kutumia mpenzi wangu, njooo! Nipo nyumbani peke yangu,” alilalamika kikike akizungusha jicho la mahaba, jicho ambalo akikukata lazima apagawe na kudhani anakutamani, mtoto huyu! Mmh!.
“Poa, upo wapi?”
“Njoo nyumbani, msaidizi wangu wa kazi za ndani hayupo, nakupenda sana na usichelewa!”
“Nakuja usijali!”
“Mwili mzima unachemka, naomba ujiandae, kuna zawadi nitakupatia kwanza, ndipo twende zetu viwanja..njoo naumia!”
“Heeh! Unaumia kitu gani sweet!”
“Nakusubiri, usichelewa damu inachemka, natamani joto la karibu ...” kumbe Boy hakuwa mbali alikuwa maeneo ya Sinza madukani, akashuka kwenye daladala na kuelekea mtaa wa pili alikokuwa akiishia Manka, jumba la kifahari lililojengwa na Alex Ganza, alipofika alifungua mlango na kuingia hadi sebuleni ambako alimkuta Manka amejilaza sofani akiwa mweupe pee! Loh! Macho yakamtoka si kidogo, ilikuwa ni maajabu ambayo hakuwahi kukutana nayo, mtoto alifumba macho sijui alihisi baridi ama vipi, alikuwa amemtega si kidogo.
Siri Chumbani- 2
Baada ya kutoka bafuni, Manka msichana mwenye sifa zaidi ya mrembo anapigiwa simu na Alex Ganza, anamtaarifu kuwa anataka kurejea nchini huku akimuomba Manka asimuite anko na badala yake amuite mchumba, Manka anakataa akidai tayari anayealiyemchagua na kwamba anampenda sana.Je, ni mwanaume gani anayemchanganya Manka, Alex atafanya nini? Kumbuka huu ni mwanzo wa chombezo hilo la kusisimua......
Neno hili likapita tena akilini mwa Alex, “Sijui kama itawezekana, tayari ninaye mwanaume ninayempenda! Pole sana Alex!” Akauma meno na kukunja ndita, kuliko kumkosa Manka ilikuwa afadhali kufa, alimdharamikia sana na kumlea mpaka alipofikia hapo anatamaniwa na mwanaume mwingine, siri kubwa ya Manka aliifahamu.
Sekunde kadhaa alizokaa kimya, akazinduka mithili ya mtu aliyetoka katika ndotoni ya kutisha na kusema jasho likimtoka.
“Mwanaume gani mzuri kuliko mimi, mwanaume gani tajiri kushinda mimi, mwanaume gani ambaye angeweza kukuokota jalalani na kukusomesha hadi leo una elimu ya juu na unasimamia mali zangu?
Wewe ndiye mke wangu, Manka...nakupenda!”Alilalamika kimapenzi, Manka akatulia akimsikiliza kwa makini, ingawa hakuwa na uhakika kama aliokotwa jalalani lakini mwanaume huyo ndiye aliyemlea kama mzazi wake, alimsomesha na kumkabidhi mali zake azisimamie, siku zote alimheshimu na asingependa kuolewa na mtu toka utotoni mwake alimuita Anko.
Roho ya huruma ikamuingia, akabaki njia panda kuendelea na mwanaume huyo ama kuendelea na kipenzi chake, moyo ukakataa na kudai kuwa, “Umemchagua John Mule, basi huyo ndiye unayetakiwa kuwa naye,” sauti kutoka moyoni iliendelea kumsihi.
“Manka...nisikilize basi mpenzi!” Sauti ya Alex ilisikika, lakini ya chini na ya kubembeleza.
“Mmh! Sawa nimekuelewa, njoo basi tuongee vizuri, nakupenda wewe pamoja na huyo mpenzi wangu anayeitwa John...” Kauli hiyo ilimrufahisha Alex nusu na kumuudhi nusu, iliyomchukiza ni kwamba anampenda pia John.
“Sawa, nimeota ndoto ya ajabu, usiku wa kuamkia leo!” Akabadili mazungumzo mzee Alex Ganza.
“Ndoto gani?”
“Siri ya Chumbani!”
“Unamaanisha nini, sijakuelewa mpenzi!” Naye akaamua kumfurahisha kwa kumuita mpenzi, na kweli Alex alifurahi sana, pesa kwake zilikuwa hazina maana bila Manka.
“Nikija nitakueleza, mapumziko mema mpenzi wangu!mmwaaa!”
“Na wewe pia! Mmmwaaaa!” Alimaliza na kukata simu, Manka akamuwaza tena muhibu wake, kila alipomuwaza alikosa hamu ya kula na kuhisi kama vile mgonjwa.
******
Alipokata simu, akatafuta jina la mpenzi wake anayetingisha mtima wake na kumpigia, huyo ndiye aliyetaka kumkabidhi mwili wake auendeshe anavyotaka, alitaka kula raha za dunia akiwa na John Mule.
“John, njoo basi unipeleke kiwanja sasa hivi, ninazo hela za kutumia mpenzi wangu, njooo! Nipo kitandani peke yangu,” alilalamika kikike akizungusha jicho la mahaba, jicho ambalo akikukata lazima apagawe na kudhani anakutamani, mtoto huyu! Mmh! Jamaniii anamvuto kila mahala.
“Poa, upo wapi?” Sauti nzito ya kiume na iliyopoa ilisikika, moyo wa Manka ukapasuka paaa’ hizia za huba zikamuingia mara moja.
“Njoo nyumbani, msaidizi wangu wa kazi za ndani hayupo, nakupenda sana usichelewa mpenzi!”
“Nakuja usijali!”
“Dakika ngapi?” Manka alihoji, ili ajiandae haraka na kuonekana mpya, si unajua tena wawili wawapo faragha lazima wajiandae fresh?.
“Robo saa,” alimjibu akihisi moyo ukimdunda.
“Mwili mzima unachemka, naomba usichelewe kuna zawadi nitaka nikupatie kabla hatujatoka OUT..njoo dear naumia!”
“Heeh! Unaumia kitu gani sweet!”
“Nakusubiri, usichelewa damu inachemka, natamani joto la karibu ...” kumbe John hakuwa mbali alikuwa maeneo ya Sinza madukani, akashuka kwenye daladala na kuchukua teksi mara zote Manka alimuonya kutopanda daladala, hiyo akajua ni sooo kuingia jumba la Manka na kumi na moja zake.
Jumba hilo juu lilikuwa na mnara uliandikwa Alex Ganza, walinzi walikuwepo wa kutosha kabisa, alipofika na kwakuwa alifahamika na walinzi, alifungua mlango pua zake zikakubwa na gharika la manukato yaliyopoa na yenye kuvutia, akatembea taratibu sebuleni ambako alimkuta Manka amejilaza sofani akiwa mweupe pee! Loh! Macho yakamtoka si kidogo, ilikuwa ni maajabu ambayo hakuwahi kukutana nayo, mtoto alifumba macho sijui alihisi baridi ama vipi, alikuwa amemtega si kidogo.
Alipofika John alipiga magoti na kuisogeza kichwa chake katika kitovu cha Manka, akatasua midomo iliyojaa mate ya huba na kumbusu mara mbili akapata taratibu huku akimwita Manka jina lake, kumbuka sauti hiyo iliendelea kuwa nzito la kimapenzi.
“Mankaa...unaniga mamaaaa...sweeetii naomba nikufunike...” Ndani ya sebule hiyo ya kifahari kulikuwa na kiyoyozi cha kotosha kabisa, wote wakawa wanapigwa na ubaridi fulani.
Taratibu mkono usio na adabu wenye kutekenya ulipita ukitalii taratibu na kufikia hatua ya kumfanya Manka afumbue macho ya ya kurembua.
“Hey sweet umekuja mpenzi wangu, nashukuru karibu,” Manka aliinuka na kumkaribisha John aketi sofani, baadaye akakibamba kila mmoja alimbamba mwenye kiuno wakaingia chumbani ambako Manka hakutaka kitu kingine zaidi ya zawadi aliyomwandalia mpenzi wake kwa muda huo.
“Mbona unazima simu mpenzi...” Manka alimuuliza, akijitupa kitandani, naye John akafuatia.
“Si unajua mambo haya hayahitaji usumbufu, hivi simu ikiita nikawa katikati ya bustani napalilia mboga mboga, si itanikata ‘stimu’,”
“Poa, si unaiacha iite mpaka ikatike, naona wivu!” Alisema akipitisha mikono yake kifuani mwa John aliyeanza kuongea kwa sauti nzito huku Manka sauti yake ikiwa nyororo zaidi, kila mtu alikuwa na shauku ya palilia bustani na kuhakikisha bustani yao inakuwa bora, kwani walihitaji kupanda mmea, wenye rutuba na utakao mfariji kila mmoja aibuke na faraja moyoni, mmh! Sijui mwiye nahadhia.
“John...taratibu, mashuka meupe...” ilikuwa sauti ya Manka akijipindua upande wa kaskazini baada ya kuona mwenyeye ana kasi katika kucheza mduara.
“Mashuka meupe.. taulo inachafuka wakati mtu ametoka bafuni kuoga, acha yachafuke baby...”
“Nina zawadi nyingine...” Manka alisema kwa sauti ya kitetemeshi mapigo ya moyo yakienda kasi.
“Ipi!”
“Subiri, ulishawahi kukutana na mwanamke mwenye mapengo ya mbele...” Alisema Manka.
“Hapana!” Manka akainuka kwenda bafuni alipotoka alikuwa amefanya usafi, mapengo yake ya mbele katika meno manne yalionekana safi na yakupendeza.
Hakujua, kumbe meno ya dhahabu ya Manka yalikuwa si urembo bali hakuwa na meno, akasogeza midomo yake na kugusanisha na midomo ya John. Hapo alikuwa mambo mengine kabisa, usijaribu! John alipagawa na kuchanganyikiwa, kwani ulimi wake haukupata tabu katika kutalii na kubadilishana mate.
Baadaye wakati John akiwa hoi taabani, Manka akatoa choculate kwenye jokofu na kummegea John kisha kumlisha na John akammegea Manka kipande kidogo, wakaanza kumumunya taratibu hali iliyowachanganya na kuwafanya warukwe na akili. Kuanzia siku hiyo, wote walichanganywa katika penzi na kutamani kukutana kila mara.
“Tulale kwanza kisha baadaye twende Club Billicanas” Alishauri Manka lakini mambo aliyopewa ya muda mfupi na Manka yalimchanganya. John hakutaka kulala alitaka kuendelea kurina asali.
********
Siku alipozaliwa Manka, ndipo mama yake kwa bahati mbaya alifariki na kumuacha Manka aliyelelewa hospitalini, na baadaye akachukuliwa na baba yake hadi nyumbani akaletewa wasichana watatu wa kumlea, hiyo yote ilifanywa na Alex Ganza, baba yake Manka.
Siku zote, Alex alihakikisha mwanaye wa pekee hajui siri hiyo, wasichana hao wa kazi aliwafahamisha kuwa wasije kuifichua siri hiyo, akiwa chekechea mzee Alex alionekana kumtamani sana mwanaye aliyefanana na marehemu mchumba wake, Angela. Msichana Angela alikuwa ni mchanganyiko wa mzungu na mwafika, kila kitu Alex alikifanya siri. Manka alipofikisha umri wa miaka saba alijaribu kumuuliza Alex kama mama yake alikuwa wapi na yeye ni nani wake, kwa hisia Alex akamweleza Manka kuwa siku moja usiku wa manane akiwa anatembea alisikika mtoto akilia jalalani, aliposimama aliweza kugundua mahala alipo, alichokifanya ni kutembea hadi jalalani na kumuokota mtoto aliyekuwa amebabuka mwili kwa joto na kuhifadhiwa kwenye mfuko wa plastiki.
“Mmh! Mtoto huyo alikuwa nani?”
“Huwezi kuamini, wewe ndiye niliyekuakota na kwa vile sikuwa na mke wala mtoto nilihakikisha nakulea vizuri na baadaye uwe mke wangu!” Alisema Alex kwa hisia kali, alimdanganya mwanaye mpendwa. Alikuwa mzuri sana na kumfanya aingiwe na hisia za ajabu.
Itaendelea

MY WIFE...SEHEMU YA 1-8


                                                              MY WIFE....EP.1.

Katika maisha yangu sikuwahi kuwaza kuua hata nzi kutokana na huruma niliyokuwa nayo.
Watu wengi walipenda kuniita mlokole japo historia yangu yote niliishi maisha ya kutokuwa na dini nikiamini Mungu wa Wakristo ndiye Mungu wa Waislamu kutokana na mafundisho ya dini zote niliyoyafuatilia.
Utashangaa kwa nini niliishi bila kuwa na dini ikiwa wazazi wangu wana dini, tena dini tofauti, baba Muislamu na mama Mkristo. Katika maisha yao hakuna aliyekubali kumfuata mwenzake na kukubaliana, kila mmoja aishi katika imani yake. Hivyo basi, nikawa mtoto wa wazazi wa dini mbili, pamoja na wazazi wangu kuishi kila mmoja na dini yake, waliishi katika upendo wa hali ya juu kwa kila mmoja kuheshimu imani ya mwenzake.

Nilipopata ufahamu nilijikuta nipo njia panda kwa vile sikutaka kumuudhi mmoja wa wazazi wangu kwa kumpendelea mmoja. Halafu kitu cha ajabu nilikuwa mtoto mmoja kama roho, hivyo niliamua kusimama katikati ya wazazi wangu kwa kutochagua dini yoyote. Lakini nilikuwa nafahamu kipi mwanadamu anatakiwa kukifanya ili usimuudhi Mungu.

Katika maisha yangu yote niliamini tofauti ya dini mbili ni ndogo sana lakini anayetakiwa kuabudiwa ni Mungu mmoja. Tokea hapo niliishi nikiwa sina dini na kuishi kama mpagani, tofauti yangu nilikuwa najua Mungu ni mmoja na ndiye anayetakiwa kuabudiwa, lakini sikwenda msikitini wala kanisani na malumbano ya dini hizi mbili mimi yalikuwa hayanihusu.

Wazazi wangu nao walikubaliana na mimi baada ya ushawishi wa kila mmoja kugonga mwamba. Huu ulikuwa muktasari wa maisha yangu ya awali ya kunifanya nisiwe na dini kwa ajili ya mapenzi ya wazazi wangu.
Kutokana na malezi mazuri ya wazazi wangu, niliweza kuishi sehemu yoyote na mtu wa aina yeyote, siku zote heshima na ucheshi ndivyo vilinifanya watu wanipende.

Kama nilivyosema awali, nilikuwa mtu wa huruma na heshima kwa wakubwa na wadogo, lakini mateso ya mapenzi yalinifanya nigeuke niwe na roho mbaya kukiko shetani.

Kuna maelezo niliwahi kusikia wakati nakua kwamba kuna matendo mengine shetani anakimbia akimuona mwanadamu anatenda. Baada ya kuteswa sana na mapenzi ilifikia hatua kutoa roho ya mtu kwangu ilikuwa kitu cha kawaida hata kwa kosa dogo la kuombana msamaha kwa kuamini hakuna kiumbe kibaya duniani kama mwanadamu ambaye hatakiwi kupewa nafasi kwa vile kama ukimchekea basi atakuumiza wewe.

Mkasa wangu unaanzia pale nilipotimiza miaka 21, nilitoka kwa wazazi wangu na kusafiri nje ya mkoa kwenda kufanya kazi baada ya rafiki yangu kupata kazi ya ujenzi.


Hivyo, hakutaka kuondoka peke yake, alinichukua na mimi huku wazazi wangu wakiniasa niishi na watu kwa heshima na taadhima. Nami niliwaahidi wazazi wangu kuwa nitaishi kama walivyonielekeza.
Nilitengana na wazazi wangu kwa mara ya kwanza toka nitoke tumboni kwa mama wangu. Nilifika mkoani na kufikia kwa ndugu wa rafiki yangu. Kwa vile tulifika Jumamosi jioni sana, tulilala na kesho yake tulipumzika na kupata nafasi ya kupelekwa sehemu ya kazi.

Ulikuwa mradi mkubwa sana ambao tuliambiwa utachukua miaka mitano kwisha, siku ile tulipumzika na kesho yake tulikwenda kuanza kazi. Siku ya pili tuliamka asubuhi na mapema na kwenda eneo la ofisi ambapo ndipo mnapangiwa kazi. Ilikuwa kuna tofauti kubwa na vijana wengi tuliowakuta nje ya geti wakisubiri kuitwa, lakini sisi tulikuwa na mwenyeji, mjomba wa rafiki yangu ambaye alikuwa ndiye msimamizi mkuu wa mradi ule ambao ulikuwa chini ya Wataliano, tuliingia bila kuitwa.
Basi huo ndiyo ukawa mwanzo wa kuanza maisha ya kujitegemea, tulianza kwa kulipwa kwa kutwa kama wenzetu kwa wiki mbili, baada ya hapo tulichaguliwa vijana kama ishirini tuliopewa mkataba na kulipwa kwa mwezi na posho yetu kuongezeka tofauti na wenzetu waliokuwa wakilipatwa kwa kutwa.
Maisha yalikwenda vizuri huku mimi na mwenzangu tukihama kwa ndugu zake na kupanga chumba kimoja na kukaa wawili. Wazazi wangu nao walikula jasho langu kila mwezi kwani niliwatumia robo ya mshahara wangu nao walizidi kuniombea kwa Mungu ili niendelee kupata zaidi.

Siku zilikatika huku nami nikipevuka kiakili na mawazo kufikia hatua ya kuhitaji mwenza. Nyumba tuliyokuwa tumepanga kulikuwa na binti mmoja ambaye Mwenyezi Mungu alimjalia umbile dogo lakini nzuri na sura jamili (nzuri). Binti yule alitokea kunipenda sana kiasi cha kumueleza mama yake angependa aolewe na mimi.
Moja ya njia ya kuonesha ananipenda aliniomba mambo yote ya kike ayafanye yeye kama vile kunipikia chakula cha jioni baada ya kazi, kufua nguo na kusafisha chumba lakini sikumpa nafasi ile kwa kuhofia wazazi wake.
Pamoja na mimi kumpenda sana bado sikumkubalia kutokana na kuwaheshimu sana wazazi wake ambao siku zote walinilea kama mtoto wao.

Siku moja usiku baada ya kutoka kazini, mama mwenye nyumba ambaye ni mama mzazi wa yule binti aliniita kwa kumtumia yule binti. Nami niliitikia wito ule, baada ya kuingia sebuleni kwao, nilikaribisha kwenye kochi lililokuwa karibu na alipokaa mama mwenye nyumba.



MY WIFE....EP.2.

Siku moja majira ya usiku baada ya kutoka kazini mama mwenye nyumba ambaye ni mama mzazi wa yule binti aliniita kwa kunmtumia yule binti. Nami niliitikia wito ule, baada ya kuingia sebuleni nilikaribisha kwenye kochi lililokuwa karibu na alipokaa mama mwenye nyumba.
SASA ENDELEA...
“Kazala,” mama aliita kwa sauti ya chini.
“Naam mama,” niliitikia kwa unyenyekevu mkubwa.
“Nimekuita mwanangu nikueleze jambo moja la muhimu sana.”
“Sawa mama.”
“Kwanza wewe dini gani?”
“Sina dini,” nilimjibu kwa mkato.
“Muongo, hebu niambie ukweli wewe ni dini gani?”
“Kweli mama sina dini.”
“Sasa kama ukipata mwanamke mwenye dini utafanya nini?”
“Sitafanya chochote nitaiheshimu dini yake, lakini mi nitabakia sina dini?”
“Kwa nini?”
Sikumficha nilimuelezea maisha ya wazazi wangu na kitu gani kilichonifanya nisiwe na dini.
“Lakini hata kiserikali mtu anapotimiza miaka kumi na nane ana haki ya kuamua chochote bila kuingiliwa, hivyo ulikuwa na nafasi ya kuchagua dini yoyote ya baba au ya mama.”
“Ni kweli, lakini bado kwa mimi sikutakiwa kufanya hivyo.”
“Kwa nini?”
“Nimesimama kati ya baba na mama yangu wote nawapenda na sitaki kumuudhi mmoja kati yao.”
“Sasa mwanangu kuna kitu nimekuitia, mdogo wako Suzana anakupenda sana tena sana kapitiliza kukupenda. Siku zote amekuwa akikuonesha kwa vitendo imeonekana kama umuelewi. Mpaka kuja kunieleza mimi mama yake basi ujue yamemfika shingoni. Kutokana na tabia yako ambayo imekuwa tofauti na wavulana wengi nimeamini unafaa kuwa mkwe wangu.
“Nakuomba uwe mkwe wangu muoe Suzy kwa kweli ni mwanamke mzuri ambaye atajivunia katika maisha yako. Najua utashtuka mama kumpigia debe mwanaye lakini kwa hili sikuwa na jinsi.”
“Nimekusikia mzazi wangu naomba unipe muda ili nami niwasiliane na wazazi wangu.”
“Kuwasiliana na wazazi wako si vibaya, lakini kwanza ni wewe kukubaliana na mwenzako.”
“Mimi nimekubali.”
“Nashukuru kwa majibu yako mazuri, basi nakuruhusu, uwasiliane na wazazi wako, usihofu gharama nitakusimamiane mpaka mwisho wa harusi yenu.”
“Nashukuru mzazi wangu.”
Baada ya kutoka kwa mama mwenye nyumba nilirudi chumbani kujipumzisha, haikupita muda mlango iligongwa alikuwa Suzy.
“Karibu,” nilikabiribisha bila kunyanyuka kitandani.
Alisukuma mlango na kuingia ndani akiwa na sinia lililofunikwa kawa.
“Karibu chakula Kazala.”
Sikutaka kubisha lakini nilitaka tule pamoja Suzy hakukataa tulikuwa pamoja. Tokea siku ule Suzy akawa na uhuru wa kuja kwangu lakini sikuwa na tamaa ya mwili kwa kujiapia mpaka nimuoe kabisa. Mipango ilienda vizuri na Suzy akawa mke wangu ndoa ilifungwa kwa mkuu wa wilaya kila mtu akiwa na imani yake.
Namshukuru Mungu maisha yalikuwa mazuri kwa mke wangu kuonesha mapenzi ya kweli nami pia nilimpenda mapenzi ya dhati. Miezi sita baada ya kuoana tulihama nyumba ya wazazi wa mke wangu na kwenda kukaa kwenye nyumba nyingine ya familia yao iliyokuwepo umbali kidogo toka kwetu, wakati huo mke wangu alikuwa na ujauzito wa miezi minne.
Nyumba tuliyohamia ilikuwa na wapangaji wawili na sisi tulikuwa sehemu ya nyumba mbele iliyokuwa ya kifamilia. Kazi nayo iliendelea vizuri kila siku kuondoka asubuhi na kurudi usiku. Maisha yalisoga muda ulipofika mke wangu alijifungua mtoto wa kike.
Mwenetu alikuwa vizuri mpaka alipofikisha mwaka mmoja na miezi saba nilipatwa na mshtuko kushindwa kutembeza zaidi ya kukaa na kujibuta kwa matako. Katika maisha yangu pamoja ya kutokuwa na dini bado sikuuamini uchawi hata kidogo japo niliusikia kuwa upo. Hali ya mwanangu ya kutotembea ilinishtua sana. Katika kuulizia kwa watu waliomuona mtoto wangu walisema mtoto wangu inawezekana amebemendwa.
Kauli ile ilinishtua sana baada ya kuelezwa maana ya kubemenda ni mtu kutoka nje ya ndoa, kwa upande wangu sikuwa na shaka kwa vile sikuwa na mpenzi mwingine zaidi ya mke wangu mama Zawadi. Pia kwa upande wa mke wangu hata kwa mtutu nisingekubali kutoka nje ya ndoa kwani nilimuamini sana.


MY WIFE....EP.3.


LIPOISHIA:Kauli ile ilinishtua sana baada ya kuelezwa maana ya kubemenda ni mtu kutoka nje ya ndoa, kwa upande wangu sikuwa na shaka kwa vile sikuwa na mpenzi mwingine zaidi ya mke wangu mama Zawadi. Pia kwa upande wa mke wangu hata kwa mtutu nisingekubali kutoka nje ya ndoa kwani nilimuamini sana.
SASA ENDELEA...

Nikawa njia panda kuelewa hali iliyomkuta mwanangu kama inatokana na mtu kutoka nje ya ndoa basi walikuwa wamekosea nikiamini huenda tatizo alilonalo mwanangu huenda linafanana na hilo.

Jumapili moja niliyokuwa nyumbani, nilitoka na mwanangu ambaye nilimpenda sana pamoja na kuchelewa kutembea. Nikiwa natoka dukani nilikutana na mama mmoja wa makamo na kusalimiana naye. Nilipishana naye lakini sikupiga hatua mbili aliniita.
“Baba Zawadi.”
“Naam mama,” niliitika huku nikigeuka kumsikiliza.
“Samahani mwanangu.”
“Bila samahani mama.”
“Basi naomba tusogee pembeni tuzungumze.”
“Hakuna tatizo mama yangu.”
Nilisogea pembeni kidogo ya barabara na kusimama kwenye uchochoro wa kutokea mtaa wa pili.
“Naam mama,” nilianzisha mazungumzo.
“Mwanangu nimekuita ili tuzungumze kitu kimoja, nina imani hukijui kinachofanyika nyuma kwa vile unatoka asubuhi na kurudi usiku kinachotendeka mchana hukijui.”
“Ni kweli mama.”
“Unamuonaje mjukuu wangu Zawadi?”
“Kwa kweli mama hata mimi nashindwa kuelewa.”
“Unashindwa kuelewa nini ikiwa mwanao mnamtesa bila kosa.”
“Mama tunamtesa kivipi?”
“Unaona hii miguu ya mwanao ipo sawa?” aliniuliza huku akiishika miguu ya mwanangu iliyokuwa haina nguvu.
“Haipo sawa, kwa kweli nachanganyikiwa hata sijui sababu ni nini japo watu wananiambia kitu ambacho naamini si kweli.”
“Kitu gani hicho?”
“Achana nacho hakina umuhimu,” sikutaka kumuambia habari ambazo mimi niliona ni za kizushi.
“Kitu gani?”
“Utayaweza maneno ya watu mama, kila kukicha hawakosi ya kusema.”
“Maneno gani?” yule mama alikazania swali lake.
“Achana nayo hayana umuhimu.”
“Inawezekana uliyoambiwa ndiyo nitakayokueleza leo.”
“Nina imani si hayo.”
“Haya, tuachane na hayo, unajua matatizo ya mtoto kuchelewa kutembea yanatokana na nini?”
“Kwa kweli sijui.”
“Yapo mambo mengi, moja kuchezewa na walimwengu na lingine ni kubemendwa.”
“Kwa hiyo tatizo la mwanangu linatokana na nini?”
“Mkeo atamuua mtoto huyu, kwa nini unakuwa na moyo wa kikatili kiasi hiki, kama hawezi kumlea basi mumpeleke kwa bibi yake kuliko kumtesa bila sababu.”
“Mama sijakuelewa, mke wangu amemfanya nini mtoto?”
“Anambemenda.”
“Eti?”
“Anambembenda na mwisho wake atamuua.”
“Mmh! Una maana gani?”
“Mkeo si muaminifu, wote mtaani wanajua, ukitoka na yeye nyuma anatoka anarudi muda umekaribia kurudi.”
“Sasa mama kutoka kwa mke wangu inaingiliana vipi na mwanangu kuchelewa kutembea?”
“Baba jasho la janaba ni baya kwa mtoto hasa ikiwa mliyekutana si wazazi wa mtoto, mmoja wenu akikosa uaminifu na akamshika na uchafu wake lazima mtoto atadhurika.”
“Sasa mama mke wangu mbona muaminifu?” kauli ile ilinishtua.
“Baba acha kusema hivyo, sisi ndiyo tunayejua, isingekuwa huyu mtoto wala nisingenyanyua mdomo wangu, ningekuacha ili siku moja ujionee mwenyewe uchafu wa mkeo.”
“Kwa hiyo chanzo cha matatizo ya mtoto ni mke wangu?” nilijikuta nikikosa amani moyoni.
“Baba usiandikie mate, kwa vile mkeo hata aibu hana, siku moja rudi nyumbani mchana utajionea mwenyewe. Kabla ya kufanya lolote fanyia kazi haya niliyokueleza. Ukipata majibu ndiyo utajua mkeo muaminifu au siyo, utapata kiini cha matatizo ya mkeo.
“Ila nakuomba kabla ya yote mtoto wako mpeleke kwa bibi yake kisha fanya uchunguzi wako.”
“Asante mama kwa maelezo yako.”
“Ila nakuomba ukienda kwako usioneshe mabadiliko yoyote, kuanzia Jumatatu siku yoyote rudi nyumbani ghafla mchana utaniambia niliyokueleza ni kweli na maendeleo ya mwanao utayaona kwa muda mfupi akiwa mbali na mama yake.”
“Asante mama.”
Niliagana na yule mama ambaye alikuwa mtu wa heshima na nilimuheshimu sana pale mtaani. Nikiwa narudi, njia nzima nilikuwa na mawazo mazito juu ya maneno niliyoelezwa na sababu ya matatizo yanayomfanya mwanangu ashindwe kutembea.
Kingine ambacho sikutaka kukikubali mara moja ni kuhusu kutoka kwa mke wangu nje ya ndoa. Kwa kweli sikuamini mke wangu kama angeweza kutoka nje ya ndoa hasa kutokana na ukimya pia kuonesha mapenzi mazito kwangu.



MY WIFE....EP.4.

ILIPOISHIA;

Kingine ambacho sikutaka kukikubali mara moja ni kuambiwa kuwa mke wangu huwa anatoka nje ya ndoa.
Kwa kweli sikuamini kama mke wangu angeweza kufanya hivyo, kutokana na ukimya wake na jinsi anavyoonesha mapenzi mazito kwangu.
SASA ENDELEA...

Nilifikiria kama ni kweli mke wangu ndiye chanzo cha matatizo ya mtoto, ina maana hajui au anafanya makusudi. Nilipofika nyumbani nilijitahidi kuficha mabadiliko mke wangu alinichangamkia huku akimchukua mtoto ambaye siku zote alimuonesha mapenzi makubwa.
Siku hiyo nilikuwa nyumbani kimwili lakini kiakili nilikuwa mbali sana, kwa kuwa nilikuwa nikiwaza yote niliyoelezwa na wote walioguswa na hali ya mwanangu kuchelewa kutembea kiasi cha watu kumtania kwa kumwita fundi majiko.
Japokuwa mwanangu alikuwa hatembei lakini alikuwa akiongea maneno yote akiwa amekaa kama fundi anayetengeneza majiko.
Kila nilipomuangalia mke wangu sikummaliza, nilivyomuamini na maneno yale nilichanganyikiwa huku upande mwingine nikiona kama maneno yale yalikuwa ni njama za kutaka kuivunja ndoa yangu.
Mke wangu alikuwa mpole na wala hakuwa muongeaji kabisa, muda wote alikuwa kimya mpaka miye nianze kumsemesha.
Niliificha siri ile moyoni mwangu japokuwa kuna wakati moyo ulikubali na wakati mwingine ulikataa kuamini kile kilichokuwa kikisemwa.
Siku ya pili ilikuwani ni Jumatatu nilitakiwa kwenda kazini nilipanga kurudi mchana ili nishuhudie kile kinachosemwa kama ni kweli au la.
Siku ya siku nilipofika kazini, nilisingizia kuumwa kwa vile sikuwahi kuomba ruhusa kutokana matatizo yoyote nilikubaliwa na kurudi nyumbani saa sita kasorobo mchana.
Nilipofika nilikuta mlango ukiwa umefungwa, nilipiga simu ya mke wangu lakini haikuwa hewani. Nilizunguka upande wa pili nilimkuta mtoto wangu Zawadi akichezea matope bila kuwa na mtu yeyote wa kumwangalia.
Nilibisha hodi chumba cha jirani, alitoka jirani yangu ilhali akiwa amepatwa na mshtuko mkubwa sana kwa kuniona muda ule.
“Ha! Shemeji leo umerudi mchana?” alisema huku akimtoa Zawadi kwenye matope na dalili zote zikionesha kwamba kwa kipindi cha mchana, mtoto yule huwa anaachwa peke yake na tayari alikwisha kula kiasi kikubwa cha matope kutokana na mdomo ulivyoonesha.
“Sijisikii vizuri,” nilimjibu kwa sauti ya chini huku roho ikiniuma kwa malezi mabaya aliyokuwa akipewa mwanangu.
Hali ile ilianza kunipa picha ya maneno niliyoelezwa, jirani yangu mama Sonono alianza kumsafisha matope kisha aliingia ndani kwake na kutoka na ufunguo na kunipa huku akisema:
“Shem naomba unitolee na nguo za Zawadi.”
“Hakuna tatizo.”
Niliingia ndani huku nikijiuliza mke wangu atakuwa amekwenda wapi, pia kama nisingekuja mwanangu angekula matope na kuwa mchafu mpaka saa ngapi. Baada ya kumtolea nguo nilimuuliza:
“Mama Zawadi ameenda wapi?”
“Amesema ameitwa na mama yake.”
“Kila siku huwa anaitwa na mama yake?” Nilimshtukiza kwa swali ambalo nilijua hakulitegemea.
“Siku nyingine huwa sijui anaenda wapi.”
“Kwa hiyo akiondoka wewe ndiye unakuwa mlezi wake au siyo?”
“Kwani vipi shem?”
“Nakuuliza wewe ndiye mlezi wake, hebu angalia nimemkuta mtoto anakula matope, kwa siku zote anazoondoka kazi yako ni kumlisha mwanangu matope?” Nilimuuliza kwa hasira.
“Ha...ha...pana shem.”
“Niambie ukweli mke wangu amekwenda wapi maana nimetoka kwao?”
“Si...si...jui akiondoka huniachia mtoto.”
“Huwa anarudi saa ngapi?”
“Jioni kabla hujarudi.”
“Asante.”
Nilimchukua mwanangu na kumpeleka kwa mama mzazi wa mke wangu na kumuuliza kama mke wangu alifika pale nyumbani kwake.
Majibu yalikuwa ni tofauti na nilivyoelezwa, nilimuomba nimuachie mtoto. Alikubali kitu cha ajabu hakuniuliza swali lolote zaidi ya kumchukua mtoto.
Nilirudi nyumbani kumsubiri mke wangu aniambie alikokuwa amekwenda.



MY WIFE....EP.5.

ILIPOISHIA;
NILIMCHUKUA mwanangu na kumpeleka kwa mama mzazi wa mke wangu na kumuuliza kama mke wangu alifika kwake.
Alijibu kuwa hajamuona, nilimuomba nimuachie mtoto. Alikubali kitu cha ajabu hakuniuliza swali lolote zaidi ya kumchukua mtoto. Nilirudi nyumbani kumsubiri mke wangu aniambie alikwenda wapi.
SASA ENDELEA...
Majira ya saa kumi na mbili na nusu mke wangu alirudishwa na gari, kwa vile nilishaelezwa muda wake wa kurudi, nilitoka na kukaa nje, ufunguo nilimpatia mama Sonono na kumwambia akija amwambie kuwa mtoto amechukuliwa na mama yake mzazi.
Alipofika aliteremka na kukimbilia kwa mama Sonono kuulizia ufunguo.
Baada ya muda nilimuona akitoka barabarani akiwa kama anayetafuta kitu, huku akiwa anapiga simu, baada ya muda gari lililomleta lilirudi.
Kabla hajapanda kwenye gari nilijitokeza na kumwita.
“Mke wangu.”
Alishtuka kuniona mpaka simu ikamponyoka chini huku akisema kwa sauti kubwa:
“Ha! Mume wangu!”
“Vipi mpenzi ingia twende nina safari nyingine,” sauti kutoka ndani ya gari ilimhimiza aingie kwenye gari.
“John nenda tu, mume wangu.”
“Mumeo kafanya nini tena mpenzi?”
“John ondoka mume wangu huyu hapa.”
“He!” Sauti ilitoka kwenye gari na gari kuondoka kwa kasi bila kufunga mlango mmoja. Sikutaka kutaharuki nilimuuliza:
“Unatoka wapi?”
“Kwa mama.”
“Yule nani?”
“Bwana wa shoga yangu alinipa lifti.”
“Mmh! Sawa.”
“Vipi mbona mapema?”
“Kawaida tu kwani kuna ubaya?”
“Hakuna, Samahani mume wangu, nilikwenda kwa mama na kupishana naye huku nyuma alikuja na kumchukua Zawadi, nilikuwa naomba nimfuate.”
“Sawa, hakuna tatizo, utanikuta.”
Alisogea mbele na kukodi teksi iliyompeleka kwao, niliingia ndani nikiwa nimefura kwa hasira nikiwa siamini nilichokiona na kuanza kuamini yote niliyoelezwa juu ya uchafu wa mke wangu.
Nilimsubiri kwa hamu kubwa arudi anieleze sababu ya kujifanya kondoo mwenye ngozi ya chui.
Kitu cha ajabu mezani kulikuwa kumeandaliwa kila kitu kuonesha kwamba mke wangu kabla ya kuondoka hufanya kila kitu kwa ajili ya chakula cha jioni ili akirudi hata kama amechelewa chakula kionekane kuwa ni tayari.
Miye nilipokuwa narudi niliamini kuwa mke wangu hakutoka kwa vile chakula kilikuwa kimeshatayarishwa.
Nilikwenda hadi chumbani na kujilaza kitandani miguu ikiwa chini bila ya kuvua viatu, niliweka mikono kichwani huku macho yangu yakitazama juu nisiamini nilichokisikia, hata nilichokiona kwa macho yangu.
Nilipatwa na mtikisiko wa moyo kwa mara ya kwanza tangu niwe na akili timamu japokuwa niliishawahi kuona na kusikia usaliti ndani ya ndoa za watu.
Nikiwa katikati ya mawazo mke wangu alirudi akiwa na mtoto na moja kwa moja alikuja kukaa pembeni yangu huku akijichekesha.
Nilijiuliza mama yake amemwambia nini kutokana na kuwa katika hali ya kawaida tu.
“Vipi mume wangu?”
“Poa.”
“Mbona kama haupo sawa?”
“Nipo sawa,” nilimjibu kwa sauti ya chini.
“Hapana mume wangu lazima utakuwa na tatizo.”
“Nipo sawa.”
“Nakuja,” mke wangu alisema huku akinyanyuka na kwenda nje akimuacha mtoto pembeni.
“Baba,” mwanangu Zawadi aliniita.
“Mama,” nilipenda kumwita hivyo kwa kuwa alikuwa akitumia jina la mama yangu mzazi.
“Pipi api?”
“Nitakwenda kukununulia.”
“Tende dukani baba kanunue pipi,” mwanangu alisema huku akijivuta kwangu na kunishika mkono, niliamua kumpelekea dukani.
Nilimuangalia mwanangu na kujikuta nikitokwa na machozi ya uchungu, alizidi kunilazimisha ninyanyuke. Nilinyanyuka kitandani na kumbeba mpaka dukani ambako nilimnunulia pipi na biskuti.
Wakati napita kurudi ndani nilimsikia mke wangu akizungumza na mama Sonono. Kwa jinsi walivyokuwa wakizunguza niliamini kabisa alijua bado nilikuwa chumbani.
“Dada umeniangushia jumba bovu,” nilisikia sauti ya mama Sonono ikilalamika.
“Jumba bovu vipi, kwani anajua nilikwenda wapi?”
“Kurudi kwa mumeo kuna sababu, hata maswali yake yalionesha anajua mengi juu yako, hata mtoto kwa mama yako alimpeleka yeye.”
“Wewee usiniambie!” sauti ya mke wangu ilionesha kushtuka.
“Kweli, kabisa ila alinikataza nisikuambie.”
“Jamani kwa nini umenigeuka?”
“Sikuwa na jinsi nilihofia kupigwa na mumeo kwa jinsi alivyokuwa angeweza kumtafuna hata mtu.”
“Akupige kwani wewe ndiye uliyetoka nje ya ndoa, wa kupigwa ni miye, kwanza jeuri hiyo ataitoa wapi?” mke wangu alizungumza kwa sauti ya kujiamini.
Maneno yale yalionesha dhahiri kwamba mke wangu alifanya yote yale kwa vile alikuwa na kitu alichokuwa akikitegemea.
“Dada ukitoka tena uondoke na mwanao sitaki ugomvi na mumeo, kwani ataona labda mimi ndiye ninayekufanyia mipango.”



MY WIFE....EP.6.


LIPOISHIA;

“Akupige kwani wewe ndiye uliyetoka nje ya ndoa, wa kunipiga ni mimi, kwanza jeuri hiyo aitoe wapi?” Mke wangu alizungumza kwa sauti ya kujiamini.
Maneno yake yalionesha kabisa kuwa mke wangu alikuwa akifanya mambo yake huku akijua kuwa kulikuwa na kitu anachokitegemea.
“Dada ukitoka tena uondoke na mwanao sitaki ugomvi na mumeo na ambaye anaweza kuona labda miye ndiye ninayekufanyia mipango.”
SASA ENDELEA...

“Mi mtoto mdogo? Nitaondoka naye kwani kazi anafanya yeye? nitamuweka kwenye kochi kisha namaliza haja zangu, hilo shoga lisikupe shaka, basi baadaye.”
Kwa vile ilikuwa giza mke wangu alitupita mimi na mwanangu bila ya kutuona na kuingia ndani.
Nami niliingia ndani na kukutana naye mlangoni, aliponiona aliniuliza:
“Vipi umetoka wapi?”
“Dukani.”
“Eti, kwani mume wangu leo umerudi saa ngapi?”
“Kwani vipi?”
“Nasikia umerudi mapema?”
“Tatizo ni nini?”
“Sasa umerudi mapema ili iweje?”
“Sina ruhusa ya kurudi nyumbani kwangu mapema?”
“Siyo hivyo.”
“Sasa tatizo nini?”
“Ujaji wako umeonekana umekuja kwa sababu.”
“Ndiyo umekuja kwa sababu maalum.”
“Sababu gani?”
Nilijikuta nikipata nafasi ya kufungua yaliyo moyoni mwangu.
“Niambie ulikwenda wapi?”
“Kutembea.”
“Kwa ruhusa ya nani?”
“Nilisahau kukuaga naomba unisamehe kwa hilo.”
“Aliyekurudisha ni nani?”
“Ni rafiki wa shoga yangu.”
“Naomba uniambie ukweli la sivyo leo nitakufanyia kitu kibaya sana,” nilimtisha.
“Unataka kunifanyia kitu gani?” alishtuka.
“Usiponieleza ukweli nitakufanyia kitu kibaya ambacho hutakisahau maisha mwako.”
“Unataka ukweli gani mume wangu?” mke wangu aliingia woga.
“Ninajua kila siku nitokapo nawe huku nyuma unatoka, huwa unakwenda wapi?”
“Nani kakuambia?”
“Si kujua aliyeniambia, bali ni wewe kunieleza ninapotoka nawe unatoka, unakwenda wapi?”
“Waongo hao mi sijawahi kutoka, ni leo tu.”
“Mama Zawadi naomba uniambie ukweli,” nilipandisha sauti.
“Nilikwenda kwa shoga yangu na wakati wa kurudi mpenzi wake alinipa lifti kwenye gari lake.”
“Huyu mtoto kakukosea nini?”
“Kwa vipi?”
“Mbona unamfanya kama yatima, kama unafanya uchafu wako basi mhurumie mtoto, unaridhika na hali ya mtoto ya kuteseka hivi?”
“Nimemtesa kivipi?” majibu ya mke wangu hayakuonesha kushtushwa na hali ya mtoto wetu.
“Kila ukiondoka unamwacha kwa mama Sonono mtoto hana matunzo, leo tu nimemkuta akila matope, kwani nini umekuwa mkatili kiasi hiki mke wangu?”
“Mume wangu mtoto kuchezea matope ni kitu cha kawaida tu.”
“Uchafu unaoufanya umesababisha mtoto aendelee kuteseka chini kama fundi majiko, au unataka azeeke akiwa amekaa?”
“Mwanao mvivu tu wala si mimi.”
“Taarifa zako za kumharibu mtoto kila mtu mtaani anazijua, wanamuonea huruma mtoto, ona miguu ilivyolegea kwa umalaya wako.”
“Sawa mimi malaya, basi nipe talaka yangu.”
“Tatizo si talaka bali kumuonea huruma mtoto.”
“Mi si malaya naomba talaka yangu.”
“Hapa talaka haitoki kuanzia leo mtoto atakaa kwa mama na siku nirudi halafu nisikukute utanitambua.”
Kwa kweli mke wangu nilikuwa nampenda sana, sikumfanya lolote tulilimaliza kwa kuniomba msamaha kwa kuondoka bila kuaga lakini suala ya kutoka nje ya ndoa alilipinga kwa nguvu zote huku akiniuliza:
“Lini tulipokutana kimwili ulikuta nimetumika? Mara nyingi mimi ndiye ninayekulazimisha kufanya mapenzi kama ningekuwa si mwaminifu kulikuwa na haja gani ya kulazimisha mapenzi kwako?”
Kwa kweli sikuwa na jibu, kwa upande mwingine nilimuona kama mke wangu yupo sawa kutokana na tangu nimuoe hakuwahi kutoa udhuru kitandani. Tena kwa upande mwingine nilikuwa namuonea huruma kutokana na kazi zangu ambazo hunilazimu kurudi nikiwa nimechoka. Suala la mtoto kumpeleka kwa bibi yake alikubaliana nalo.
***
Maisha yaliendelea huku nikiamini kabisa kuwa mke wangu amejirekebisha, alipokuwa akitaka kutoka nyumbani alikuwa lazima aage ndipo atoke.



MY WIFE....EP.7


ILIPOISHIA:

Nilipotoka kazini nilikwenda sehemu aliyonielekeza na kushtuka kukuta amepanga kwenye nyumba ya gharama iliyokuwa ndani ya fensi, kitu kilichonipa wasiwasi na kujiuliza kama kodi aliyolipa mke wangu ikiisha nitaweza kuilipa. Mke wangu alinipokea kwa furaha.
SASA ENDELEA...

“Karibu mume wangu kwenye makazi mapya.”
“Asante.”
“Mbona kama unashangaa?”
“Nashangaa kwa mambo mawili, kwanza nyumba nzuri sana na pili na wasiwasi kodi yake ni kubwa.”
“Ni kweli kodi ni kubwa lakini ni sehemu nzuri tutakayoishi bila bughuza za watu.”
“Nyumba yote kwa mwezi shilingi ngapi?”
“Laki moja na nusu.”
“Mke wangu laki moja na nusu kwa mwezi umelipa kwa muda gani?”
“Mwaka mzima.”
“Ndiyo shilingi ngapi?”
“Hesabu unajua, zidisha laki na nusu mara kumi na mbili.”
“Sasa mimi nitaweza kulipa fedha zote hizo?”
“Nitakusaidia, kuwa na amani moyoni mwako.”
Sikutaka kuhoji sana fedha zote hizo kazipata wapi, kwani Waswahili wana msemo wao kuwa ukimchunguza sana bata huwezi kumla na ukimchunguza sana mkeo hutaweza kuishi naye. Tuliyaanza maisha ya Uzunguni, sehemu waliyokuwa wakiishi watu wenye uwezo. Kwa kweli maisha ya makazi mapya yalikuwa mazuri sana yenye furaha na amani.
Kwa muda mfupi, afya yangu ilirudi katika hali ya kawaida baada ya kuteseka kwa muda mrefu kutokana na vituko vya mke wangu. Kutokana na kuonesha mke wangu amejirekebisha tulimchukua mtoto wetu na kuishi naye. Heshima aliyoonesha ilimshtua hata mama yake mzazi.
Maisha yalisonga mbele, mke wangu akashika ujauzito wa pili, kitu kilichozidi kunipa faraja moyoni mwangu. Lakini ilikuwa tofauti kwa upande wa pili, mke wangu hakupenda kubeba ujauzito kwa vile mtoto wetu alikuwa bado mdogo.
“Mke wangu tatizo nini?”
“Huoni Zawadi bado mdogo.”
“Miaka mitatu si michache na mpaka unajifungua atakuwa amesogea sana.”
“Kwa upande wangu nilipanga kuzaa baada ya Zawadi kufikisha miaka mitano.”
“Basi bahati mbaya, itabidi uzae hivyohivyo.”
“Siwezi, lazima niitoe hii mimba.”
“Usiitoe mke wangu, Zawadi tutampeleka kwa bibi yake ili asipate shida.”
“Bado nina hamu ya kumlea mwanangu, kama mtoto utapata tu muda ukifika,” mke wangu bado alishikilia msimamo wake.
“Nakuomba usiitoe hiyo mimba, nipo chini ya miguu yako mke wangu,” nilimbembeleza mke wangu mpaka nikampigia magoti.
“Kwa hilo siwezi kukusikiliza, sihitaji senti tano yako, nitatoa kwa fedha zangu.”
Kwa mara nyingine mke wangu alinizidi nguvu, nikamkubalia kwa shingo upande. Siku ya pili nikiwa kazini, majira ya saa tisa alasiri, mke wangu alinipigia simu kunijulisha kuwa amefanikiwa kuitoa mimba salama. Nilimkubalia lakini upande wa pili moyo uliniuma sana, hata kazi ilinishinda na kwenda sehemu ya peke yangu ambapo nililia sana kumpoteza mwanangu mtarajiwa.
Jioni niliporudi, nilimkuta mke wangu nyumbani, hali yangu ya unyonge ilimshtua mke wangu na kunifuata nilipokuwa nimekaa, akawa ananibembeleza.
“Mume wangu, najua kiasi gani nilivyokuumiza lakini sikuwa na jinsi, nilifanya vile kwa maana kubwa. Kwa sasa ni vigumu kunielewa lakini amini nilichokifanya si kukukomoa bali kumpa nafasi Zawadi. Kumbuka makosa yangu ya awali yalimtesa mwanangu hivyo sasa hivi nina deni la kumlea.”
Kutokana na kumpenda sana mke wangu, nilikubaliana naye. Maisha yalisonga huku akionesha mapenzi mazito kwangu, kitu kilichofuta mawazo ya kutoa ujauzito.
Siku zote kimya kingi kina mshindo mkuu. Mwezi mmoja baada ya kutoa ujauzito, asubuhi moja nilidamka kwenda kazini huku hali yangu kiafya ikiwa si nzuri.
Nilijitahidi kwa kuamini mwanaume si mtu wa kujilegeza. Nilipofika kazini, nilijitahidi kufanya kazi lakini kutokana na kufanya kazi juani, hali yangu ilibadilika na kuwa mbaya hivyo niliruhusiwa kwenda hospitali kupata matibabu.
Nilikwenda hadi hospitali ya wilaya na kupata huduma japo dawa nilikwenda kununua duka la kuuza dawa. Nilibeba dawa zangu na kurudi nyumbani kupumzika. Nilipofika nyumbani, ndani ya geti nilikuta kuna gari ambalo kwangu halikuwa geni sana japo sikukumbuka nililiona wapi.
Baada ya kutafakari, niligundua lile gari ndilo lililomshusha mke wangu, nikashtuka kulikuta nyumbani kwangu na kujiuliza limefuata nini pale. Niliingia ndani na kukuta sebuleni kuna pombe kali juu ya meza na glasi mbili.
Sikujishughulisha navyo, nilielekea chumbani, nilipofika kwenye mlango wa chumbani, nilikuta umefungwa kwa ndani, nikasikia sauti mbili ya mwanamke na mwanaume. Sauti ya mwanamke ilikuwa ya mke wangu ya kiume sikujua ni ya nani. Kwa haraka nilitoka mpaka nje na kuzunguka dirishani na kuchungulia ndani.




MY WIFE....EP.8.


ILIPOISHIA;

MLANGO nilirudisha na kuzima taa ya sebuleni na kukaa kwenye kochi ili kumsubiri mke wangu ambaye sikujua atarudi muda gani.
Mpaka muda ule ilikuwa ni saa saba na nusu za usiku.
SASA ENDELEA...

Nilijitahidi kukaa macho ili mke wangu akirudi na kugonga, niweze kumuona. Kuna kipindi nilipitiwa na usingizi niliposhtuka nilitoka mpaka nje kuangalia kama labda nitamuona mke wangu akiwa amerudi na kuniita na kushindwa kumsikia.
Nilizunguka nyumba nzima bila kumuona mke wangu na kurudi tena sebuleni kumsubiri.
Siku ya pili ilinikuta nikiwa bado nipo sebuleni nikimsubiri mke wangu, nikiwa najiandaa kwenda chumbani, mke wangu aliingia akionesha amekunywa pombe kitu ambacho hakuwahi kukifanya katika maisha yake yote niliyomjua na nywele zake zilikuwa timtim.
“Ooh! Mume wangu, habari za asubuhi?”
“Nzuri, habari za wapi?”
“Nilikwenda kwa mama wakati narudi shoga yangu alinipigia simu kuwa kuna harusi ya ndugu yake. Nilijua nitawahi kurudi kumbe sherehe ni sherehe kuja kushtuka muda umekwenda na usafiri ulikuwa wa tabu nikaamua kulala huko huko.”
“Kwa nini hukunipigia simu?”
“Wakati unanipigia simu ilizimika hata kabla sijakujulisha.”
“Na mbona umekunywa pombe, umeanza lini?”
“Mume wangu sherehe ina vishawishi vingi, lakini sikunywa sana.”
Nilijikuta kwa mara nyingine nikishindwa kumhukumu mke wangu, niliamua kumsamehe kwa vile nilikuwa nampenda sana. Ila nilimuomba asiondoke nyumbani bila kuaga pia asiwe anakunywa pombe.
Mke wangu kama kawaida yake aliniomba msamaha na kuniahidi kuwa hataweza kuondoka bila ya kuaga, pia hatarudia tena kunywa pombe.
Nilimsamehe mke wangu kwa vile nilikuwa nampenda sana na sikutaka kumpoteza maishani mwangu kwa kuamini kuwa yeye ni kila kitu kwangu.
Baada ya tukio lile mke wangu alitulia na heshima ya ndoa ikarudi ndani kama kawaida.
Wakati huo mtoto wetu alikuwa amekazana kutembea, kwa kitendo cha mwanangu kutembea niliwashukuru sana majirani. Wiki moja baada ya tukio la mke wangu kulala nje aliniomba tuhame mtaa ule.
“Mume wangu naomba tuhame hapa.”
“Tuhame hapa twende wapi?”
“Sehemu yoyote lakini mbali na hapa.”
“Kodi si itatusumbua?” Nilimwambia kwa kuwa hali yangu ya kiuchumi aliijua.
“Mume wangu unafanya kazi, acha kujilegeza, inatakiwa sasa hivi tuishi maisha ya kwetu wenyewe bila kuwategemea watu,” yalikuwa maneno ya kweli lakini yalitakiwa maandalizi ya muda mrefu hasa nikizingatia kulipa kodi ya miezi sita kwa haraka ulikuwa mtihani mkubwa kwangu.
“Lakini mbona mama alisema hii ni nyumba yako amekupa baada ya kuoana?” Ilibidi nihoji baada ya mke wangu kulazimisha kuhama.
“Kazala, husikii tunavyosimangwa kuhusu hii nyumba, hasa wewe mume wangu maneno yao kwa kweli huwa yananiumiza sana pale wanapokusema vibaya eti nimekuoa badala ya kunioa, hayo ni maneno gani mume wangu?”
“Mmh! Sina jinsi kwa vile ni haraka sana, nipe wiki nijaribu kukopa kazini ili tutafute nyumba.”
“Kuhusu kodi ya kuanzia nitalipa mimi itakayofuata utalipa wewe.”
“Hakuna tatizo,” nilikubaliana naye bila kuhoji fedha ataitoa wapi kwa kuhofia kubadili uamuzi wake.
Siku ya pili nilipokwenda kazini mke wangu alinipigia simu na kunijulisha kuwa amekwisha hamisha kila kitu na kunielekeza nikitoka kazini niende sehemu alipo na siyo pale tena.
Nilipotoka kazini nilikwenda sehemu aliyonielekeza na kushtuka kukuta amepanga kwenye nyumba ya gharama iliyokuwa imo kwenye uzio, kitu kilichonipa wasiwasi na kujiuliza kama kodi aliyolipa mke wangu ikiisha nitaweza kulipa.