Friday, November 27, 2015

DAVID MUSA AFARIKI DUNIA


MWANAMUZIKI mwanzilishi wa kundi la Safari Trippers na aliyekuwa mwalimu wa wanamuziki wengi sana David Musa amefariki usiku wa kuamkia leo. Msiba uko nyumbani kwake Chang'ombe. Habari zaidi tutazileta kadri tutakavyozipata. 
safari trippers
Kushoto mwenye miwani David Musa, wa tatu Marijani Rajabu na kulia mwisho Jumanne Uvuruge mtunzi wa wimbo wa Georgina.
 Mungu amlaze pema

Monday, November 23, 2015

MFAHAMU MBARAKA YUSUPH MWANAMUZIKI WA NATIONAL PANASONIC NA POWER IRANDA

“NIMEACHANA na muziki wa dansi hivi sasa na nimeamua kugeukia sanaa ya filamu, ambapo sababu kubwa ni kupungua kwa kasi yangu ya ucharazaji gitaa, kutokana na kupata mara mbili kwa nyakati tofauti, ugonjwa wa kupooza.”
Hayo ni maneno ya Mbaraka Yusuph, kati ya wacharazaji mahiri wa zamani wa magitaa yote pamoja na Saxophone, aliyewahi kuzitumikia bendi mbalimbali hapa nchini, zikiwamo, The Smashers, National Panasonic, OSS ‘Power Iranda’, Seven Blind Beats na the Big Africa ya Arusha..ENDELEA HUKU

Monday, November 9, 2015

MWANAMUZIKI MKONGWE CAPT JOHN SIMON AFARIKI DUNIA


IMG_9699
 Capt John Simon
 MWANAMUZIKI mkongwe ambaye kwa siku za karibuni alikuwa kwenye bendi ya Shikamoo Jazz, Capt John Simon, amefariki dunia leo katika hospitali ya Muhimbili. Mzee huyu alikuwa mmoja ya waanzilishi wa NUTA Jazz band, na baadae kadri ya maelezo yake mwenyewe, Mheshimiwa Rashid Kawawa, ndie alimtoa NUTA Jazz na wanamuziki wengine na kwenda kuanzisha JKT Jazz Band, iliyopata umaarufu kama Kimbunga Stereo. 
FIL6
Waimbaji wa NUTA Jazz Band, toka kulia John Simon, Muhidin Gurumo, na kushoto Ally Akida
  Mzee John Simon pia alikuwa mwanzilishi wa Shikamoo Jazz Band, bendi ambayo ameitumikia mpaka siku zake za mwisho. Capt John Simon pia alikuwa makamu mwenyekiti wa CHAMUDATA mwishoni mwa miaka ya 90, akiwa makamu wa John Kitime, na hatimae kuwa mwenyekiti baada ya John kitime kujiuzuru nafasi yake. Taratibu za mazishi zitapatikana baada ya ndugu kukutana. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga.

Wednesday, October 14, 2015

MWANAMUZIKI ENZI ZA MWALIMU PART 1


1358232950030_1358232950030_rLEO ni miaka 16 toka Kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mungu amlaze pema Mwalimu. Vyombo vya habari vinaeleza mengi kuhusu hali ya maisha ilivyokuwa zama za Enzi ya Nyerere, kwa tuliekuweko enzi hizo tunaona mengi yanayosemwa ni ya kweli na mengi si sahihi, mengine yanatungwa ili kufanikisha azma fulani, mengine si kweli kwa kuwa mtoa habari hakuweko au alihadithiwa na mtu ambaye hakuwa mkweli au pengine hakumbuki vizuri, lakini hiyo ndio hali halisi kutokana na kuwa mengi yaliyokuwa yakitendeka wakati ule hayakuwekwa katika maandishi kutokana na uwoga wa kusema ukweli enzi hizo, na kutokana na ukweli kuwa hata sasa ni vizuri uchunge unachosema kuhusu Mwalimu kwani kama ni mwanasiasa unaweza ukajikuta unatengwa na jamii ukionekana unakinzana na Mwalimu. Lakini mimi si mwanasiasa ni mwanamuziki, na leo nitasimulia ilikuwaje kuwa mwanamuziki enzi za Mwalimu. Mimi ni mzaliwa wa Iringa, nilipata bahati kuzaliwa katika nyumba ambayo muziki ulikuwa sehemu kubwa ya maisha. Wazazi wangu starehe yao kubwa ilikuwa muziki, baba yangu alikuwa mpiga gitaa mzuri aliyerekodi nyimbo zake kwa mara ya kwanza Tanganyika Broadcasting Services (TBC) mwaka 1960 na nyimbo hizo kupigwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha Jimbo Letu, 16 May 1960. baba alilipwa shilingi 40. Hili ni ushahidi kuwa kabla ya Uhuru wanamuziki walilipwa mirabaha kila nyimbo zao zilipopigwa katika redio miaka hiyo!!. IMG_20151014_103437 Niliwahi kumuona baba pia akipiga accordeon, trumpet na saxophone, ila chombo chake haswa kilikuwa gitaa lisilotumia umeme, acoustic guitar akipiga katika katika mtindo wa Folk Music, au mtindo wa kupiga gitaa kwa kutumia vionjo vya utamaduni asili wa mpigaji, nae tungo zake zilitokana na utamaduni wa kabila lake la Kihehe.Akordeon_Morino_V_120_De_Luxe_firmy_HohnerHivyo nilipokuwa mdogo nilishirikishwa kuimba wakati akipiga gitaa na kulipenda muziki toka nikiwa na umri mdogo. Pia nyumbani tulikuwa na radio na gramaphone iliyokuwa na santuri za muziki aina mbalimbali,muziki wa Kiswahili, Kihindi, Kiingereza na muziki toka Afrika ya Kusini, hivyo muziki ulikuwa masikioni muda mwingi wa maisha yangu ya awali.10325634   Nilianza shule mwaka uleule ambapo Tanganyika ilipata Uhuru, nakumbuka tulifagia barabara za jirani na shule yetu kisha kuzimwagia maji ili siku ya Uhuru kusiwe na vumbi. Shuleni kulikuwa na kipindi kilichoitwa ‘Kuimba’, mwalimu alihakikisha anafundisha japo wimbo mmoja kwa wiki, vitabu maalumu vilikuwepo vikiwa na nyimbo zilizokuwa na mafunzo ya maisha, kuheshimu wazazi, wakubwa, kupenda shule na kadhalika. Somo hili lilikuweko katika ngazi zote za shule za msingi, na kulikuweko waalimu wengi waliokuwa wakijua kusoma na kuandika muziki kwa nota hivyo wanafunzi kupewa elimu ya muziki zaidi ya kuimba nyimbo.39177_1575474865695_4871210_n  38929_1575486745992_1262472_n
Shule zote zilikuwa na bendi ya shule. Ambayo kila asubuhi ilipiga muziki wakati wa wanafunzi kukaguliwa kama wamekuja shuleni wasafi, moja ya ndoto za wanafunzi wengi ni kuwa katika bendi ya shule. Aidha kuwa mpiga ngoma au mpiga filimbi na kubwa kuliko yote ni kupata bahati kuwa mshika kifimbo. Shule zilishindana kwa kuzivalisha bendi mavazi bora na upigaji kuwa makini na hivyo siku za sikukuu kila shule ilijitahidi bendi yake ndio iwe bora. Hakika nakumbuka raha iliyokuwepo wakati shule mbalimbali zilipokutana siku ya siku kuu au kukiwa na maandamo na kisha kila bendi kupita mbele ya mgeni wa heshima, wanafunzi tulijitahidi kuwa wakakamavu wenye nidhamu ili shule yetu ishinde.385966614_7bb17e8e14 marangu  Kila shule ilikuwa na vikundi vya kwaya, ngoma za asili na nyingine kuwa na bendi za muziki wa kisasa. Nilisoma shule iliyokuwa na wahindi wengi, Iringa Aga Khan Primary School, bila kujali kabila wote tulicheza ngoma za asili. Hakika kulikuwa na wahindi wanajua kucheza sindimba kuliko waswahili. 168692_1847421224184_6326389_n Siasa ya Ujamaa iliingia wakati niko darasa la saba 1967. Mambo mengi yalibadilika, nyimbo, ngoma ngonjera, mashahiri yakanza kuwa ni ya kisiasa, nyimbo nyingi za kiasili zikapewa maneno ya kisiasa, maafisa utamaduni ndio walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha hili, kwa kuzunguka kuhamasisha na hata kutoa adhabu kwa vikundi vilivyoonekana havitaki kuimba nyimbo za siasa. Mashuleni tulianza kuimba nyimbo za siasa kwa uwingi zaidi, somo la kuimba lilikuwa likifundisha nyimbo za siasa tu. Kwaya zilizokuwa na nyimbo mbalimbali za siasa kutoka kila upande wa nchi, zilirekodiwa na Radio ya Taifa ambayo kwa wakati huu iliitwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD). Uzalendo ulikuwa ndio ‘habari ya mjini’. Kila mwisho wa onyesho la muziki bendi zililazimika kupiga ule wimbo wa ‘Chama cha Mapinduzi chajenga nchitanu yl mwanza 1966 (pichani TANU Youth League Mwanza 1966 wakicheza ngoma)
TANU Youth League (TYL) ilikuwa na matawi kila mahala. Kimuziki TYL ilichangia sana, kwani kila kwenye tawi la TYL lazima kulikuwa na kundi la muziki aidha kwaya au ngoma, na mara nyingi vyote na sehemu nyingi TYL pia ilinunua vyombo vya bendi na hivyo karibu kila wilaya ilikuwa na bendi. Hapa ndipo wanamuziki wengi maarufu wa miaka hiyo na ambao nyimbo zao bado maarufu mpaka leo walikotokea. Pale Iringa, vyombo vya TYL hatimae viliishia kuwa chini ya shule ya Sekondary ya Mkwawa na hivyo pale kulikuwa na bendi nzuri sana ambayo iliweza kuja kurekodi RTD, kati ya waliokuwa wanamuziki wa bendi hiyo, mpia solo ni mzazi wa producer mmoja maarufu wa Bongo fleva na hata yeye alikuja kuwa na bendi yake TZ Brothers, mpiga rythm kwa sasa ana chuo kikubwa cha muziki pale Tabata, wakati muimbaji mmoja wa bendi hiyo alianzisha bendi maarufu pale Arusha.  

Tuesday, October 6, 2015

Smokie Norful - Forever Yours - 2014

Com sua voz de tenor soulful e uma capacidade infalível para fundir gospel contemporâneo, com sensibilidades de hip-hop, Smokie Norful é uma das luzes mais brilhantes no cenário gospel atual. O filho de um Metodista Episcopal ministro Africano, Norful passou seus primeiros 14 anos em Muskogee, OK, Com dois anos , ele estava escolhendo melodias no piano, por quatro, ele estava ativamente tocando e cantando na igreja de seu pai, e por dez anos, ele era um artista de destaque em um álbum personalizado montado por um diretor musical regional. Embora a música era sua paixão duradoura, Norful em vez optou por estudar história na Universidade de Arkansas em Pine Bluff, acabou trabalhando como instrutor de história por quatro anos antes de se mudar para Chicago em 1998, a fim de ganhar um mestrado em Divindade do Seminário Teológico Garrett .

With his soulful tenor voice and an unerring ability to fuse contemporary gospel with hip hop sensibilities, Smokie Norful is one of the brightest lights in today's gospel scene. The son of an African Methodist Episcopal minister, Norful spent his first 14 years in Muskogee, OK, with two years he was picking melodies on the piano, for four, he was actively playing and singing in his father's church, and for ten years he was a featured artist on a custom album assembled by a regional musical director. Although music was his enduring passion, Norful instead chose to study history at the University of Arkansas at Pine Bluff, ended up working as a teacher of history for four years before moving to Chicago in 1998 to earn a master's degree in divinity from Garrett Theological seminary.


01.Mighty God
02.No Greater Love
03.I Need a Word
04.I've Got What You Need
05.Imperfect Me
06.Forever Yours
07.In the Meantime
08.Nothing Is Impossible
09.Run Run
10.He Loves Me
11.I Feel Good
12.Always Remember
13.Love
14.Say So

Clique Aqui Para Baixar (Click Here To Download)

Smokie Norful - Once In A Lifetime - 2012



01.Once in a Lifetime
02.I Need You Now
03.No One Else
04.God Is Able
05.I Understand
06.Justified
07.Um Good
08.In the Middle
09.Dear God
10.Still Say Thank You
11.Where Would I Be
12.Run Til I Finish
13.Nothing Without You
14.Don't Quit
15.Celebrate

Smokie Norful - How I Got Over - 2011


01.Sunday Morning Medley: I'm a Soldier in the Army of the Lord/God Is a Good God/There's a Storm Out on the Ocean/I Want to Live So God Can Use Me/Praise the Lord Everybody (Feat. Myron Butler)
02.Solid Rock (Feat. Melvin Williams)
03.Trouble in My Way (Feat. Vanessa Bell Armstrong)
04.Hymn Medley: Father, I Stretch My Hands to Thee/Amazing Grace/He's a Wonder in My Soul/I Need Thee/Yes Lord/Hallelujah, Thine the Glory (Revive Us Again)/Alleluia
05.The Lord Will Make a Way (Feat. Sheri Jones-Moffett)
06.The Communion Medley: The Blood Will Never Lose Its Power/Oh the Blood of Jesus/There Is Power in the Blood/Nothing But the Blood
07.I Know It Was the Blood (Feat. Joe Ligon)
08.Intro To Amazing Grace
09.Father I Stretch My Hands To Thee Amazing Grace (Feat. Pastor W.R. Norful Sr)
10.He's A Wonder In My Soul I Need Thee Yes Lord (Feat. Pastor W.R. Norful Sr)
11.Hallelujah, Thine The Glory (Revive Us Again) (Feat. Pastor W.R. Norful Sr)
12.I Gotta Praise (Feat. Pastor W.R. Norful Sr)
13.Alleluia (Feat. Pastor W.R. Norful Sr)
14.The Lord Will Make A Way (Feat. Sheri Jones-Moffett)
15.The Blood Will Never Lose It's Power
16.Oh The Blood Of Jesus  There Is Power In The Blood  Nothing But The Blood
17.I Know It Was The Blood (Feat. Joe Ligon)

Clique Aqui Para Baixar (Click Here To Download)