ORCHESTRA SAFARI SOUND ILIPITIA SURA NYINGI KABLA YA KUONDOKA KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI. KATI YA SURA HIZO NI MASANTULA, DUKUDUKU, NA NDEKULE...VIDEO HII NI KIPINDI CHA MASANTULA
Tuesday, April 22, 2014
JIKUMBUSHE ORCHESTRA SAFARI SOUND ENZI ZA MASANTULA LIVE-VIDEO
ORCHESTRA SAFARI SOUND ILIPITIA SURA NYINGI KABLA YA KUONDOKA KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI. KATI YA SURA HIZO NI MASANTULA, DUKUDUKU, NA NDEKULE...VIDEO HII NI KIPINDI CHA MASANTULA
Sunday, April 13, 2014
Monday, April 7, 2014
Sunday, April 6, 2014
PROFESA JUMA BHALO AMEFARIKI DUNIA NA KUZIKWA MOMBASA
Juma Bhalo alizaliwa 1942 huko Shela katika wilaya ya Malindi. Mwaka1954, alijiunga na shule ya msingi ya Sir Ali bin Salim , wakati huohuo familia yake ilihakikisha anahudhuria Madrassa ili kupata elimu ya dini. Bhallo mwenyewe aliwahi kusema hamu yake ya kuimba ilimuanza katika wakati huu na sauti yake kuwa na mvuto kutoka kipindi hiki alipokuwa Madrassa Akiwa na miaka 9 tayari muda wake mwingi ulitumika kusikiliza santuri, na akili yake ilianza kupenda sana muziki. Hakumaliza elimu ya msingi kwa kuwa wazazi wake walishindwa kulipa ada ya shule. Mwaka 1957 alihamia Mombasa na kupata kazi Forodhani, akiwa Mombasa alianza kukutana na kushirikiana na wanamuziki wa Taarab wa Mombasa. Hakuipenda sana kazi ya Forodha hivyo 1959 akahamia Tanga kwa mjomba wake, na hapo akajiunga na kundi maarufu la Taarab wakati ule lililoitwa Young Noverty, hapa alipata ujuzi mkubwa wa muziki wa Taarab.
Alirudi kwao Malindi kwa muda mfupi na hatimae kurudi tena Tanga 1962 na kujiunga na kundi la Young Stars Taarab. Mwaka 1966 alirudi Mombasa na kuanzisha kundi la Bhalo and Party, kundi ambalo amedumu nalo mpaka Mauti yake. Mwaka 2007 baada ya zaidi ya miaka 50 ya kuwemo katika muziki wa Taarab, Juma Bhalo ambaye wapenzi wake walimuita Profesa na hata Mfalme wa Taarab alitangaza kuacha kufanya maonyesho ya wazi ya Taarab, alitangaza hilo siku alipopiga katika harusi ya mwanae. Alistaafu kazi hiyo kwa maneno yafuatayo "Waswahili wasema kiwate kitu kabla hakijakuata. Kwa hivyo kama mulivyo nishuhudiya usiku huu nlivyowatumbuiza ambavyo ni kama kawaida yangu basi leo hii usiku huu kabla hawajaja watu wakasema ahhhhh Bhalo ashazeeka hawezi tena kuimba kwa hivyo najiuzulu ningali bado niko fiti. Kwa hivyo siimbi tena hadharani kikazi. Nawashkuru kwa ushabik wenu na musijali Mungu akiniwezesha Kasseti mpya ntawatoleya".

Taarab yake iliegemea sana muziki wa Kihindi na hivyo kuwa tofauti na taarab nyingine,
MUNGU AMLAZE PEMA PROFESA ,
Kwa wale wanaopenda kusikiliza au kununua nyimbo zake waingie HAPA Angalia video ya mwanae Anwar Juma Bhallo
Sunday, March 30, 2014
Saturday, March 22, 2014
MARCH 23 2014, MIAKA 19 TOKA KIFO CHA MWANAMUZIKI MARIJANI RAJABU-DOZA..BY FRED MOSHA
Machi 23 mwaka 1995 ni siku isiyosahaulika kwa wapenzi wa muziki wa zamani nchini. Siku hiyo ndipo tulipompoteza mwanamuziki kipenzi chetu, Marijani Rajabu. Alizikwa kesho yake yaani Machi 24 kwenye makaburi ya Kisutu.
Historia ya gwiji huyu inaanzia Machi mwaka 1955. Mara baada ya kumaliza elimu yake ya Sekondari, Marijani alijitosa moja kwa moja kwenye muziki licha ya kuwa awali aliwahi kuwa Mlinda Mlango hodari kwenye timu mbalimbali ikiwemo Timu yake ya Shule. Mwaka 1970 alikuwa miongoni mwa wanamuziki wa bendi ya STC Jazz na kushiriki kuimba na kutunga vibao kadhaa. Ewe mwana inaweza kuwa ndio wimbo maarufu zaidi. Mwaka 1972 alijiunga na The Trippers ya David Mussa ambayo kwa wakati huo ilikuwa inapiga zaidi nyimbo za hoteli na za kukopi na muimbaji wao kiongozi wakati huo alikuwa Ali Rajabu. Kuingia kwa Marijani kukaleta mapinduzi mapya kabisa ndani ya bendi na muziki wake. Ikiathiriwa zaidi na muziki wa vijana wakati huo, muziki wa Soul, Trippers ambayo punde ikaongeza neno Safari kwenye jina lake ilianza kupiga na kutunga nyimbo zake kali na ambazo hata leo hii bado zinakumbukwa. Wimbo Georgina ni mfano tu. Marijani alishiriki kutunga, kuimba nyimbo karibu zote za Trippers sanjari na kupiga gitaa kwa baadhi ya nyimbo. Mfano wimbo Olila ambao alipiga rhythm na kuimba. ![]() |
| Safari Trippers-Marijani wa pili toka kulia waliosimama. Wa kwanza mwenye kofia ndie mtunzi wa wimbo Georgina- Uvuruge |
![]() |
| Tanzania All Stars..Marijani wapili toka kulia |
Sunday, March 9, 2014
URAFIKI JAZZ BAND 2
![]() |
| Urafiki Jazz Band |
Bendi ya Urafiki ikiwa katika hali yake ya uchanga mwaka 1970 ilipata ajali ya gari, wakati kundi zima likitoka katika onyesho huko Chang’ombe, gari lao aina ya Volkswagon Kombi liligonga mti maeneo kona ya Kigogo na Msimbazi Mission.
Baadhi ya wanamuziki waliumia sana na gari lao, likawa halifai kabisa.
Wapigaji walioumia walikuwa ni Hamisi Mashala – Drummer Boy - alivunjika mguu, Mohamed Bakari Churchil aliumia kichwani na kushonwa nyuzi kadhaa, na pia Ayoub Iddi Dhahabu na Maarifa Ramadhani walipata maumivu makali kwa ndani mwilini.

Bendi ilisimamisha maonyesho yake kwa muda hadi wanamuziki wake walipopata nafuu na kuanza maonyesho tena. Hali ya ajali ile ilileta fikra mbaya kwa wanamuziki hao na wapenzi wao na ilionekana kana kwamba kulikuwa na mkono wa mtu katika ajali ile. Juma Mrisho ‘Ngulimba’ alitunga wimbo ‘Nimekosa Nini Jama’, wimbo ulioelezea kadhia hiyo. Katika kipindi hiki dhana ya ushirikina ilitawala sana katika bendi mbalimbali. Vifo vya wanamuziki mara nyingi vilihusishwa na upinzani katika bendi.
Kufikia miaka ya ‘80’ kati bendi ya Urafiki ikawa inasua sua kutokana na uchakavu wa vyombo na Menejimenti iliyokuwepo wakati huo haikuwa tayari kutoa pesa kununulia vyombo vipya. Bendi ya Urafiki ilifikia tamati katika miaka ya ‘80’ kati kati na bendi hiyo ikatoweka katika anga za muziki na kubaki historia.
Subscribe to:
Posts (Atom)