Thursday, March 29, 2018

MIMI MARS :SIWEZI KUOLEWA NA MWANAUME WA KABILA LA WAPARE

Msanii ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya 'Sitamani' chini ya Mdee Music, Mimi Mars amesema hawezi kujihusisha mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwenye kabila la Mpare kwa madai makabila hayo wanatabia ya ubahili na kujisikia. 

Mimi amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuulizwa swali na ripota wa kipindi hicho kuwa anatamani mwanaume wa...
kabila gani ambaye awe naye katika mahusiano au ndoa.

"Kutokana na mimi mwenye kuwa ni Mpare kwa hiyo tabia za wanaume wa kipare ninazifahamu vizuri halafu wanasema mafahari wawili hawezi kukaa zizi moja hivyo najua tutashindwana tu kwasababu wote tunajisikia, wabahili 'so' tukikaa wawili 'type' hiyo mambo yatakuwa magumu", amesema Mimi Mars.

Pamoja na hayo, Mimi ameendelea kwa kusema "inanibidi nitafute kabila ambalo tofauti na mimi ndio maana sitoweza kuwa kabila hilo ila sio kwa ubaya ila mimi mwenyewe tu nimesema sitoweza.

Download: Wakwanza x Vidy Mb_Sikati Tamaa rmx


Download

Watch & Download: Ervixy ft Mwana FA_Text (Official Video)


Watch Here

Download: Orezi_Ijo Wakanda


Download

FAIZA ALLY ATEMA POVU BAADA YA ZARI KUPATA DILI NCHINI TANZANIA


Tokeo la picha la zari dili nono
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Faiza Ally huenda akawa ni moja ya mastaa ambao wamekasirishwa na kitendo cha mwanamama Zari kupata dili la kutangaza nepi za watoto za Soft Care. 

Faiza Ally amesema kuwa ameshangazwa na kampuni hiyo kumtumia Zari kutoka Uganda kwenye matangazo yao ile hali kuna Watanzania wengi na wenye majina ambao...
wangetumika kutangaza bidhaa zao.

“I know this is gonna look bad for somepeople but let me be honest , how stupid Tanzanian can be , mastaa wote watanzania , watu wote watanzania hamkuona hata mmoja anae stahili kupata dili zaidi ya zari ? Ina maana uhitaji bongo umeisha mpaka tuweke watu kutoka nje ?? Kwa nini tunawapa kipa umbele wageni tunajizarau sisi ??? Mlishawahi kuona Uganda na kenya wamempa nani dili wakamuacha wa kwao ?? Eti sasa hivi mganda na mkenya wanapongezan na sisi wote tunaonekana hatukufaaa,“ameandika Faiza Ally kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, Faiza amemshangaa mwanamitindo Noel ambaye yeye ndiye aliyehusika kwa kiasi kikubwa kufanya connections hadi Zari kupata dili hilo.
“Noel you know all the Tanzania star na uko karibu hukuona anae faa ? I don’t hate zari but I hate kuona vitu wanavyo stahili kupata watanzania kapata mganda this is no good ! Hakuna nchi duniani utaenda ukaona mgeni anapewa kipa umbele zaidi ya mwenyeji , kiasi mpaka ukiwa unasuburi tax mpaka mwenye nchi apate na wewe ndio unafata,“ameeleza Faiza Ally.

Mtazamo wa Faiza umepigwa na baadhi ya Watanzania waliotoa maoni yao kwenye posti yake wakidai kuwa wanawake wengi wa Tanzania wanautumia umaarufu wao vibaya.

mimahrayvannyWabongo mpo serious na Instagram mganda yupo serious na kazi acha tu apewe.
 
oddy_is_a_baeMarekani yenyew iliongozwa na mkenya sembuse Tz mwachen zari wa watu anastahili
rukkysaidWanaangalia vitu vingi dear,kwa mfano wewe ile post ya mchupi umechoka vile kweli wanaweza kukupa dili km hyo kirahis.
iam_g_mtonyohakuna mtu anayeweza kushawishi kuwa balozi @faizaally_ kwanza hatujui kujiwekea brand alafu tupo cheap sana unafikiri angeenda mbongo hicho kitu kisingejulikana yaana hakuna wa kutustua bongo, wenye makampuni wanatarget za mbali sio za hapo ulizofikiria wewe..! Zari ni brand tosha kama ulikuwa hujui, na anajimudu. SASA wewe kwa mfano ndo kampuni ni yako ungemuita nani aje kuwa barozi!
 
mwana_heriFaiza jamaniii kha eti “hakuna nchi duniani utaenda ukaona mgeni anapewa kipaumbele zaidi ya wenyeji” iiii hamjuwi mambo ya nchi zilizoendelea  HEAD OF THE BANK OF ENGLAND IS A CANADIAN CITIZEN (one of the top jobs available) because he was the best man for the job! First foreigner to run that institution in over 300 years but they had to make changes walisikia how successful alivyokuwa akiwa head of the Canadian bank. Sisi wa chini huku ndio usiseme! Mpaka unajiuliza kwa nini hawakumpa hii kazi mwenzao? Ma employer hapa wanaajiri sana watu wa eastern European sana wakiulizwa kwa nini hamuajiri watu wenu jibu ni moja “they are lazy and have no work ethic” mara leo mgonjwa, mara kesho kafiwa, mara anataka holiday! Muajiri ataweza? Lazima achukuwe mfanyakazi bora! Wewe unaonekana kama ni mpambanaji endelea tu kujitahidi please acha roho ya kwa nini mwenyeezi mungu hapendi, mshukuru tu kwa anachokupa akuongezee na juwa cha mwingine hakiwezi kuwa chako.
 

Jana Machi 28, 2018 Zari alisaini dili hilo nono la kutangaza bidhaa za Softcare Diapers ingawaje bado haijajulikana mkataba huo umemuingizia kiasi gani cha fedha.

DMX AHUKUMIWA MWAKA MMOJA KWENDA JELA

Rapper kutoka nchini Marekani anayeunda kundi la Ruff Ryders, DMX amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kukwepa kulipa kodi. 

DMX alikamatwa July mwaka jana, kwa mujibu wa CBS rapper huyo anadaiwa kiasi cha dola milioni 1.7 ambapo inasemekana alifungua akauti benki nyingine na kutumia jina jingine ili kukwepa...
kodi.

DXM alikuwa akikabiliwa na mashtaka 14 ya ukwepaji kodi, hata hivyo alilipa faini ya dola 5000,000 za Kimarekani kinyume na hapo angetumikia kifungo cha miaka 44 jela.
Imeripotiwa kuwa DMX ameingiza zaidi ya dola milioni 2.3 kwa mwaka 2010 hadi 2015 lakini msanii huyo alikwepa kulipa kodi. Rapper huyo ni baba wa watoto 15.

TAMMY THE BADDEST: MSANII ILI UUZE UNATAKIWA UWE NA MUONEKANO


Female Rapper Tammy The Baddest amesema muonekana wa msanii mbele ya mashabiki wake una nafasi katika kuuza muziki wake anaofanya. Tammy amesema kuwa msanii si kuandika nyimbo tu na kuingia studio kurekodi bali hata muonekano wake ni kitu cha kuzingatia.

“Msanii kama msanii hasa mtoto wa kike unatakiwa uwe full package, sio unaonekana tu umefanya muziki basi, no!, you have to sale, ili kuuza ni lazima uwe na muonekano mzuri hata kama una shida mtu...
aone mmmh!, kumpa Tammy show kiasi fulani hapana,” Tammy amefunguka.

Ameongeza kuwa muuoneka wake ndio kila kitu kwake japokuwa muda mwingine inakuwa tabu kwake kwa kuwa baadhi ya mashabiki wake hufikiri ana fedha nyingi kitu ambacho si kweli.