
Thursday, March 29, 2018
Thursday, March 22, 2018
LEO TUNATIMIZA MIAKA 23 TOKA ALIPOFARIKI MARIJANI RAJAB, FAMILIA YAKE KUFANYA HITMA...video ya Marijani akiwa jukwaani
ALHAMISI, Machi 23 mwaka 1995 ndio siku alipofariki mwanamuziki gwiji mtunzi muimbaji na mpiga gitaa Marijani Rajabu. Alizikwa kesho yake Ijumaa Machi 24 kwenye makaburi ya Kisutu.
Leo hii 23 Machi 2018 familia ya gwiji huyu itafanya hitma kwa kumbukumbu ya marehemu baba yao, nyumbani kwa binti yake mkubwa huko KIjichi.
Historia ya gwiji huyu inaanzia siku alipozaliwa tarehe 3 Machi mwaka 1955, katika eneo la Kariakoo. Mama yake alikuwa mama wa nyumbani wakati baba yake alikuwa na shughuli za uchapishaji. Maisha yake ya utoto yalikuwa ya kawaida ila alikuwa kipenda sana uimbaji wa Tabu Ley na mwimbaji mmoja wa Guinea Sorry Kandia. Alisoma shule ya Msingi ikiambatana na elimu ya Madrasa. Mwaka 1970 Akiwa bado shuleni, utaona umri wake ulikuwa miaka 15 tu, alijiunga na STC Jazz, ikiwa chini ya mpiga gitaa maarufu wakati huo Raphael Sabuni, kabla ya hapo bendi hii ilikuwa unajulikana kama The Jets. Katika bendi hii Marijani aliweza kutoka nje ya Tanzania kwa mara ya kwanza ambapo alikwenda Nairobi na kurekodi nyimbo zilizotoka katika label ya Phillips., hili jambo la mwanafunzi kusafiri na bendi likaleta shida na kwa vile STC ilikuwa mali ya umma akaachishwa kazi na mwaka1972 alijiunga na The Trippers ya David Mussa ambayo kwa wakati huo ilikuwa inapiga zaidi nyimbo za hoteli na za kukopi na muimbaji wao kiongozi wakati huo alikuwa Ali Rajabu. Hapa ndipo ubora wake ulifunguka haswa na kuweza kuinyanyua Trippers, ambayo sasa ilibadili jina na kuwa Safari trippers kutokana na msimamo wa serikali wakati huo wa kutaka majina ya nyumbani yatumike bala ya yale ya kigeni na kuwa moja ya bendi maarufu za wakati huo. Waliweza kutoa vibao vilivyopendwa mfululizo na kuweza kuzunguka nchi nzima. Vibao kama Rosa nenda shule, Georgina,Mkuki moyoni, viliweza kuuza zaidi ya nakala 10000 za santuri na hivyo kuwezesha bendi kuwa na vyombo vyake vizuri. Bendi wakati huo ikiwa na wanahisa wanne, ambao kwa bahati mbaya wakati bendi ndio iko juu, wakakosa kuelewana na ukawa ndio mwisho wa bendi hiyo. Marijani alishiriki kutunga, kuimba nyimbo karibu zote za Trippers sanjari na kupiga gitaa kwa baadhi ya nyimbo. Mfano wimbo Olila ambao alipiga rhythm na kuimba.
Mwaka 1976, Marijani na baadhi ya wanamuziki wa Trippers waliamua kuihama bendi na kwenda baadaye kuasisi Dar es salaam International chini ya umiliki wa Mzee Zakaria Ndabemeye ambaye bado yu hai hadi sasa. Baadhi ya wanamuziki hao ni pamoja na Abel Baltazar kutoka Msondo, Kassimu Mponda kutoka Trippers, Abdallah Gama, Joseph Mulenga, Haruna Lwali na George Kessy Omojo waliokuwa wanapiga muziki Magot pale, Said Mohamed kutoka Polisi Jazz, Cosmas Chidumule kutoka Urafiki, Belesa Kakere kutoka Biashara Jazz, Joseph Bernard kutoka Trippers, Ali Rajabu kutoka Trippers, na King Michael Enock kutoka Dar es salaam Jazz. Akiwa Dar Inter alishiriki kutunga nyimbo mbili, Betty na Sikitiko. Hata hivyo kama waswahili wanavyosema mafahari wawili hawakai zizi moja ndivyo ilivyotokea kati yake na Abel Balthazal kiasi cha hatimaye Marijani kufukuzwa ndani ya bendi kutokana na ubishi kuhusu wimbo aliotunga Marijani, kuna maelezo kuwa wimbo ulionekana unafanana na wimbo fulani toka Kongo na hivyo Marijani akatakiwa aubadilishe na ndipo ugomvi ukaanza. Hata hivyo mwishoni mwa mwaka 1978, Marijani alirejeshwa tena kundini kutokana na rundo la wanamuziki wa Dar Inter kuihama bendi kwa kishindo kikubwa na kwenda kuifungua bendi mpya kabisa ya Orchestra Mlimani Park. Aliporejeshwa Marijani alikuja na wanamuziki wengi wapya wakati huo kama akina Christopher Kasongo, Mohamed Tungwa, Mafumu Bilal, Hamis Milambo, Athuman Momba, Mzee Alex Kanyimbo na wengine na kuja na mtindo wa Super Bomboka. Katika kudhihirisha hasira zake kwa Abel, Marijani alimtungia Abel wimbo wa kumnanga ukiitwa Kidudu mtu ambao hata hivyo RTD waliukataa kuurekodi, jambo lililokuwa kawaida enzi hizo kwa redio kukataa wimbo. Sifa nyingine ambayo Marijani alikuwa nayo ni kuibua wanamuziki chipukizi kama alivyofanya mwaka 1983 alipomuibua kutoka Tanga kijana Mkuu Waziri Kungugu Kitanda Milima almaaruf Fresh Jumbe ambaye kwa hakika kabisa Marijani hakujutia kumchukua kijana huyo. Alimuamini kupita maelezo kiasi kwamba wakati mwingine alikuwa akimuachia bendi aongoze na yeye anapumzika nyumbani. Mbali na Fresh, wanamuziki wengine ni kama vile Tino Masinge, Mohamed Mwinyikondo, Juma Choka na wengine kibao. Ni vizuri kuelezea hapa kuwa kadri ya maelezo yake mwenyewe marehemu baada ya kurekodi Zuena na Mwanameka na nuimbo nyingine katika album hiyo alichoambulia ni malipo ya nauli toka RTD ya sh 2500/- tu. Kilichosikitisha zaidi ni kuwa nyimbo zao tisa ziliuzwa kwa kampuni ya Polygram bila ridhaa yao.
Hata hivyo safari ya Dar International ilikoma mwaka 1987 kutokana na sababu za kawaida za kufa kwa bendi lakini kubwa ni uchakavu wa vyombo. Hata hivyo Marijani aliendelea kufanya muziki na kwa kipindi kifupi amewahi kucheza na Kurugenzi ya Arusha na Mwenge Jazz ambayo alirekodi nayo wimbo mmoja wa Ukimwi na hata kupitia bendi ya Watafiti ambayo hatimae ilikuja kuwa 38.. Mwaka huohuo wa 1987 Marijani na Muhidin Maalim Gurumo waliliongoza kundi la wanamuziki zaidi ya 50 kutunga nyimbo maalum hasa kwa maadhimisho ya miaka 10 ya CCM na 20 ya Azimio la Arusha. Naizungumzia Tanzania All Stars. Aidha mwaka 1994 aliwahi kurekodi zong zing na marehemu Eddy Sheggy. Bendi yake ya mwisho ilikuwa ni Africulture ama Mahepe Ngoma ya Wajanja, iliyokuwa mali ya Rogers Malila, alikokuwa na wanamuziki kadhaa kama akina Hassan Kunyata, Mgosi na wengine. Bado Marijani ataendelea kukumbukwa na wapenda muziki kote nchini na hata Afrika kwa ujumla kwa nyimbo zake zenye mafundisho na tamu huku akienzi utamaduni na ngoma za kwao Kigoma.
VIDEO YA MARIJANI AKIWA JUKWAANI
VIDEO YA MARIJANI AKIWA JUKWAANI
Monday, March 19, 2018
CHRISTIANO RONALDO AWA MCHEZAJI WA KWANZA KUFUNGA MABAO MENGI MWAKA 2018

Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amemfunika nyota wa Barcelona Lionel Messi pamoja na washambuliaji wengine akiwa ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi ndani ya mwaka 2018.
Ronaldo amefanikiwa kufikisha mabao 21 kwenye mashindano yote tangu mwaka 2018 uanze, baada ya jana usiku kufunga mabao 4 kwenye ushindi wa...
mabao 6-3 iliyopata Real Madrid dhidi ya Girona.
Kwa idadi hiyo ya mabao imemfanya nyota huyo raia wa Ureno kuwazidi nyota kadhaa akiwemo mpinzani wake Lionel Messi mwenye mabao 16 pekee ndani ya mwaka 2018 katika michuano yote.
Kwa upande mwingine Ronaldo amefanikiwa kufunga Hat-trick yake ya 50 katika maisha yake ya soka. Kati ya hizo 44 ameifungia Madrid, 5 timu ya taifa ya Ureno na 1 Manchester United.

Mbio za kiatu cha dhahabu kwa La Liga maarufu (PICHICHI) zinaongozwa na Messi mwenye mabao 25 akifuatiwa na Ronaldo mwenye mabao 22. Mbio za Ubingwa zinaongozwa na Barcelona wenye alama 75 wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye alama 64.
Ronaldo amefanikiwa kufikisha mabao 21 kwenye mashindano yote tangu mwaka 2018 uanze, baada ya jana usiku kufunga mabao 4 kwenye ushindi wa...
mabao 6-3 iliyopata Real Madrid dhidi ya Girona.
Kwa idadi hiyo ya mabao imemfanya nyota huyo raia wa Ureno kuwazidi nyota kadhaa akiwemo mpinzani wake Lionel Messi mwenye mabao 16 pekee ndani ya mwaka 2018 katika michuano yote.
Kwa upande mwingine Ronaldo amefanikiwa kufunga Hat-trick yake ya 50 katika maisha yake ya soka. Kati ya hizo 44 ameifungia Madrid, 5 timu ya taifa ya Ureno na 1 Manchester United.

Mbio za kiatu cha dhahabu kwa La Liga maarufu (PICHICHI) zinaongozwa na Messi mwenye mabao 25 akifuatiwa na Ronaldo mwenye mabao 22. Mbio za Ubingwa zinaongozwa na Barcelona wenye alama 75 wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye alama 64.
MADEE: SIWEZI KUACHA MUZIKI LABDA NIFE

Madee ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) inayorushwa na EATV baada ya msanii huyo kuonekana kusajili wasanii wake wapya kila...
kukicha jambo ambalo lilipelekea baadhi ya watu kudhania pengine Madee ana mpango wa kuacha na kuimba kwa sasa.
"Music my life yaani toka napata akili naanza muziki nikasema nitakuachana na kazi hii labda siku ambayo nitakuwa nimemaliza pumzi zangu 'kufa'. So hata kama ntakuwa sipeleki nyimbo kwenye stesheni mbalimbali, si-rekodi lakini ntakuwa bado ntakuwepo nimeegemea kwenye biashara ambayo itakuwa inahusiana na muziki", amesema Madee.
DIAMOND AWEKA REKODI YOUTUBE AMTUPA MBALI DAVIDO NA WIZKID
Wazungu wanasema ‘Hard work Pays’ huu msemo unajidhihirisha kwa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye kila kukicha anaendelea kuweka rekodi kwenye muziki wake na awamu hii sio views wa kwenye mtandao wa YouTube bali ni Subscribers.
Diamond kwenye akaunti yake ya YouTube tayari amefikisha Subscribers milioni 1+ na kuwa msanii wa muziki wa 8 barani Afrika kuwa na...
Subscribers zaidi ya milioni 1.
Kwa sasa Diamond Platnumz ameungana na wasanii kama Amr Diab kutoka Misri mwenye Subscribers milioni 1.6, Kundi la muziki la Die Antiwoord kutoka Afrika Kusini subscribers milioni 1.8, Dzjoker Chemsou milioni 1.6, Lartiste milioni 2.2, Ilias Tiiw milioni 1.8, Sofia Carlsberg milioni 1.8 .
Wengine ni Tamar Hosny milioni 2.8, shady Srour milioni 2.8 wote kutoka Misri na Saad Lamjarred kutoka Morocco ambaye ndiye msanii wa muziki anayeongoza kwa bara la Afrika kuwa na Subscribers wengi milioni 4.4 .
Kwa upande wa wasanii wengine kutoka Afrika kama Davido, Wizkid, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sarkodie, Alikiba na Cassper Nyovest wote bado hawajafikisha Subscribers milioni 1 ingawaje hao wanatumia mtandao wa VEVO, na akaunti inayoongoza kuwa na Subscribers wengi ni ile ya kundi la PSquare ina subscribers laki 7.
Wiki iliyopita Diamond Platnumz aliachia album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ na tayari imepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki barani Afrika ambapo imeanza kutrend kwenye mitandao ya kununulia nyimbo kwenye baadhi ya nchi kama Burkina Faso.
BLACK PANTHER YAZIDI KUWEKA HISTORIA YAINGIZA BILIONI 1.182.5
Filamu ya ‘Black Panther’ imezidi kufanya vizuri katika mauzo yake duniani. Filamu hiyo imetajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 605.4 kwa Marekani ndani ya mwezi mmoja tangu ilipotoka February 16 ya mwaka huu, pia imeingiza kiasi cha dola bilioni 1.182.5 duniani kote.
Kutokana na kiasi hicho kilichoingiza filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Marvel Studios, imevunja rekodi zilizowahi kuwekwa na filamu kibao kwenye...
box office.
Black Panther ambayo imeongozwa na Ryan Coogler, ilitumia bajeti ya kiasi cha dola milioni 200–210 katika kuitengeneza.
Black Panther imewakutanisha waigizaji kama Chadwick Boseman ambaye ndio staa wa filamu hiyo, Lupita Nyong’o, Michael B. Jordan, Danai Gurira, John Kani na Connie Chiume.
Subscribe to:
Posts (Atom)

