Rapper Femi One kutoka nchini Kenya, amefunguka kuhusu wimbo wake mpya wa ‘Zaga Zaga’ na sabau za kumshirikisha Mejja kwenye ngoma hiyo.Akiongea na Bongo5, rapper huyo wa kike ambaye yupo chini ya lebo ya Kaka Empire, amesema kuwa ngoma hiyo inamliwaza mtu anapokuwa na matatizo na pia ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu kufanya... kazi na Mejja.“Kufanya kazi na Mejja imekuwa ndoto yangu ya muda mrefu, na wakati alipokubali kufanya kazi na mimi ilikuwa ni ndoto ya kweli,” amesema Femi.“Zaga Zaga ni wimbo mzuri ni unaenda kwa mtu yeyote anayetaka kuwa na wakati mzuri baada ya mawazo mengi. Watu wangu wote wa Eastlando ukiskia hii ngoma weka shida zako kando,” ameongeza.
Inawezekana wewe ni moja kati ya watu wanaopenda chocolate kama kitafunwa (snack) lakini je umewahi kuhisi kuna chocolate ya gharama ya juu zaidi kiasi cha kupelekwa kwenye maonyesho ya biashara?.Basi jana March 16, 2018 chocolate inayodaiwa kuwa ya gharama ya juu zaidi duniani ilipelekwa kwenye maonyesho ya biashara kwenye Mji wa Obidos nchini Ureno.Chocolate hiyo ambayo ni ya gharama ya Euro 7,728 ambayo ni sawa na Fedha za Kitanzania Shilingi Milioni 20.7, imefunikwa na... dhahabu inayoweza kuliwa, na imetengenezwa na vitu vingine ikiwa ni pamoja na truffle nyeupe, nyuzinyuzi za saffron, na vanilla kutoka Visiwa vya Madagascar.Mtengenezaji wa chocolate hiyo Daniel Gomes ambaye ni raia wa Ureno ameeleza kuwa chocolate hiyo ambayo ina umbo la fedha imepewa cheti cha kutambuliwa kama Chocolate ya gharama ya juu zaidi duniani na Kitabu cha Kumbukumbu cha Guiness mwaka 2017.
Staa wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani Calvin Cordozar Broadus ambaye wengi wanamfahamu kwa jina maarufu kama Snoop Dogg alitangaza kuachana na muziki wa Hip Hop (kidunia) na kumrudia Mungu kwa kuanza kufanya nyimbo za dini.March 16 Snoop Dogg ameachia rasmi album ya nyimbo za injili inayokwenda kwa jina la ‘Bible of Love’ mkongwe huyo katika muziki wa Hip Hop March 16 ameachia album yake hiyo ya gospel, baada ya... kufanya muziki wa kidunia na kutoa jumla ya album 15 za Hip Hop, Snoop anafanya maamuzi hayo akiwa na umri wa miaka 46 sasa.Album mpya ya Snoop Dogg alioitoa March 16 ‘Bible of Love’ amewashirikisha wasanii mbalimbali kama Pattie Labelle, Rance Allen, The Clark Sisters, Faith Evans, Kim Burrell, B. Slade Charlie Wilson, Marvin Sapp, Tye Tribbett, James Wright Chanel, Isaac Carre, Fred Hammond, Chris Bolton, Uncle Chuce, John P. Kee, Mali Music, Mary Mary, Lonnie Beareal na Jazze Pha.
Msanii wa BongoFleva Q Chief ameibuka na kujitetea kuwa hana tofauti yeyote ile na Papii Kocha pamoja na Nguza Vicking ila kuna baadhi ya watu ndio wanataka kuwatia ubaya kuhusiana na kuzimiwa MIC akiwa kwenye jukwaa akitumbuiza. Q chief ametoa kauli hiyo akiwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea msanii huyo kuzimiwa MIC kwenye 'show' ya... kuwakaribisha kwa mara nyingine katika tasnia ya muziki Papii na mzee Nguza kutokana na kupotea kwa miaka mingi kwa machoni mwa mashabiki na wapenda burudani wa dansi."Wakati mimi nina 'perfom' wimbo wangu wa kwanza katika 'show' wa nikilala naota, nilipata baraka zote kutoka kwa MC wa shughuli, Papii na Baba pia. So kwenye kazi unapoona watu wanamuitikio mzuri inabidi ujiongeze kutokana na wao kuonesha mapenzi yao hivyo mimi nimefanya kazi yangu kama vile ninavyofanya sehemu nyingine kwasababu nina nguvu nyingi katika kazi zangu lakini baadae wakati napanda juu nikashangaa kati kati ya wimbo nimezimiwa kipasa sauti 'MIC'", amesema Q chief.Pamoja na hayo, Q chief ameendelea kwa kusema "sitaki kuweka kama kulikuwa na tofauti lakini kama zilikuwepo basi nilikuja kujizua baada ya kuangalia zile video tena na watu wa karibu pamoja na mke wangu kuniuliza ni jambo gani lilikuwa linaendelea mpaka kutokea vile. Lengo langu lilikuwa ni kutoa burudani, kumfariji rafiki ambae alipotea machoni mwangu kwa muda mrefu kwa mapenzi yote lakini MIC ikazimwa, sio kosa la Papii wala Mzee wangu Nguza kwasababu wao hawaitahi 'stress' bali ni kosa la ambaye alikuwa fundi mitambo 'technical' aliyekuwepo nyuma anashughulikia masuala ya vyombo vyote"
Muigizaji wa filamu mwenye nyota yake bongo na Afrika Mashariki Wema Sepetu, amedai amevumilia matusi vya kutosha anayotukanwa na kupitia mitandao ya kijamii bila kosa lolote hivyo kwa sasa ataenda nao hatua kwa hatua. Wema Sepetu ametoa kauli hiyo alasiri ya jana (Machi 16, 2018) baada ya baadhi ya watu kupenda kumtolea maneno machafu na kumdhihaki kwa jambo ambalo yeye... hakupenda awe nalo au limfike katika maisha yake."Naona mmeshanikariri hua nakaa kimya pale mnapo ona 'comment' ya matusi, nimepuuzia kwa muda mrefu mno ila tukumbuke kuwa na mimi nina moyo ambao una nyama tena ni binadam kama nyie tu. Kama vile usivyopenda kuona mtu anakukebehi basi ndio hivyo hivyo ninavyo 'feel', kwani lazima matusi?, hakuna asiyejua kutukana kwenye ulimwengu huu tena midomo michafu haswa ila tunajitahidi kujistiri", amesema Wema.Aidha, Wema Sepetu amesema hakuna jambo ambalo linamkera kupita kiasi kama kuona anatukanwa kupitia 'social media' tena kwenye ukurasa wake mwenyewe. "Kwani kuna ulazima ku-coment tena matusi 'sometimes' mtu anaweza 'ku-push ur buttons to the extent when it comes to me nina extents' zangu 'and u don't go there', navumilia vingi mno jamani kweli kweli. 'Try putting yourselves in my shoes for a minute and see if they fit'. Ukipost kitu chako kuna ile mijitu iliotapikwa inakuja na maneno yao ya chooni utasema imetumwa. Kwani ni mashindano?, sio poa jamani", amesisitiza Wema.Kwa upande mwingine, Wema Sepetu amewakumbusha baadhi ya watu wenye tabia hiyo kuwa naye ni binadamu kama walivyo wao na mwenye moyo wa nyama na wala sio chuma hivyo anasikia maumivu makali kama wayapatao wao pindi wakitukanwa katika mitandao ya kijamii.