UNGEPENDA KUSIKIA AU WIMBO MAALUMU WA ZAMANI, AU KUJUA HABARI ZA MWANAMUZIKI WA ZAMANI TUMA SMS KUPITIA +255 763 722557, NA JIBU UTALIPATA KUPITIA EFM RADIO 93.7FM KILA JUMAPILI KUANZIA SAA 2-5 USIKU NA PIA KUPITIA KURASA ZA BLOG HII
Monday, June 30, 2014
Sunday, June 29, 2014
KATIKA KIPINDI CHA ZAMA ZILEE 93.7FM LEO
![]() |
| BEMBEYA JAZZ TOKA GUINEA |
Monday, June 16, 2014
KIJIWE CHA KITIME SASA PIA KATIKA 93.7 FM REDIONI KILA JUMAPILI
Kila Jumapili kuanzia saa 2 hadi saa 5 usiku kupitia EFM 93.7 Fm, ntakuwa nikikuletelea muziki wa zamani kutoka ulimwenguni kote. Kipindi hiki kitakuwa kikirushwa kupitia radio mpya EFM. Katika kipindi hiki licha ya muziki pia kutakuwa na hadithi mbalimbali kuhusiana na muziki na maisha yalivyokuwa wakati huo. Unaweza kuwasiliana nami kupitia ukurasa wa Facebook huu https://www.facebook.com/pages/ZAMA-Zileeeee/288646357969709 ingia hapa u Like ukurasa huu na kutoa mapendekezo ya unachokitaka. Pia unaweza kuipata redio hii katika mtandao wa internet kupitia http://tunein.com/radio/E-FM-Radio-937-s224740/ haya ingia hapa ufaidi muziki, vichekesho masaa 24.
Saturday, May 31, 2014
ALHAMISI MAY 31, 1990. SIKU ALIPOFARIKI HEMED MANETI ULAYA
Tarehe 31 May 1990 siku ya Alhamisi majira ya saa kumi na moja jioni, ndipo alipofariki Hemed Maneti katika hospitali ya Mwananyamala. Hemed wakati huo alikuwa ni mwanamuziki muimbaji na Kiongozi wa Vijana Jazz Band. Alikuwa ameanza kuwa na matatizo ya afya miezi kadhaa kabla ya hapo na hatimae kupelekwa Tanga kwa ajili ya matibabu. Hali yake ilipozidi kuwa mbaya alirudishwa kwa ndege kuwasili Dar Jumatano 30 May na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Mwananyamala ambapo alilala na kufariki kesho yake. Marehemu alisafirishwa kwenda kuzikwa Tanga siku moja baadae.
Wimbo wa mwisho kurekodi ulikuwa wimbo wa kufunguliwa kwa Mandela uliotungwa na John Kitime
Wimbo wa mwisho kurekodi ulikuwa wimbo wa kufunguliwa kwa Mandela uliotungwa na John Kitime
![]() |
| Hawa walikuwepo mortuary siku ya kuondoka na mwili wa marehemu kwa ajili ya kupeleka Tanga, wa mwisho kulia Mzee Jacob John, mwenye jacket jekundu marehemu Mzee Faya |
Tuesday, May 20, 2014
EXCLUSIVE- MANGELEPA LIVE ENZI ZAO HAPA WAKIPOROMOSHA EMBAKASSY
NI BAHATI SANA KUWEZA KUPATA VIDEO ZA ENZI BENDI ORCHESTRA MANGELEPA WALIPOKUWA JUKWAANI. NI VIDEO YENYE MAFUNZO MENGI KWA BENDI ZA ZAMA HIZI, JINSI WATU WACHACHE AMBAVYO WALIWEZA KUPOROMOSHA MUZIKI ULIOPANGIKA NA KUTOA SHOW NZURI. NI VIDEO TAMU KWA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI WA ENZI HIZO.....
Saturday, May 17, 2014
UNAMKUMBUKA SULTAN SKASSY KASAMBULA?
Kwa wapenzi wa muziki wa dansi wa Afrika ya Mashariki na hasa Tanzania, jina la Skassy au maarufu Sultan Skassy Kasambula si geni hata kidogo, sauti yake ilisikika katika bendi na nyimbo nyingi maarufu. Kwa sasa yuko nairobi na kundi lake la Orchestre Viva Mosukusuku, muangalie na kumsikia katika kazi yake moja kwenye video hii
Thursday, May 8, 2014
DDC MAGOMENI WAVUNJWA RASMI
Kumbi za DDC zilikuwa maarufu sana katika jiji la Dar katika miaka ya 80. Kulikuweko na kumbi za DDC Kariakoo, DDC Magomeni, DDC Keko, zikuwa maarufu kwani wakati huo kulikuwa na uhaba mkubwa wa bia, lakini katika kumbi hizi bia zilikuwa hazikauki, Pia zilikuwa kumbi maarufu kwa madansi na matukio makubwa yakiwemo masumbwi. DDC Magomeni ulikuwa kituo kikubwa cha burudani. Wiki hii ukumbi huo umepigwa nyundo na pamebaki uwanja mtupu ambao kunaelekea kutajengwa kitu. Kuna uwezekano mdogo sana kuwa nafasi hiyo itajengwa tena kwa ajili ya burudani bye bye DDC Magomeni, mengi makubwa ya muziki yalifanyika pale.
Subscribe to:
Posts (Atom)


