Tuesday, May 20, 2014

EXCLUSIVE- MANGELEPA LIVE ENZI ZAO HAPA WAKIPOROMOSHA EMBAKASSY

NI BAHATI SANA KUWEZA KUPATA VIDEO ZA ENZI BENDI ORCHESTRA MANGELEPA WALIPOKUWA JUKWAANI. NI VIDEO YENYE MAFUNZO MENGI KWA BENDI ZA ZAMA HIZI, JINSI WATU WACHACHE AMBAVYO WALIWEZA KUPOROMOSHA MUZIKI ULIOPANGIKA NA KUTOA SHOW NZURI. NI VIDEO TAMU KWA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI WA ENZI HIZO.....

Saturday, May 17, 2014

UNAMKUMBUKA SULTAN SKASSY KASAMBULA?

Kwa wapenzi wa muziki wa dansi wa Afrika ya Mashariki na hasa Tanzania, jina la Skassy au maarufu Sultan Skassy Kasambula si geni hata kidogo, sauti yake ilisikika katika bendi na nyimbo nyingi maarufu. Kwa sasa yuko nairobi na kundi lake la Orchestre Viva Mosukusuku, muangalie na kumsikia katika kazi yake moja kwenye video hii 

Thursday, May 8, 2014

DDC MAGOMENI WAVUNJWA RASMI

Kumbi za DDC zilikuwa maarufu sana katika jiji la Dar katika miaka ya 80. Kulikuweko na kumbi za DDC Kariakoo, DDC Magomeni, DDC Keko, zikuwa maarufu kwani wakati huo kulikuwa na uhaba mkubwa wa bia, lakini katika kumbi hizi bia zilikuwa hazikauki, Pia zilikuwa kumbi maarufu kwa madansi na matukio makubwa yakiwemo masumbwi. DDC Magomeni ulikuwa kituo kikubwa cha burudani. Wiki hii ukumbi huo umepigwa nyundo na pamebaki uwanja mtupu ambao kunaelekea kutajengwa kitu. Kuna uwezekano mdogo sana kuwa nafasi hiyo itajengwa tena kwa ajili ya burudani bye bye DDC Magomeni, mengi makubwa ya muziki yalifanyika pale.

Tuesday, April 22, 2014

JIKUMBUSHE ORCHESTRA SAFARI SOUND ENZI ZA MASANTULA LIVE-VIDEO




ORCHESTRA SAFARI SOUND ILIPITIA SURA NYINGI KABLA YA KUONDOKA KATIKA ULIMWENGU WA MUZIKI. KATI YA SURA HIZO NI MASANTULA, DUKUDUKU, NA NDEKULE...VIDEO HII NI KIPINDI CHA MASANTULA

Sunday, April 13, 2014

MZEE MUHIDIM MAALIM GURUMO (MJOMBA) HATUNAE TENA



Mwanamuziki muimbaji wa miaka mingi Mzee Muhidi Maalim Gurumo hatunae tena. Mzee Gurumo amefariki alasiri hii katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Mungu amlaze Pema Peponi Amin

Monday, April 7, 2014

VIDEO YA MSIBA WA PROFESA JUMA BHALO..KWA HISANI YA KTN