Saturday, May 31, 2014

ALHAMISI MAY 31, 1990. SIKU ALIPOFARIKI HEMED MANETI ULAYA

Tarehe 31 May 1990 siku ya Alhamisi majira ya saa kumi na moja jioni, ndipo alipofariki Hemed Maneti katika hospitali ya Mwananyamala. Hemed wakati huo alikuwa ni mwanamuziki muimbaji na Kiongozi wa Vijana Jazz Band. Alikuwa ameanza kuwa na matatizo ya afya miezi kadhaa kabla ya hapo na  hatimae kupelekwa Tanga kwa ajili ya matibabu. Hali yake ilipozidi kuwa mbaya alirudishwa kwa ndege  kuwasili Dar Jumatano 30 May na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Mwananyamala ambapo alilala na kufariki kesho yake. Marehemu alisafirishwa kwenda kuzikwa Tanga siku moja baadae.
Wimbo wa mwisho kurekodi ulikuwa wimbo wa kufunguliwa kwa Mandela uliotungwa na John Kitime
Hawa walikuwepo mortuary siku ya kuondoka na mwili wa marehemu kwa ajili ya kupeleka Tanga, wa mwisho kulia Mzee Jacob John, mwenye jacket jekundu marehemu Mzee Faya

Tuesday, May 20, 2014

EXCLUSIVE- MANGELEPA LIVE ENZI ZAO HAPA WAKIPOROMOSHA EMBAKASSY

NI BAHATI SANA KUWEZA KUPATA VIDEO ZA ENZI BENDI ORCHESTRA MANGELEPA WALIPOKUWA JUKWAANI. NI VIDEO YENYE MAFUNZO MENGI KWA BENDI ZA ZAMA HIZI, JINSI WATU WACHACHE AMBAVYO WALIWEZA KUPOROMOSHA MUZIKI ULIOPANGIKA NA KUTOA SHOW NZURI. NI VIDEO TAMU KWA WAPENZI WA MUZIKI WA DANSI WA ENZI HIZO.....

Saturday, May 17, 2014

UNAMKUMBUKA SULTAN SKASSY KASAMBULA?

Kwa wapenzi wa muziki wa dansi wa Afrika ya Mashariki na hasa Tanzania, jina la Skassy au maarufu Sultan Skassy Kasambula si geni hata kidogo, sauti yake ilisikika katika bendi na nyimbo nyingi maarufu. Kwa sasa yuko nairobi na kundi lake la Orchestre Viva Mosukusuku, muangalie na kumsikia katika kazi yake moja kwenye video hii 

Thursday, May 8, 2014

DDC MAGOMENI WAVUNJWA RASMI

Kumbi za DDC zilikuwa maarufu sana katika jiji la Dar katika miaka ya 80. Kulikuweko na kumbi za DDC Kariakoo, DDC Magomeni, DDC Keko, zikuwa maarufu kwani wakati huo kulikuwa na uhaba mkubwa wa bia, lakini katika kumbi hizi bia zilikuwa hazikauki, Pia zilikuwa kumbi maarufu kwa madansi na matukio makubwa yakiwemo masumbwi. DDC Magomeni ulikuwa kituo kikubwa cha burudani. Wiki hii ukumbi huo umepigwa nyundo na pamebaki uwanja mtupu ambao kunaelekea kutajengwa kitu. Kuna uwezekano mdogo sana kuwa nafasi hiyo itajengwa tena kwa ajili ya burudani bye bye DDC Magomeni, mengi makubwa ya muziki yalifanyika pale.